East Africa Television (EATV), itazindua kipindi kipya cha uchaguzi kiitwacho Uchaguzi Express siku ya Jumatatu ya tarehe 06/ 09/ 2010 saa tatu kamili usiku.

Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa hewani moja kwa moja yaani live siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kituo hicho namba moja kwa vijana, kwa lengo la kuwaelimisha vijana mambo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini.

Katika kuhakikisha vijana wanapata muamko na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu, EATV imeandaa mada zaidi ya 15 zitakazojadiliwa kwa kina ili kuwapatia ufahamu wa kutosha vijana.

Mbali na mada kipindi hicho kitakuwa na vipengele mbalimbali ili kufikisha elimu sahihi ya uchaguzi kwa vijana, miongoni mwao ni pamoja na maswali, maigizo, burudani, mashairi na sanaa ya ucheshi.

Pia kipindi cha Uchaguzi Express kitakuwa kikionyesha taarifa mbalimbali za uchaguzi mkuu zilizofanyiwa kazi na timu ya EATV, na kujadiliwa katika kipindi hicho.

Watu mbalimbali wataalikwa kutoa michango yao katika kipindi cha Uchaguzi Express, wakiwemo vijana, wataalam, wanasiasa pamoja na wadau wa vyombo vya habari nchini.

Aidha, watazamaji wa EATV wanaweza kushiriki katika hicho kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kutuma barua pepe ama kutumia blogu.

Mwezi uliopita EATV ilizindua kampeni ya kuhamasisha vijana kupiga kura yenye ujumbe “Kijana Acha Kulalamika, Tumia Kura Yako”, hii ni baada ya kufanya utafiti na kubaini vijana wengi wamekata tamaa na hawana mwamko wa kupiga kura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nadhani hakitakuwa chombo cha chama kimoja CCM kama ITV na TBC

    CCM ina Mizizi kila sehemu mara nyingi zio mizizi ya usawa

    Mtanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...