YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.
Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-
1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa Zanzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)
2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:-
Na.
HALMASHAURI KATA
1 Newala DC Mtonya
2 Mbulu DC Endegikot
3 Manyoni DC Kitaraka
4 Same DC Kisiwani
5 Kibaha DC Janga
6 Rufiji (a)Kibiti
(b) Chemchem
(c) Ngorongo
(d) Kipugira
(e) Mjawa
7 Uyui DC (a)KIgwa
(b)Ibelamilundi
8 Sikonge Kisanga
9 Njombe Mji Mwema
10 Ulanga DC Msogezi
11 Karagwe DC (a) Kimuli
(b) Kamuli
12 Kasulu Kitagata
13 Chato DC Buseresere
14 Mwanza (Jiji) (a) Mkuyuni
(b) Mirongo
3 Manyoni DC Kitaraka
4 Same DC Kisiwani
5 Kibaha DC Janga
6 Rufiji (a)Kibiti
(b) Chemchem
(c) Ngorongo
(d) Kipugira
(e) Mjawa
7 Uyui DC (a)KIgwa
(b)Ibelamilundi
8 Sikonge Kisanga
9 Njombe Mji Mwema
10 Ulanga DC Msogezi
11 Karagwe DC (a) Kimuli
(b) Kamuli
12 Kasulu Kitagata
13 Chato DC Buseresere
14 Mwanza (Jiji) (a) Mkuyuni
(b) Mirongo
Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.
Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.
(Rajabu R. Kiravu)
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi


.jpg)
Wameshaanza mazingaombwe!
ReplyDeleteHuu ni uzembe wa Tume ya Uchaguzi na Makosa makubwa sana kuahirisha uchaguzi bila sababu ya msingi. Najua maandalizi ya uchaguzi yalianza muda mrefu sana na idadi ya wapiga kura iwe ya Marais, Wabunge, Madiwani n.k inajulikana kwa muda mrefu sasa. Iweje leo tuambiwe kuna upungufu wa makaratasi ya kupigia kura? Hii inaashiria nini? Tume ninaomba sana tuwe makini sana katika masuala ya uchaguzi maana ni suala nyeti sana....
ReplyDeleteHon Rajabu Kiravu, at least you should have shown the minimum courtsey and decency of apologising to the electorate in general and the involved constituents and wards in particular. Maneno ASANTE, SAMAHANI, POLE na TAFADHALI ni muhimu sana katika maisha. Tafadhali anza kuyatumia japo uzeeni.
ReplyDeleteKama kawaida yetu ngozi nyeusi...zoezi la uandikishaji wapiga kura lilifungwa mapeeema kwa kujihadhari na mambo kama haya lakini kwa muda woote wa maandalizi ndo tunakumbuka leo kwamba tulikosea hesabu kati ya waliojiandikisha na idadi ya karatasi tunazopaswa kuzipeleka......
ReplyDeletemsemo huu wanipa burudani ya kutosha...."Pole pole ndo mwendo hatimaye tutafika huko tunakoelekea....."
Nitafanyaje sasa wacha niendelee kujivunia uafrika wangu
AISEE HUU NI UZEMBE WA HALI YA JUU. WATU WAMEJIANDIKISHA SIKU NYINGI. IDADI YA WALIOJIANDIKISHA INAJULIKANA TANGU SIKU NYINGI ZILIZOPITA. IWEJE SIKU 1 KABLA YA UCHAGUZI MSEME KARATASI HAZITOSHI??? HUU NI ULAGHAI, MAMBO YA KUANZA KUCHELEWESHA MATOKEO, KUHESABU KURA KWA MAFUNGU, KUPOTEZA MUDA NA KADHALIKA. HUU NI UZEMBE UMENIUDHI SANA KAMA MTANZANIA.
ReplyDeleteinakuwaje uchaguzi wa ubunge na udiwani unahairishwa na wa rais kuendelea wakati karati ni hio hio moja ya kuwachagua wote?
ReplyDeletenashindwa hata cha kusema kuhusu hili jambo,yaani hakuna siku kitu kikafanywa kikawa perfect kila siku kuna upuuzi fulani somewhere,nyinyi mlijua kabisa idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura kwanini hamkujiandaa mapema upuuzi gani huu sasa mnatuambia?baba wa tume ya uchaguzi ningekuwa idhini yangu ungeng'oka kwenye hiko kiti..i swear
ReplyDeleteGemu la ccm hilo kuahirisha uchaguzi ili waibe kura.
ReplyDelete