kinogozi wa wanafunzi wa kitanzania nchini Algeria,Habibu H.Ruhombo (pili kishoto) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngasa (pili kulia) na nyanda namba 2 wa Stars,Jackson Chove (kushoto) pamoja na mdau wa huko Algeria walipokwenda kuwapokea airport.
Taifa stars ikiwasili uwanja wakimataifa wa Algiers taya kwa kuelekea kwenye usafiri maalumu walioandaliwa na wenyeji wao katika ulizi mkali wa viosi vya usalama.
mashabiki wakiimba nyimbo za hamasa wakati timu yetu ya Taifa ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Algiers kwa ajili ya mpambano wao na wenyeji Algeria uliopigwa usiku wa kuamkia leo na kutoka sare ya bao 1-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. kwa mwendo huu tutafika, Nimeangalia match viungo wa kati akuna. walikuwa wana karibisha mashambulizi langoni mwao viungo wakati kulikuwa akuna kabisa. pia nazani goalkeeper hatuna
    tungeweza shikilia goal moja na kushinda goalkeeper angekuwa pia. ONgereni fanyeni marekebisho mlipo kosea. then chezeni match kama hizi na waarabu si na wakenya match na wakenya uganda hatujifunzi chochote

    ReplyDelete
  2. safi sana ndugu zetu mlio kuwa huko hiyo amasa mlio ionyesha ndio iliyo sabababisha wachezaji wetu kujiamini

    ReplyDelete
  3. wadau hapo mmefanya jambo la kizalendo sana kwenda kuipokea timu yenu...safi sana..

    ReplyDelete
  4. MAMBO KAMA HAYA NDO YANATAKIWA, KUWA NA IMANI NA TIMU NI KITU SAFI SANA. YAANI WENZANGU WATANZANIA WAISHIO HUKO WALIJUA STARS INAWEZA KUWATOA NISHAI, YAANI NIMEFURAHI SANA. MAPOKEZI WALIOWAPA VIJANA NI MAKUBWA! NA VIJANA NAO WAMA-PAY BACK SHUKRANI!
    WE R READY FOR FIFA 2014, VIVA STARS. BAHATI YAO WAMEPONEA CHUPUCHUPU, WAKIJA BONGO WATACHEZESHWA MCHAKAMCHAKA TENA GEMU NAJUA LITAANZA SAA SABA MCHANA KUBABAKE!!

    ReplyDelete
  5. Kwa mtoa hoja wa kwanza. Timu yetu ilicheza 4-2-3-1. Kwa jinsi walivyocheza ni matokea ya mfumo huo. Muda mwingi wa mchezo mtakuwa mnashambuliwa kwa sababu mna mabeki wanne na holding mid wawili. Uzuri wa mfumo huu ni wakati mnashambulia ni rahisi sana kufunga. Kama uliangalia vizuri Netherland kwenye kombe la dunia walikuwa wanatumia sana mfumo huu ila uzuri wao wana mtu mmoja anayeweza kufanya vitu peke yake. Kwa ujumla nadhani mfumo unaweza kutufaa ila inabidi tutafute kipa na mtu mmoja mbele kwenye uwezo.

    ReplyDelete
  6. nimesoma hapo juu kuwa Watanzania waishio Algeruia waliimba nyimbo za kuhamasisha wachezaji. Je nymbo hizo ni zipi huenda wakaja nchi ninayoishi mimi ningependa kuwaimbia hizo nyimbo.

    ReplyDelete
  7. huyo mdau asie na jina anaitwa Juma Ahmed.

    -Mdau Ukerewe

    ReplyDelete
  8. Nikiwa mmoja wa waliokuwepo 'ndani ya nyumba' wakati wamatumbi wanakiyumbisha na kuotesha mbawa kibarua cha kocha Saadane wa 'L'Equipe National d'Algérie', napenda kuwahakikishia kuwa timu yetu ni nzuri na imeweza kuhimili makali ya wenyeji hasa wachezapo katika uwanja wa Mustafa Tchaker Blida ambao ni uwanja wao wa ushindi/ndumba (ndio, wao pia wana maimani pori, ha haa).

    Kulikuwa na mbinu mwitu kibao ambazo walizitumia, aidha katika kuspy maandalizi ya timu yetu kwenye mazoezi au dhidi ya washabiki wetu kiduchuu waliohudhuria au kudhamiria kuhudhuria (wengine walidhoofishwa kuja uwanjani kwa mbinu mwitu).

    Enewei, pamoja na hayo yote mapleya wetu walikuwa ngangari kama mlivyoona, na masapota pia waliwafunika wanyeji kwa muda wote tuliokuwamo pale uwanjani. Walikosa uchangamfu kabisa pamoja na uwingi wao na staili yao ya ushangiliaji.

    Anony wa Tarehe Sun Sep 05, 03:16:00 AM, kwa kweli una hoja. Hatuna wimbo rasmi wa kushangilia Taifa Stars. Hiyo ni homework ambayo pengine inabidi tuwape 'UTITIRI WA WASANII' ulioko bongo na sehemu nyingine kuutafuta. Sisi tulukuwa tunaungurumisha wimbo wowote tuu uliokuwa una kuja, kama kimanu manu, Oooh kidedeaaa,kukata mapanga pamoja na nyingine nyiiiingiii. Pia tuliwakaanga na mafuta yao wenyewee ya '1-2-3 Viva L'Algérie', tukachenji na kuimba 1-2-3 Viva la Tanzanie!

    Tunaomba timu ipokelewe vyema nyumbani. Ni mwanzo mzuri. Kila mtu aisapoti timu yetu. Tunashukuru kwa kushirikishwa.

    Mdau, Algiers - Algeria

    Viva

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...