Ule mpambano wa kukata na shota wa watani wa jadi Simba na Yanga Ughaibuni sasa timu zote kuingia na uzi mpya,mpambano huu utakaochezea uwanja wa Uhuru(Meadowbrook Pk) badala ya wanja jipya la Taifa(Kalmia) ni kwa sababu Simba wamegomea kuchezea wanja hilo jipya kwa sababu wanadai ni nuksi,kwani hawajawahi kuibuka kidedea kwenye uwanja huo,uliopo mpakani mwa Silver Spring na DC.
Kambi zote ziko shwari safari hii Simba hawaongei sana kama ilivyo kwenye mechi zilizopita,inawezekana ni kwa sababu ya kuingiwa na woga na mchezaji wa kutumainia wa Simba na Stars United,Liberatus Mwag'ombe hatakuwepo kwenye mpambano huo kutokana na kukosa ruhusa ya mwajili wake.
Kwa upande wa Jangwani,wao wanaendelea na mazoezi mepesi na wapo READY kwa mpambano huo unaosubiliwa na mamia ya mashabiki Washington,DC,na vitongoji vyake.
Mtanange huu ni sehemu ya sherehe za labor Day Weekend,utachezewa Meadowbrook Park Jumapili Sept 5.
Jumamosi Sept 4 uwanja wa Kalmia kutakua na Tournament itakajumuisha timu nne,Stars United,Kenya kutoka(NJ),Kenya(DC) na MT.Zion.Mechi hizi zitaanza kwenye saa 5:30 asubuhi na kuendelea mpaka jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...