Sehemu ya wakaazi wa jiji la Mbeya wakisikiliza mdahalo huo
Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Joseph Mbilinyi a.k.a MR.II akiingia ndani ya ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya kwa ajili ya kushiriki mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Mbeya (MBENGONET) kwa ufadhili wa asasi za kiraia Tanzania,huku akishangiliwa kwa nguvu sana
Mratibu wa midahalo mikoa ya nyanda za juu kusini kutoka asasi za kiraia Tanzania Bw Sisila Ngalemwa (Kulia) akijaribu kuwatuliza wananchi waliofurika katika ukumbi wa Mkapa Mbeya kumsikiliza mgombea ubunge wa Chadema Joseph Mbilinyi a.k.a MR II katika mdahalo huo ulioandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Mbeya (MBENGONET) Vijana wakijitolea kumtoa nje ya ukumbi wa mdahalo mmoja kati ya mashaiki wa msanii Joseph Mbilinyi a.k.a MR II aliyeshindwa kujizuia kushangilia kwa staili ya kutaka kumshika mkono msanii huyo wakati akijinadi mbele ya wananchi katika mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Mbeya mjini. MR.II (chadema)ni mmoja kati ya wagombea watano wa ubunge jimbo hilo.
Wapenzi na mashabiki wa msanii Joseph Mbilinyi a.k.a MR II na wale wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) jijini Mbeya wakiwa wamemzunguka msanii huyu nje ya ukumbi wa Mkapa baada ya kutoka kushiriki mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Mbeya mjini
Picha zote na Francis Godwin





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sumaye: Msichague mafisadi mwaka huu

    ReplyDelete
  2. Mr II KAMA HAO JAMAA WAMEJIANDIKISHA KUPIGA KURA "WEWE MBUNGE HUNA MPINZANI"

    ReplyDelete
  3. Nakupongeza sana MrII kuwa msanii wa kwanza wa Tz kuingia katika kugombea Ubunge kwa tiketi ya upinzani hii inaonyesha kwamba si lazima uwe CCM ndio uweze kugombea Ubunge.Nina uhakika MrII atashinda kwa kishindo katika kura za ubunge kwa Mbeya Mjini.
    Keep it up we are behind you!!!!

    ReplyDelete
  4. Haya Bwana Sugu!!
    Lakini Wanyakyusa hawajui kutamka CHADEMA, wao wanatamka KYA NDIMA, yaani chama cha maharage!!

    ReplyDelete
  5. Bwana Joseph Mbilinyi (Mr II) tuwekee video ya huo mdahalo ili tuone ulichosema.

    ReplyDelete
  6. Pamoja na kwamba nashabikia mageuzi watu wa Mbeya wakimchagua huyu. Nitawashangaa sana.

    He is not at his AGE

    ReplyDelete
  7. HICHI KICHWA LAZIMA KIINGIE MJENGONI DODOMA.SIONI WA KUMZUIA HAPO JIMBONI.

    ReplyDelete
  8. Hadj Drogba "mwana chelsea"October 12, 2010

    Kila la kheri kaka lakini utamuweza mwalimu wako MPESYA?Maana huo ni mpambano wa mwalimu na mwanafunzi wake wa zamani hapo mbeya secondary school,mwalimu ccm mwanafunzi chadema,hapatoshi mbeya mjini,

    ReplyDelete
  9. Mr II hata kama hutafanya chochote, tunachotaka ni kubadilisha huu upepo tu maana CCM wanaamini hata wakisimamisha kivuli kitashinda tuu. Nakutakia kila la heri na hii safari ngumu, iyojaa matisho na kila aina ya uzushi. Kajifunze wanachoking'ang'ania hawa wazee wa CCM huko bungeni na wasitusaidi chochote sisi walala hoi. Nchi yetu imeuzwa ati!!!

    Mkereketwa aliyechoshwa na CCM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...