Marehemu Mzee Matthew Salukele

Wapendwa ndugu zetu,

Kwanza napenda kuwaelezea kuwa hii ni mara ya kwanza katika jamii yetu ya Columbus, Ohio kupata tukio kama hili. Ni mara nyingi tumepatwa na misiba nyumbani Tanzania; hivyo huwa tunashirikiana kuwawezesha wafiwa kwenda nyumbani. Hii ni mara yetu ya kwanza kuhusika na kusafirisha mwili nyumbani.

Tuwieni radhi na mabadiliko ya gharama. Sasa hivi tumepata update mpya ambazo zina gharama halisi za kuandaa, kuhifadhi na kusafirisha mwili wa marehemu baba yetu Mzee Matthew Salukele kuelekea nyumbani kwa mapumziko ya milele. Na gharama hizo ni kama zifuatavyo:
Kuandaa, kuhifadhi na kusafirisha mwili ni $ 9,000.00
Tickets za wafiwa (2) ni $4,200.00 ($2,100 kwa kila mmoja)
Rambirambi kwa wafiwa ni $1,000.00

Kwa hiyo jumla ya gharama zote ni $14,200.00.

Jumla ya rambirambi zilizokusanywa nyumbani kwa wafiwa ni $1,800.00.

Kwa hiyo ndugu zangu bado tunahitaji msaada mkubwa sana. Tegemeo letu kubwa ni harambee itakayofanyika leo saa kumi na moja jioni katika ukumbi wa Worthington Activity Center; address yake ni 909 Proprietors Road, Worthington, OH 43085 (Worthington ni suburb ya Columbus. Iko karibu na high street & 161).

Kufika kwenu ndio kufanikisha shughuli hii.

Kwa wale ambao hawatawaweza kuhudhuria, tunaomba wawakilishe michango yao kupitia Bank ya Chase kwa jina la Happiness Salukele Account# 911969095; Routing# 044000037.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati na Mungu azidi kuwabariki.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Kassim Mtambo - 614-805-4428
William Mwandambo 614-537-1448
Bidan Mchao - 614-670-2312
Walter Kalosi 614-946-2213
Maiga Mapigano 614-783-8258
Yusuf Mecca - 614-589-6140
Metty Nyang’oro 614-226-4216

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. A: Ipo haja kubwa ya kuachana na
    tamaduni za Omba omba..

    1. Omba omba ya michango ya
    harusi.
    2. Omba omba ya misiba.

    B: Tujifunze..

    1. Kujiwekea akiba
    2. Kujiwekea bima ya mambo hayo

    wa-AFRICA TUSONGE MBELE jamani

    ReplyDelete
  2. Hizo $1000 wafiwa wanachangiwa za nini? Is it pocket money. Cha muhimu ni kupata hela ya kusafirisha marehemu na mtu atakayemsindikiza.

    ReplyDelete
  3. jamani heshima kitu cha bure, yaani tuchangie hadi pocketmoney? kwanza hao wafiwa inabidi wakatiwe oneway ticket.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana kwa msiba na nawatakia kila la kheri katika kukusanya michango ili hizo dola elfu 14 zipatikane. Ingekuwa ni hapa Dar hiyo pesa ingepatikana wthin seconds. Wiki hii tuu tumefiwa na mzee Aloyce Swai hapa Dar es Salaam na watu walijitoa kwa moyo sana kuchangia kupeleka mwili Kibosho Masoka Moshi. Tanzania watu bado wana ili sense of community lakini wenzetu huko majuu kidogo mko wagumu kuchangia. Jua linalompata mwenzio leo nawe kesho litakupata. Jitoleeni kwa moyo. Kila mtu akitoa dola mia hiyo pesa itapatikana haraka sana. POLENI NA MUNGU AWAPENI NGUVU KATIKA MAANDALIZI

    ReplyDelete
  5. MIMI NAWASHANGAA SANA NDUGU ZANGU KWANINI MUNAJITIA GHARAMA NA KWATIA WATU WENGINE GHARAMA KWANINI MAREHEMU ASIZIKWE HAPO HAPO ALIPOKUFIA KUNA HAJA GANI KUPELEKA MAITI TANZANIA? GHARAMA YA MAZISHI HAZITOZIDI $6000 KAMA MUTAZIKA HAPO. POPOTE ATAKAPOZIKWA TAYARI AMEFIKA KWA MOLA WAKE KITAKACHO MSAIDAIA NI IBADA YAKE ALIYOKUWA NAYO NA AMALI ZAKE . HILI NAOMBA MUWE MUNAFIKIRIA SANA. SISI NDUGU ZENU WAISALAMU MARA NYINGI TUNAZIKANA PALE PALE MTU ALIPOKUFIA NA WALA HATUEKI MUILI WA MAREHEMU SIKU NYINGI HII INAPUNGUZA GHARAMA KWA WAFIWA NA MAJONZI PIA.

