JK akijiandaa kumkabidhi Mh. Fatma Maghimbi kadi ya CCM baada ya kutangaza kujiengua chama cha wananchi CUF katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Tanganyika Packers vya Kawe jijini Dar leo
JK akimkabidhi kadi ya CCM Mh. Juma Othman Jumaambaye pia alitangaza kujiengua CUF leo
Wah. Juma Othman Juma na Fatma Maghimbi wakifurahia kujiunga na CCM leo
Mwenyekiti wa kampeni wa CCM Mh. Abdulrahman Kinanaakimpongeza Mh. Juma Othman Juma kwa kujiunga na CCM leo
Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za CUF na kuchukua za CCM leo jimboni Kawe jijini Dar es salaam na kuahidi wenzao wengi watafuata nyayo zao kutoka CUF.
Akielezea sababu zake za kurudi CCM, Juma Othman Juma amesema ameguswa kwa kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Kikwete Tanzania Bara na Visiwani hususan aliporejesha amani na utulivu visiwani Unguja na Pemba kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.
"Lakini sasa napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Kikwete kwa kurudisha heshima ya nchi yetu duniani kwani mwaka huu wa kampeni, hakuna hata mmoja aliyehama visiwani humo kukimbia uchaguzi" alimaliza Juma Othman akishangiliwa na umati mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mama Fatma Maghimbi amewahi kuwa waziri kivuli wa Katiba na Sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mbunge wa Chama Cha Wananchi CUF. Naye Juma Othman Juma amewahi kuwa muanzilishi wa Chama Cha Siasa visiwani kabla ya kujiunga na Chama cha Wananchi CUF.

Sisi Wabongo kweli tutaendelea kubaki nyuma milele,wache wakenya watuite mazoba,wewe Maghimbi na Othman hamujui kuwa upinzani mzuri ndio unaoifanya serikali iongoze kwa umakini?Na bado hamujajua kuwa Cuf zanzibar munaotupa hope ya future democrasy,kweli Bongo imeoza.
ReplyDeleteNa wewe michuzi CCM,usikunje hii comments
Mdau Istanbul
CHADEMA mpooo... hampo.
ReplyDeleteMdau wa Instanbul,Hao waheshimiwa wametupwa na CUF,na unajua SIASA ni ajira kwa nchi zetu hizi,sasa WAKALE wapi hawa???,wesha vuta AJIRA upande wa pili,MAISHA YANASONGA kama kawa.
ReplyDeletenawasikitikia sana hawa wawili; na hasa kwa wakati huu wakati almost CUF Zanzibar wanaiona bandari! lakini upande mwengine ni bora walipotoka mapema kwasababu CUF Zanzibar wakishika serikali ni uwajibikaji na kazi mtindo mmoja! watu wasio na usimamo kama hawa hawatakiwi.
ReplyDeletemsiwalaumu jamani, wenzetu wanafata kula!
ReplyDeleteHivi we wafikiri watala nini na cuf hawana uongozi,usitoshe unaelalama kama sio wewe nduguyo kafoji vyeti anatafuta kazi ili ale. waachaeni msiwazonge hii ni siasa tuuuuuuuu. hata Slaa mwenyewe aweza rudi ccm akikosa kula chadema. Hamuoni viongozi wa CCJ walitoka wapi na wameenda wapi ni kula tu ndio mihangaiko yote hiyo.
ReplyDelete