Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Bi. Chiku Ngalawa akifungua onesho la Kanga za kale usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee VIP holi, kulia ni Mwandaaji wa onesho hilo Mamaa wa Mitindo, Asia Idarous.
Pichani kulia ni Afisa Utamaduni wa manispaa ya Ilala Bi. Shani Kitogo akitoa historia ya vazi la Khanga kwa wageni waalikwa usiku huu.
Mc wa shughuli ya Usiku wa Khanga za Kale, Mtangazaji wa Clouds FM Geah Habib na mwenzake wakisherehesha usiku huu.
Muaandaaji wa onesho la Kanga za kale Mama Asia Idarous Khamsini akikatiza jukwaani na Mumewe Mzee Khamsini kuwashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye onesho hilo usiku huu.
Mama Asia Idarous Khamsini akikatiza jukwaaani na baadhi ya mamodo waliovaa mavazi aliyoyabuni mbele ya wageni waalikwa.
Mastaa mbalimbali walioshiriki katika onesho la Usiku wa Khanga za kale lilifana sana usiku huu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kukatiza jukwaaani na mavazi yao mbalimbali ya kanga yaliyobuniwa na Mamaa wa Mitindo,Asia Idarous.

kwa picha zaidi za onesho hili.

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. KITU KINACHOTUANGUSHA SISI WATANZANIA NI HAYO MABANGO YA BIA KILA KONA..KWANI HAMWEZI FANYA MAONYESHO YA KHANGA BILA HAYO MATANGAZO YA BIA TUSKER TUSKER..

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha kuona mwanamke wa kiislam anafanya vitu kama hivi,... wake up Mama Asia its time to do good deeds and ask for forgiveness to win ALLAh's love and forgiveness dah! na huyo baba mtu mzima masikini ameshafikia magharibi kabisa , Insha ALLAh nawaombea ALLAh awazindue mfanye mema katika hizi siku zenu zilizobaki ...

    ReplyDelete
  3. Mungu ndiyo anaye hukumu na wala siyo wewe anony wa oct 2nd. Muache mama Asia an mme wake waishi wanavyo taka. Msikitini si wana kwenda? Mawaidha si wana sikia? Quran si wanasoma? Sasa wewe yana kuhusu nini?

    ReplyDelete
  4. Mama Idarous onyesho lilifana ila tu jaribu kuchagua mamodo wa standard za ukweli,nguo inaweza isionekane imetulia kwa sababu ya mjaribishaji.
    Tizama,huyo moda wa kiume,mwili choka mbaya,na huyo mwanamke naye.....wacha tu nimsitiri.

    Mdau Istanbuli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...