    ReplyDelete
  6. Hizo comments za hapo juu hazisaidii , kama hutaki kuchangia nyamaza , usiwakatishe tamaa watu wengine wanaofikiria kusaidia.

    ReplyDelete
  7. michuzi sikiliza, mimi ninaishi uingereza lakini nimekuja kusoma na nitarudi. naomba utoe ushauri kwa hawa watu wanaokaa huku ughaibuni warudi nyumbani inasikitisha kuona kwamba hata nauli ni issue,jamani kukaa nje jina kubwa lakini hela hakuna, kuosha vibibi na kubeba box ndio kazi yao kubwa

    ReplyDelete
  8. poleni sana wafiwa
    tx

    ReplyDelete
  9. WE MWISILAMU HIYO NI IMANI YAKO, WENGINE LAZIMA MWILI URUDISHWE NYUMBANI UNLESS OTHERWISE. HIYO HELA UNAYOONA NI GHALAMA ITAKUFISHA WAPI. HAYA MAJONZI SIJUI UNAPUNGUZAJE, AZIKWE ALIKOFIA AU APELEKWE NYUMBANI MAJONZI NI YALE YALE, NA YANAKUWA MENGI KWA WALE WA NYUMBANI AMBAO UTAWANYIMA NAFASI YA KUMUUGA MAREHEMU. KAMA INAWEZEKANA BASI MAREHEMU ARUDISHWE NYUMBANI, ZIKENI NJE PALE INAPOSHINDIKA.

    ReplyDelete
  10. Poleni sana wafiwa najua ugumu wa hali ya namna hii, mchangiaji wa kwanza kama ni mtaalam wa kufundisha namna ya watu kuishi na kujiwekea bima ya shida za matatizo kama haya angesubiri tumalize msiba huu na kusafirisha marehemu alafu aje na ufahamu wake tungefaidika naye, lakini huyu mchangiaji hana busara hata kidogo kwani michango ya kusafirisha marehemu inafanyika sehemu mbali mbali hii ndizo mila zetu wa Tanzania,hasa wahaya na wachaga, kama huna hela ya kuchangia kwanini usikae kimya?wafiwa hawajalazimisha hila wanaomba kupitia tamaduni zetu.Kwakuwa huyu siyo baba yako kwanini usinyamaze wewe mshamba asiyejua kesho kitatokea nini kwako au kwa wanafamilia wako? Ndugu zangu jifunze kujiheshimu wacha kuropoka.
    Mdau uk

    ReplyDelete
  11. hakuna mtu mwenye namba ya hashim thabiti atusaidie au atuazime??????,na vile vile tujiangalie wazee wetu wakiwa wazee trusiwalete huku kutibiwa tuwatumie hela wakatibiwe amana.sasa tunataka kuhangaishana hapa wengine renti zetu tunataka kudaiwa late fees halafu mnatuomba dola mia aaah jamani, baba yangu ataponea panado na aspro haji kufia huku.au kaka michuzi tuazime basi walahi tutakulipa haki ya mungu utalipwa,tarehe tu hizi mbaya,

    ReplyDelete
  12. Nyinyi mliochangia na kwa mdhaaa hayaja wakuta pindi yakiwa kuta chungu mtaita tamu..na si lazima mchangie kwa kuandika marehem azikwe kokote.poketi money.omba omba na kadharika,
    WAO WANATAKA WENZAO WA COLOMBIS KUWA NAO PAMOJA KWA MSIBA WALIOPATA LEO WAO KESHO WENGINE.
    NDUGU ZANGU POLENI SANA NATUMAI MTAMSAFIRISHA MAREHEM MZEE WENU
    MDAU ICELAND

    ReplyDelete
  13. Acheni maneno ya dharau shida inatokea bila hodi, unaweza kuwa umeweka akiba ile umemaliza kufanya jambo fulani tatizo linatokea. Pia suala la kiimani lisiingie hapa wewe ukitaka kuzikwa popote ni juu yako kama Mungu akijalia wengine huwa ni busara kuzikwa mtu alikozaliwa au kuishi kwa muda mrefu maana hutoa nafasi kwa wanaomfahamu kumuaga mwenzao. Pia ndugu wa karibu wao ndio wawe msitari wa mbele kuchangia ndio marafiki nao watachanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...