mambo vipi kaka Michuzi,

naomba uiweke hii katika Globu ya Jamii ili wadau waweze kuipata na kuifanyika kazi.

Siku za hivi karibuni kumetokea habari kuhusu mwanya uliopo kwenye Adobe Acrobat na Adobe Reader ambao unawawezesha mahacker kutengeneza code na kuziweka kwenye mtindo(format) wa pdf huku wakizipamba kwa jina zuuuuri,pindi ufunguapo tu basi imekula kwako kwani hizo code zitajirun na kushusha minyoo na virusi kwenye kompyuta yako itakayomuwezesha hacker kuitawala kompyuta yako bila wewe kujua.

Hii ni hatari mno kwani wengi wetu tumekuwa tukiamini kuwa hauwezi kukutana na virusi au minyoo kwenye faili kama la Adobe.

katika kukabiliana na hili Adobe wametoa ushauri wa kiusalama kwa watumiaji wawe makini katika kipindi hiki wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo.

AfroIT inawashauri wanajamii kuwa makini la hili pia kufuata ushauri uliotolewa na Adobe APSA10-02, Vilevile unaweza kutumia Microsoft's Enhanced Mitigation Toolkit (EMET) ambayo inakuwezesha kujilinda na uvamizi kama huu ambao kwa lugha ya kitaalamu tunauita uvamizi wa siku ya sifuri(Zero-day exploit),hii ikimaanisha mianya ayopatikanika kwenye programu bila mtengenezaji kujua.

Unaweza kupata maelezo ya ziada kwa kutembelea Microsoft Security Research and Defense blog.

Timu nzima ya AfroIT itakuletea update pindi mbalimbali za masuala ya kiusalama. Kwa masuala mbalimbali ya ICT tembelea AfroIT.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ahsante sana mdau kwa habari nzuri kama hizi kwa sisi watumiaji wa kompyuta. Tafadhali usichoke kutuhabarisha!!

    ReplyDelete
  2. Thanx,ni vema kuona habari nzuri kama hizi,kuliko ccm vijijini.

    ReplyDelete
  3. ahsante sana kaka...tunaomba utuelezee kuwa kuna virus gani ameattack server za zain na voda na kusababisha watumiaji wa cell phones kupata message za vifo??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...