Wakazi wa kata ya Ilala katika manispaa ya Iringa wakishuhudia polisi wakiwa wamemkamata kijana mmoja ambaye alikuwa akichana picha za mgombea ubunge wa CCM Monica Mbega na zile za Jk mara baada ya kampeni zamgombea ubunge kumalizika katika eneo hilo leo jioni. Picha na Francis Godwin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Yaani mnatumia resources zote izo kumkamata mpiga picha? Mbona kuna mafisadi kibao tunaowajua ambao hamuwakamati? Polisi bwana, mara nyingine wanafanya mambo ya kitoto sana.

    ReplyDelete
  2. Wewe uliyetoa maoni hapo juu Tue Sep 14, 11:11:00 PM, umyasomasoma hayo maelezo ya picha vizuri au umerukia kutype tu mawazo yako? hebu soma japo hiki kijisehemu cha hayo maelezo ya picha ".........polisi wakiwa wamemkamata kijana mmoja ambaye alikuwa akichana picha za mgombea ubunge wa CCM ............."

    Mdau

    KCC

    ReplyDelete
  3. 1.Zote hizo ni dalili za Mama Mbega kutokukubalika, watu wanataka mchezaji wa akiba waone kama ataweza kufunga magoli ya maendeleo, dk ulizocheza MM Mbega zinakutosha mpishe mwingine.

    2.MM Mbega unatuambia eti ni heshima kwetu wana Iringa Mjini kwa ww kuwa mkuu wa Mkoa,hilo MM umechemka, hatutaki mtu aliye mbali na wapiga kura wake, miaka yote imekuwa hivyo ukiondoa mwaka 1995(Upinzani ulipokuwa madarakani) kwa wabunge kukaa mbali na wananchi safari hii imekula kwako historia inajirudia

    3. Ofisi ya msaidizi wako imekuwa kero kwa kiasi kikubwa, bora aingie mwingine tuangalie hali itakuwaje.

    4. Kitendo cha NEC kukupitisha ilikuwa ni dharau kwa Mhehe/Iringa mjini na hili unalijua fika rejea historia ya mwaka 1995.

    Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli

    ReplyDelete
  4. Sasa kosa la huyo kijana ni nini? freedom iko wapi? kwani ukichana mapicha yaliyobandikwa mitaani ni kosa au kwa vile ni za Raisi?


    Mimi nashindwa kabisa kuelewa nchi yetu ikoje na sheria zake. bado ni ubabe babe tu and pp cannot express atheir feelings at all halafu ndio mnasema kuna amani , kuna amani ...amani gani kama mabo yenyewe ndio hivyo

    Nawee michuzi najua hutaposti hii kwa vile na wewe ni hao hao tu

    ReplyDelete
  5. bora wangewakamata wezi wa TRA pole kaka wewe ndo 6 au 10 miaka sawa na mwizi wa kuku wanaozea jela wezi wa mabilioni ni 2years and back to work with transfer some place but same company tanzania shame on ourserf

    ReplyDelete
  6. Anon Hapo Juu, Sidhani Kama ni aliyekamatwa ni mpga picha ila amechana picha!!

    Sioni Kosa kosa hapo!! Kwani Uchani maana yake ni nini? Ni kitu chochote ambacho hakiko mahali pake/panapostahili. Sasa Tunajuaje hizo picha zilikua mahali gani na labda zilikua mahalli ambapo kwake yeye ni kama uchafu au ni ktk himaya yake!! Wanaochana za Chadema, Cuf..... Mbna sijasikia kuna aliekamatwa au wao za kwao kuchanwa ni haki!!??

    Msitulazimishe woote tuwe CCM!! Muachiane Mara Moja. Mfuatilie masuala ya msingi.

    ReplyDelete
  7. watu wote hawa kwa ajili ya kumkamata kijana mmoja? kweli polisi wapo kuilinda ccm.

    ReplyDelete
  8. Kama tumewaambia kwa maneno wana Iringa hatumtaki Monica Mbega hamsikii so what next ni kuchana na kutupa it away.

    ReplyDelete
  9. Mbona hao wakazi wote ni watoto? Just being curious...!!

    ReplyDelete
  10. SISIEMU MTATUMIA NGUVU SANA KUFANYA VITU VIDOGO SANA AISWEA HATA KAMA CHADEMA WATAPATA KURA MOJA SAFARI HII, BASI HIYO KURA NI YANGU.

    ReplyDelete
  11. yani kweli ccm wamefuliaaaaaaaa,picha za chadema,cuf zimechanwa hatujaona polisi wakiwakamata,na nyie polisi angalieni mnaikumbatia ccm halafu ndo hao wanakupeni mishaara mbuzi,ppfffuuuu

    ReplyDelete
  12. nshimimana aka dumisaneSeptember 15, 2010

    mtu amechana picha, mnakuja na bunduki, kweli Juma Nature alisema kweli.. mi nilidhani anatania!

    nikikumbuka nacheka, nikisahau nalia!?

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  13. Kawasaidia Kutowa Picha jamani kampeni mshaandika zimeisha sasa mnataka nini? ah Chi Che Mi bwana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...