Marehemu Syllesaid Mziray 'Mwanangu'


HABARI ZIMEINGIA ASUBUHI HII ZINASEMA SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA AKISUMBULIWA N MALARIA. HABARI ZA MIPANGO YA MAZISHI ZITAFUATA MARA TU BAADA YA KUPATIKANA.


COACH MZIRAY , ALIYEKUWA MWAJIRIWA WA CHUO KIKUUU HURIA KAMA MHADHIRI, ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI SOKA KATIKA VILABU MBALIMBALI HADI TIMU YA TAIFA ILIYOSHINDA UBINGWA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. ALIFUNDISHA PIA PILSNER, SIMBA, YANGA, PAN AFRICAN NA KABLA YA MAUTI KUMKUTA ALIKUWA MWALIMU WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA WA KLABU YA SIMBA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA MSIBA HUU MZITO AMBAO NI PIGO KWA TASNIA YA MICHEZO NCHINI UKIZINGATIA TUNA MAKOCHA WACHACHE WALIOSOMEA FANI HIYO NA KUBOBEA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALA PEMA PEPONI
- AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Poleni sana wanafamilia na marafiki wa Super Coach. Nilikuwa Agakhan kama wiki iliopita nikabahatika kumuona Super Coach. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi na nikiwa kama mwana Simba naungana na wanamsimbazi wenzangu katika maombolezo haya.

    ReplyDelete
  2. Rest in peace my PE instructor.

    ReplyDelete
  3. i.w.r kwake Allah ndiko tulikotoka na kwake ndiko marejeo..Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira familia ya Al marhoum Sylersaid Mziray

    ReplyDelete
  4. Du, kweli duniani tunapita, poleni sana familia, wapenda michezo wote Tanzania, kaka nitakukumbuka kipindi cha maximo timu ikicheza vibaya ulivyokua unamrushia maximo wa watu makombora ya wazi2, mungu akuweke mahali pema peponi na akupunguzie adhabu ya kaburi. Amen.

    ReplyDelete
  5. Rest in peace Big man

    Mjussi

    ReplyDelete
  6. RIP Mziray!

    Na wakuda wengine watasema eti Yanga imemuua! Sam pipo bwana, agh!!!

    ReplyDelete
  7. Mziray is behind Tanzania soccer developments, he will be remembered by children, youths and the old. "We are from the almighty, and back to him we return.

    Baba Ochu Jr
    Mpendae, Z'bar.

    ReplyDelete
  8. Mziray alinifundisha "Sports Journalism" pale Mlimani. Mtu mzuri na msomi makini aliyetumia taaluma yake kwa faida ya wengi.

    Apumzike kwa amani!!!

    ReplyDelete
  9. Abiola Jr. New Albany, OhioOctober 30, 2010

    Poleni wadau wote wa soka huko nyumbani TZ.
    Ankal, huyu jamaa pia aliifundisha kwa mafanikio makubwa klabu ya African Sports ya Tanga (Wana Kimanumanu) hadi kuchukua ubingwa wa nchi.

    R I P Super Coach

    ReplyDelete
  10. RIP Supercoach.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  11. Poleni ndugu na jamaa wa marehemu mziray

    ReplyDelete
  12. yaani nimeshtuka sana, namkumbuka ndugu yake ali mziray nilimdate saa niko mdogo alinisumbua kweli tete

    poleni wafiwa

    ReplyDelete
  13. Kusema ukweli katika maisha yangu ya kuipenda soka ya Bongo, Mziray ndo kocha pekee niliona alikuwa na uwezo wa kufundisha na kubadilisha mwelekeo wa soka. Mungu amlaze mahara pema peponi...

    Amen

    ReplyDelete
  14. Inalilah wainalilah Rajoiun!!! Eeh mola msamehe madhambi yake yote na umpokee mahala pema peponi amiin. Kweli wapenzi wa soka tutakukumbuka sana na tunakuombea kheri muda wote.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  15. Rest in Peace Super Coach Mziray.

    ReplyDelete
  16. Mziray was so vibrant, charismatic and an excellent sportsman. We'll all miss him.

    ReplyDelete
  17. Du, huyu mheshimiwa apumzike kwa amani. Nakumbuka mwaka tisini alivyohama Simba na kwenda Yanga, basi ilikuwa kilio kwa Simba maana Simba walibamizwa 3-1, huku Gaga akikosa penalti kwa upande wa Simba. Kapumzikw kwa Amani

    ReplyDelete
  18. Rest in peace coach. Tutakumbuka makala zako za changamoto za masuala ya michezo. R.I.P.

    ReplyDelete
  19. RIP Super Coach.
    Namkumbuka sana kwenye mechi ya Simba na Yanga Zenji, ambapo Coach alipigwa nyekundu, paka mweusi alitokea uwanjani na Mwakalebela akakosa Penalti. Natamani tungekuwa na paka wawili kwani tungechukua kombe siku ile.

    ReplyDelete
  20. r.i.p. Super coach, Mungu aipokee roho yako. Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...