Marehemu Abdallah Ramadhan enzi ya uhai wake
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiongoza msafara wa magari na pikipiki kuelekea katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya Marehemu Abdallah Ramadhani, aliyekuwa Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten, leo jioni
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Abdallah Ramadhani katika makaburi ya Kisutu, leo jioni. Abdallah alifariki juzi kwa ajali ya gari.
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati)akiwaongoza wakazi wa jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten, marehemu, Abdallah Ramadhani leo jioni.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. jamani!inatia uchungu kwa kweli,huyu kaka huwa mara nyingi
    naangalia taarifa ya habari ya samoja channel ten ni mtangazaji
    mahiri yani cwez hata kuamini kama ni kweli amefariki, MUNGU AILAZE ROHO YA ABDALLA MAHALI PEMA PEPONI' AMINA!

    ReplyDelete
  2. KELAND NURSERY & PRIMARY SCHOOLOctober 12, 2010

    Mwenyezi Mungu awafariji wafiwa wate hasa mjane na mtoto wa marehemu. POLENI SANA

    ReplyDelete
  3. Pole sana mama mzazi wa Abdallah;ni uchungu wa ajabu kufiwa na mtoto wako mzazi (uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi), tena mtoto ambaye anajitegemea na unaexpect kufaidika kwa njia moja ama nyingine from achievements zake, POLE SANA MAMA. Pole sana mke wa Abdallah, Pilly; ni upweke na uchungu wa ajabu kufiwa na rafiki mpenzi aliyekuwa mume, mliyeshirikiana kwa tabu na raha, uliyejua siri zake zote, uliyemueleza siri zako zote, uliyempa moyo wako wote, uliyejitoa kwake kwa hali zote, aliyekutia nguvu pale unapokuwa mpweke, pale unapopungukiwa, aliyekufariji kuliko binaadamu wengine wote, furaha na tulizo la
    moyo wako, baba wa mtoto wako nk nk, POLE SANA MJANE WA ABDALLAH. Pole sana mtoto kipenzi wa Abdallah, Yu; ni ukiwa na uchungu wa namna gani kuondokewa na baba mzazi katika umri mdogo kama huu, baba uliyemuona kama kioo cha maisha yako, role model, real fighter, aliyeleta mlo hata uwe wa namna gani kila arudipo nyumbani, aliyekukimbiza hospitali kila afya yako inapohitaji msaada wa tabibu, bado u mdogo sana kuelewa pigo ulilolipata... POLE SANA YU. Lakini Mungu anatukumbusha wote kuwa yeye ni mume wa wajane na pia yeye ni baba wa yatima, familia yote muaminini Mungu maana amemchukua mpendwa wenu akijua kuwa mngali mkimuhitaji SANA, yeye Mungu atasimamia mahitaji yenu yote ya kimwili na kiroho, mkimtumaini yeye hakika pengo la Abdallah litazibwa na Mungu mwenyewe. poleni pia kaka na dada za Abdallah, it's so sad to face death of your sibling, Mungu atawapa faraja ya kweli. Amen.

    ReplyDelete
  4. Michuzi umefanya haki kumuita Abdallah MPIGANAJI. Kwa mtanzania yeyote aliyewahi kuwa mfuatiliaji wa kipindi cha Morning Magic kinachorushwa kila siku aubuhi na kugundua jinsi marehemu alivyokuwa hodari na asiye na woga wa kutetea hoja inayomlenga mnyonge au mtu anayeonewa kwa namna yeyote kulingana na mada husika atakubali kuwa kweli Abdallah alikuwa mpiganaji. Orest na Mishi kiukweli i can imagine how sad u must be, mlikuwa na chemistry ya ajabu mnapokuwa katika kipindi the three of u! RIP comrade! Mungu akupatie pumziko la amani la milele.

    ReplyDelete
  5. U will dearly be missed by every body who knew the real u. Muonekano wako wa nje ulikuwa kama wa majivuno ila kwa mtu aliyepata nafasi ya kuongea na wewe atakubaliana na ukweli kuwa u were so much down to earth person..... Umati uliojitokeza kupumzisha mwili wako ni kiashiria kuwa u were a man of people. RIP Abdallah.

    ReplyDelete
  6. Huyu kaka si ndio yule yule watu waliandika wakisema anavaa suit za stripes sana au sio yule? Maisha haya basi tu na hizi ajali ndio usiseme tena

    Oh May God rest his soul in peace

    ReplyDelete
  7. Rest in peace Abou. Ee Mungu baba naomba endelea kumpa faraja Pilly na mtoto wake na familia yote. Wapatie mahitaji yao yote ya kimwili na kiroho. Mjalie mtoto wa marehemu yale yote yaliyokuwa ndoto ya baba yake hasa kiafya na kielimu. Asante Mungu kwasababu hutoiacha familia ya Abou ipate tabu, amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...