Novatus Makunga,Arumeru
Mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Goodluck Joseph Ole Medeye ameahidi kuimarisha mfuko wa maendeleo wa jimbo kwa kuhakikisha wananchi wote kutoka wilaya hiyo waliosambaa sehemu mbalimbali duniani wanachangia.
Alisema kuwa lengo la mkakati huo ni kuuwezesha mfuko huo kutatua kero mbalimbali badala ya kutegemea kodi na fedha za serikali.
Ole Medeye alitoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika uwanja wa Ngaramtoni na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi ambao waliongozwa na msururu mrefu wa magari na pikipiki kuanza makao makuu ya chama hicho eneo la Sekei
Alibainisha matatizo yanayohitaji mkakatati wa haraka wa mfuko huo kuwa ni pamoja na shida sugu ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mengi ya jimbo hilo pamoja na kwamba jimbo hilo lipo karibu na mlima Meru
Ole Medeye ambaye pia ni kamanda wa umoja wa vijana (UVCCM) wilayani Arumeru alisema kuwa mlima huo ndiyo wenye vyanzo vingi vya maji ambayo yanatumika katika jiji la Arusha pamoja na wilaya jirani ya Monduli
“Lazima tuweke mkakati wa kushughulikia tatizo la mabomba kukatisha katika jimbo letu yakipeleka maji katika wilaya ya Monduli huku hapa maeneo mengi yakiwa na tatizo la maji,”alisema
Alitaja matatizo mengine kuwa ni pamoja na ukosefu wa barabara ambazo zinaweza kutumika katika vipindi vyote vya mwaka na kuahidi kuwa uimara wa mfuko huo utawezesha jimbo kuwa na barabara bora kiangazi na masika
Akizundua kampeni hizo mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Arusha Yonah Nnko alisema kuwa anaamini aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka kumi na tano,Elisa Mollel atamsaidia ole Medeye katika kampeni na hatimaye kuibuka na ushindi wa kishindo.
“Mollel ni mbunge ambaye amefanya kazi kubwa hapa jimboni na pia ni msomi na mtu ambaye anajiweza kiuchumi hivyo sina shaka naye kabisa katika kushiriki katika kampeni hizi,”alisema.
Hata hivyo Mollel ambaye alishika nafasi ya tatu katika kura za maoni kwa kupata kura 2,603 pamoja na mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya ambaye alishika nafasi ya pili kwa kura 6,715 maoni ndani ya chama hicho hawakuhudhuria uzinduzi huo wa Ole Medeye aliyepata kura 7,481.
Ole Medeye anatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa mgomba wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia(CHADEMA),Mathius Ole Kisambu ambaye hata katika uchaguzi wa mwaka 2005 alimpa shida kubwa sana Mollel kwa kupata kura 33,593 dhidi ya 57,397
Katika uzinduzi huo imejidhihirisha kwamba aliyekuwa mpinzani wa karibu wa Mollel katika kura za maoni za mwaka 2005 kanali mstaafu Mika Metili ndiye mshauri mkuu wa Ole Medeye katika kampeni zake.

hakuna jipya hapo, mtu ana roho mbaya na ngumu kama paka. sijui utaendelea na kamchezo kako hadi huko bungeni? yetu macho. michu nawakilisha
ReplyDeletewacha aende bungeni akakutane na wababe wenzie siyo kuonea watu wapole. Mungu waangazie wote waliopitia manyanyaso ya huyu bwana.
ReplyDeletebora aondoke. nashukuru Mwenyezi Munguu kusikia kilio changu
ReplyDeleteMMASAAAAIIII, WALE WALE AKINA LOWASSA
ReplyDeletembona bro michu hautouonyeshi umati wa watu??? au walikuwa wachache????
ReplyDeletemmmh, huyu baba mbona kakunja uso? kazi kweli kweli, anonymous hapo juu, pole sana ndiyo dunia hiyo
ReplyDeleteMadeye ha ha ha ha , watakukoma bungeni mwaka huu ha ha ha. ila jaribu kuwa mtu mzuri kwa watu, kama unajua atakayekuzika endelea hivyo hivyo, sehemu unayoenda ni hatari
ReplyDeleteAll the best madeye but mhhhhhh ....
ReplyDeleteWe michu kumweka huyu bwana unatafuta uchokozi na watu... ila pole sana kwa anonymous hapo juu, Mungu ni wa haki ipo siku atakusaidia. pole sana ilishawahi kunitokea na mimi huku uingereza, this world is unfair ila mtegemee Mungu
ReplyDeleteMbeba box,
Reading
Mmmh watu wanaocomment humu wako makini kweli. yani nimeshangaa kufungua comments na kuona hivi, yani ni ukweli mtupu mpaka naogopa. ila turespect kila mtu jamani.siyo vizuri kuishi vibaya na watu
ReplyDeleteNahisi bunge lijalo watu watachapana makonde ukumbini kama Taiwan kama wagombea wenyewe hi hawa.
ReplyDeleteKaaaaaaz kwel kwel!!!
ReplyDelete