Ukitaka kuona video ya mji huu
mkongwe ulioko mkoani Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mikindani ni mji gani na upo wapi? Hebu tupe basi full intro wengine tulikimbia geographic

    ReplyDelete
  2. Si rahisi kuamini kuwa kuna Mtanzania amabaye hajawahi au haujui mji wa Mikindani kwakuwa historia ya Tanzania inautaja sana mji huu. Vinginevyo, labda mdau anafanya masihara. Kwa vyovyote vile iwavyo:

    Mji wa Mikindani ilikuwa bandari kwa ajili ya kusafirishia watumwa waliokuwa wakikamatwa katika uknda wa kusini kuanzia Malawi/Zambia/Kongo....hadi pwani ya kusini ya Tanganyika/Tanzania. Mandhari ya mji huu yanafanana sana na ya Bagamoyo. Wakazi wake wa asili ni mchanganyiko wa Waarabu na Wamakonde. Kwa sasa unakaliwa na Wamalaba, sehemu ya kabila la Wamakonde.

    Mji huu uko kilometa chache kutoka mjini Mtwara. Mji huu ni miongon m vivutio muhimu sana vya kitalii wa kitamaduni na kimazingira ambavyo, kwa bahati mbaya sana, serikali yetu, kwa miaka mingi, imeshindwa kuuendeleza. Mandhari ya Mikindani ni mazuri sana kiutalii. Mji huu unakbiliana na Bahari ya Hindi na mikondo ya bahari huingia hadi ndani ya mji hivyo kutengenza mandhari nzuuri sana.

    Mji huu ungekuwa Brazil, Marekani, Ufaransa, basi ungekuwa maarufu sana duniani. Mandhari yake ni ya kipekee, kwa hakika.

    Kuthibitisha haya, jipe fursa na panua jiografia kwa wewe mwenyewe kenda pale.

    ReplyDelete
  3. Thanks lakini amini usiamini mimi nilikua sijuijui ndio maana nimeuliza. na anilizania uko Zanzibar. Nmzawa halisi lakini hiyo mikindani ilinipita ...I don't remember...

    Na asante kwa maelezo yako nikija bongo this time nitajitahidi niende huko. Mikoa ya kusini sijafika na hiyo ni moja ya mambo nataka niende nikakuone...

    Na sio lazima ungekua Brazil ...Kama uliona ziara ya President Obama Ghana..eneo lao ambalo walikua wanapitishwa watumwan ni baaabu kubwa. Nilibaki mmdomo wazi. Siye tumelost sana..Hatujui thamani ya nchi yetu...tuna rich country lakini tunashindwa kuitumia....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...