Ridhiwani Kikwete akiwa na mwalimu aliyemsomesha darasa la kwanza 1987 katika Shule yaMsingi Matangini Mwl. Sophia Makong'o, alipomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea. Kulia ni mtoto wa Mwl. Makong'o, Husna, ambaye alisoma naye Ridhiwani darasa la kwanza katika shule hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa Ridhiwani Kikwete akiongea na wanafunzi wakati alipotembelea Shule ya Msingi Matangini iliyopo Nachingwea,Mkoa wa Lindi, aliyosoma darasa la kwanza mwaka 1987, wakati huo babake, Rais Jakaya Kikwete akiwa Katibu wa TANU wilayani humo.
Ridhiwani akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo


Ridhiwani akifurahia na wanafunzi wa shule hiyo




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. uncle misupu, hivi TANU bado ilikuwepo mwaka 1987?? au ulimaanisha katibu wa CCM..

    ReplyDelete
  2. Aisee Michuzi umenikumbusha home.. Yani Nachingwea pale miembeni ndo nyumbani penyewe hapoo .....amaa

    ReplyDelete
  3. Huyu kijana ana matatizo kichwani, na anahitaji msaada wa ushauri nasaha wa haraka, vinginevyo huko tuendako tutaona vioja vyake vingi!!!

    ReplyDelete
  4. NATAKA NIFANYE UTAFITI HUO MDA ALIOPIGA PICHA NA HAO WATOTO WA SHULE ILIKUWA SAA NGAPI. MAANA KAMA ILIKUWA NI WAKATI WA VIPINDI KUNA KILA SABABU YA KUWAWAJIBISHA HAO WAALIMU KWA KUMRUHUSU MPITA NJIA KUINGIA DARASANI KUWA SUMBUA WATOTO WAKATI WA VIPINDI.

    ReplyDelete
  5. BIG UP RIDHIWANI.TUWE TUNAPELEKEA ANGALAU VIFAA VYA MICHEZO KATIKA MASHULE TULIKOSOMA WAJAMENI!

    ReplyDelete
  6. Hivi baada ya kumtembelea mwalimu wake ambaye anaishi katika mzingira duni.. angalia kitanda cha telemka tukaze.. yeye na chama chake wana mpango gani kuwainua watumishi kama hawa ambao wamejitoa mhanga kuwapa elimu hadi wafanikiwa?

    ReplyDelete
  7. Sasa bwana Ridhiwani inabidi amchumbie Husna,manake mtoto anaonekana mrembo,

    ReplyDelete
  8. CCM ilizaliwa huko zanzibar 1977/1978 kama sikosei. Hizi habari zinakanganya. Halafu unataka kunambia Kikwete alikuwa katibu wa TANU 1987? Mmmh hawa ndo wale wale.

    ReplyDelete
  9. Ridhiwani, toa asante kwa mwalimu wako kama vile kumnunulia angalau pea moja ya viatu. Utapata baraka huko mbele.

    ReplyDelete
  10. Ukiiangalia picha ya kwanza inaeleza mengi. Mwalimu Makong'o na bintiye wanaonekana kama watu ambao walikuwa hawataki kupiga hiyo picha ila kuna wanakiogopa ndio maana wakakubali.

    ReplyDelete
  11. mambo mengine hayana umuhimu kuyaweka public this like uzalilishaji flani vile. ni kama dogo anatuambia oneni maisha yangu yalivyotofauti na ya wengine. let us be realistic.

    ReplyDelete
  12. Huyo Rizwani kama hajaoa namshauri amuoe huyo binti wa Mwalimu wake.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  13. najua kuna comments nyingi zimebanwa sitopoteza mda kutoa maoni yangu.

    ReplyDelete
  14. Duuuhh hii imenikumbusha enzi za marehem Saddam Hussein na watoto wake Qusay na Uday Hussein,ilikuwa imefanana kihivi.

    ReplyDelete
  15. Hivi Ridhiwani kikwete ndo mjumbe pekee wa baraza la utekelezaji la umoja wa vijana?Baraza hili lina wajumbe wangapi? yale yale ya Omar Bongo? familia hii ina viongozi wangapi?tusipoangalia tuarudi kwenye unyalubanja sasa hivi? na Madaraka Nyerere, Vicent hatukuwasikia kipindi cha mwalimu.Katiba ya nchi sasa ionyeshe mwisho na mipaka ya madaraka ya familia ya rais Kikwete huu ni uswahili, hata Mkapa hakufanya haya.Mwalim Nyerere fufuka uone haya.
    Mdau, mpenda maendeleo ya Tanzania.

    ReplyDelete
  16. Amaaa bwana wewe wa miembeni ,mi wa posta pale,ulijumushila?Ngunjaaaaaaaa hatariiiiii.

    ReplyDelete
  17. amaaa ulijumushilaa, abali ingine? Wee aloo ngunja ile atalii, mimi kummiss nyumbani uko atalii bwana wewe ....amaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...