Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Bahi, Omar Baduwel, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo wakati alipofanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akivua kofia yake na kumvisha Kijana, James Charles wakati akifurahia ngoma ya asili ya Kikundi cha Vijana cha Chomamoto wakati alipowasili Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.Picha na Muhidin Sufiani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nina masuali matatu kwako michuzi.

    1. Hivi ni ccm peke yao wanaoendesha kampeni za uchaguzi?
    2. Ikiwa CCm wanajiamini sana na kwa vile wamekuwa madarakani miaka tele, hivi kweli wana haja ya kupoteza mamilioni yote haya kwa kufanya kampeni? au wanajua kama wanahatari ya kupoteza serikali mara hii?
    3. Wakati Kikwete na viongozi wake wako bize na kampeni hizi, ni nani anaeiongoza serikali kwa wakati huu? maana na kila kukicha wanaonekana wanafanya kampeni sehemu tafauti tanzania.

    ni hayo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...