Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ushindi kwa timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) ninayofuraha kubwa kuwapa pongezi uongozi mzima wa timu yetu ya Taifa pamoja na wachezaji wetu kwa ushujaa waliouonyesha katika mechi yao dhidi ya Timu ya Taifa ya Algeria iliyochezwa siku ya Ijumaa tarehe 3/9/2010 ikawa ni kampeni za kuelekea katika kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa nini nasema ni ushujaa?
Kwa nini nasema ni ushujaa?
Ni kwa sababu ya kuweza kuonyesha mchezo safi ile hali kukiwa na uonevu ulioonekana wazi ukiwa na lengo la kukandamiza timu yetu isipate ushindi. Hakuna mtu yoyote ambaye aliyeshuhudia mechi hiyo atapingana nami eti kulikwa hakuna uonevu! Lakini matokeo tuliyoyapa yamedhihirisha ukomavu wetu katika soka la kimataifa, Pongezi zangu za dhati zimfikie kocha mkuu wa Jean Paulsen kwa kuweza kuwatayarisha wachezaji kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya uonevu na pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitampa pongezi nyingi Abdi Kassim (Babi) kwa goli zuri alilolifunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Vilevile tukumbuke haya yote ni matunda ya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuamua kuweka nguvu kubwa katika mchezo wa soka nchini naye pia nampa pongezi kubwa na ninafahamu naye anasheherekea pamoja nasi matokeo haya popote pale alipo.
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Taifa Stars Ahsanteni Sana.
Mwenyekiti - Kamati ya Operation Ushindi.
Tunawashukuru pia wanafunzi wa tanzania waliopo nchini Algeria kwa kuonyesha uzalendo mkubwa kwa timu yetu ya taifa tangu ilipowasili uwanja wa ndege ,wengi wao pia walikuwa wakija kuangalia mazoezi,hakika walitoa kampani kubwa sana na wachezaji wetu wakajiona wapo kama nyumbani!kubwa zaidi siku ya mechi pia walitoa kampani kubwa sana ya ushangiliaji! God bless zem
ReplyDeletekweli vijana wanastahili pongezi!
ReplyDeleteIla tungeomba nyie viongozi mchukue hatua zinazostahili kupeleka malalamiko kunakohusika. Sisi tunaposhiriki michezo hii tunategemea haki itendeke kutoka kwa waamuzi kwani kitendo chao ni uonevu na inavunja moyo hasa kwa wapenzi wa mchezo. Tusilalamike bila kuchukua hatua zaidi cause this behaviour has to be stopped! im sick and tired of always being mistreated when we play Arab teams!!
My next president of Tanzania. This will be a change
ReplyDeleteGabachori!
ReplyDeleteWatanzania tunaweza mpira wa maneno,mpira bado.Mie nadhani tunaitaji jitoa ktk mashindano ya nje kwasasa,nakuwekeza ktk soka academy,after 10yrs then tunaweza anza tena.
ReplyDeleteHatuwezi kuwa na Rais mfanyabiashara.Labda akagombee India
ReplyDeleteJitoeni kwa miaka 10 muone adhabu yake kutoka FIFA!!!
ReplyDeletePongezi za maneno sio ishu.
ReplyDeletePongezi plus Kampeni juu kwa juu duuuh!!bongo tamabarare
Pongezi za maneno sio ishu.
ReplyDeletePongezi plus Kampeni juu kwa juu duuuh!!bongo tamabarare