Balozi mpya Mh. Kalaghe (mwenye miwani) kwa mara ya kwanza amekutana na viongozi wa jumuiya za watanzania UK kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Katika kikao hicho viongozi wa jumuiya hizo wa taifa na wale kutoka mikoani walikutana ili kumfahamisha mheshimiwa majukumu yaliyopo katika utaratibu wa kushirikiana kati ya wananchi waishio Uingereza, uongozi wao na ubalozi pia.

Aidha katika kikao hicho, mheshimiwa Kalaghe alitoa ahadi ya kutoa ushirikiano wake wa dhati wakati wowote.

Baada ya hapo mheshimiwa tawakutana na watanzania waiushio nchini hapo kwa nyakati tofauti kama itakavyoelezwa hapo baadaye.

Umoja ni nguvu

Ofisi ya mawasiliano TANZ UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Karibu balozi Kallaghe na fikra zako.

    ReplyDelete
  2. Mh. Balozi unakaribishwa katika eneo lako jipya la kazi. Lakini tunashangaa kuona Balozi na JUMUIYA YA Watanzania bila hata Benedera ya Utaifa wenu?Tulizoea sana kuona mambo mazuri sana tena ya mfano wakati Balozi Maajar akiwakilisha Tz Uingereza. Tafadhali muendeleze mazuri yaliyoanzishwa na Balozi MAAJAR NA WENGINE KOKOTE MLIPO TUITUMIE VIZURI NAFASI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WENGINE. MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...