JK akisikiliza kwa makini wakati daktari wake, Profesa Janabi, akichukua maelezo ya mzee Msiani Msisi (Kushoto) ambaye ana matatizo ya mguu wa Kushoto. Mzee Msisi anatumia mguu wa bandia aliopatiwa na JK. Hapa ilikuwa ni baada ya JK kuhutubia mkutano wa kampeni huko Kibaha mkoani Pwani leo.
wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi,wakiwa wamejichora mwilini maandishi ya CCM na KIKWETE wakati JK akihutubia mkutano wa kampeni leo Kibaha mkoani Pwani.
Umati mkubwa ulijitokeza kumsikiliza JK leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi ni kwanini raisi wetu anapenda kumsaidia mtu mmoja mmoja? Na mimi babu yangu ana matatizo kama hayo... Hii inaonyesha udhaifu labda hamna sera za kusaidia jamii nzima au hana imani na mfumo ulioko ambao angeweza badilisha. Michuzi usiibanie hii najua una tabia hiyo.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la Bongo watu bado wanafikiri siasa ni ushabiki kama wa Simba na Yanga.Kwa mfano,hata Yanga ifungwe mara mia na magoli mia na Simba ushabiki wa Yanga unabaki pale pale.

    Siasa inatakiwa isiwe hivyo, Siasa ni nyanja muhimu kwa maendeleo ya Taifa. Watu wakifanya ushabiki kwenye siasa nchi itabaki imesimama tu. Watu wanatakiwa wawe na akili za kuchambua hali ya maisha yao ya kila siku na kupima ni jinsi gani viongozi wanaomba uongozi wanaweza kuwasaidia kuinua maisha yao. Sio kuchagua tu viongozi kwa hisia za kishabiki.

    Wanapiga kura ndio waajiri wa viongozi. Hii ina maana kuwa viongozi ni wafanyakazi wa wanapiga kura. Katika hali ya kuwaida mwaajiri anapotaka kuajiri mfanyakazi lazima afanye usaili. Na huwa anachagua yule ambaye ameonyesha ana uwezo zaidi ya wengine. Na ikitokea baada kupewa kazi huyo mfanyakazi akashindwa kufanya kazi ile alipewa basi mkataba wake unafunjwa au hataongezwa muda. Hivyo ananyimwa kazi na anapewa mfanyakazi mwingine.

    Hivyo kama viongozi wamepewa nafasi watafanya kazi kweli kweli la sivyo watakuja kunyimwa uongozi kwenye uchaguzi unafuatia.

    Hivyo ndivyo watu kwenye nchi zilizopiga hatua kwenye maendeleo wanafanya. Angalia Marekani, Uingereza, Japani, Ufaransa, Ujerumani n.k.

    ReplyDelete
  3. Tanzania kweli watu hawana la kufanya! kujichora kote huko na kupoteza vijipesa vyao kununua sare pamoja na kupoteza muda wao badala ya kufanya ya maana utafikiri ccm itawakumbuka baada ya kupata kula zao? oh samahani ni kura!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...