Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, imekiri kupata taarifa za kuwepo kwa ujumbe unaosambazwa kupitia simu za kiganjani ambao umekuwa ukiwahamasisha wananchi kutokuwachagua baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

Akihojiwa na TBC, Naibu Mkurugenzi wa TCRA, Richard Kayombo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha namba hizo huku akitoa rai kwa Wananchi kutokuzijibu au kusambaza ujumbe huo.

"Tumepokea malalamiko mengi tu, na ujumbe unakuja kwenye namba ambazo 03588108226 na mwingine kwenye namba 03588976578. Kwa mwelekeo wa haraka haraka, hizi namba zinaonekana ni namba za nje ya nchi. Lakini kwenye teknolojia, chochote kinaweza kikatokea. Inawezekana ni kweli ni namba ya nje ya nchi, lakini laini inayotumika na mtu aliyeko kwenye nchi nyingine. Lakini vile vile, inawezekana ni ujanja wa simu kutoka kwenye mtandao" alisema Kayombo.

Hata hivyo, Kayombo alisema TCRA itazuia matumizi ya namba hizo kwa sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika hapo Oktoba 31, 2010.

Aidha, wananchi wameaswa kutojibu wala kusambaza ujumbe wanaotumiwa katika simu zao ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na uchunguzi unaoendelea wa kubaini chanzo cha mtandao huo.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya saa mbili ya TBC, tarehe 11 Oktoba 2010.

credit source: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/tcra-simu-hadaa-2010.html#ixzz127x0Nkik

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Vipi kuhusu Ujumbe kama hizo ambazo zi nasambazwa kwa njia ya barua pepe, kwa njia ya picha na kupitia tovuti pro-vyama?

    ReplyDelete
  2. Hizi habari hata mimi, nilipata hii sms siku ya jumapili asubuhi sana, ila nilizifuta haraka coz izo number sikuzitambua niza kutoka wapi, mawazo yangu yalikuja kwenye zile number ukipokea unakwishinea!!
    Kweli hizi simu zinatuogopesha kweli hata mtu ukipigiwa simu na number kama haujaisave kwenye simu yako inakuashida mno kupokea mtu unajiuliza mara mbili mbili, Hivi kwani hawa TRCA au kampuni za hizi simu zetu wanashindwa kweli kufuatailia haya mambo ya hizi number zinazojitokeza kila leo? mbona wanaonekana kama wameshindwa kufanya kazi yao ipasavyo? mlisema watu wajisajili ili kupunguza makosa lakini mbona hayo makosa yapo kila siku? jamani nyie vyombo vya mawasiliano chukueni hatua acheni kuongea kila siku kwenye vyombo vya habari kua mnalifanyia kazi wakati bado maovu ya simu yanatokea kila siku. Angalieni sasa wamekuja mpaka kwenye uchaguzi hamuoni kama hii ni hatari sana kwa nchi yetu?

    ReplyDelete
  3. TCRA mna kazi ya ziada maana technologia inavyokimbia inabidi vijana wenu muwa-update kila kukicha ili muweze kujibu query kama hazi kwa uhakika na sio kubahatisha na kuhatarisha maisha ya watu!!
    Asanhteni kwa kujibu haraka.
    Msemakweli

    ReplyDelete
  4. HAMNA LOLOTE CCM MNAOGOPA

    ReplyDelete
  5. Mdau wa TeknohamaOctober 12, 2010

    Hiyo namba ya 358 ni country code ya nchi ya Finland (kama vile ya Tanzania ilivyo 255).

    SUALI: Kwa vile Balozi wa Finland yupo Dar, je Serikali yetu inachukua hatua gani ya kushirikiana na Serikali ya Finland ili kubaini kwamba huyo mwenye simu ni nani, halafu kumchukulia hatua?

    Si ajabu anakiuka pia maadili au sheria za Finland kuhusu matumizi bora ya simu. Ila, tusipopeleka hoja kwenye Serikali yao, basi wao watakosa sababu ya kumfuatilia huyo anayetuma hizo SMS za kuvuruga amani nchini mwetu.

    ReplyDelete
  6. TCRA can u be serious please? With all the money and facilities u have still u can not do ur job! Tracing the source of the msg and where about of the source is possible. Talk to telecom engineers we have here in tz

    ReplyDelete
  7. +358 ni code namba za Finland, kama namuona vile muandishi wa hizo msg! Hahahaaa! alikuwa anajifanya mjanja kwa namba za Ulaya wala sio tabu kumpata ukinunua sim card lazima ujirejiste mpaka namba ya nyumba!Wapeni kazi Interpol watawapa mpaka jina lake!

    ReplyDelete
  8. Mimi binfsi sioni kosa

    ReplyDelete
  9. Nina hakika ujumbe huu ungekuwa unakichafua chama tawala badala ya kukilinda TCRA wangetuambia leoleo huyo ni nani na kufikishwa mahakamani bila kungojea uchaguzi upite.

    Anayefanya hiyo kazi anajulikana na hakuna haja ya uchunguzi, mi nikimtaja hapa Michuzi wa Ukada wake hatatoa maoni yangu ila tunamjua na hata TCRA wanamjua pamoja na kundi lake zima la IT lililokuwa limepewa kazi maalum ya kuhakikisha watu maalum wanashughulikiwa kitechnology mpaka chakachua.

    ReplyDelete
  10. Mimi sioni ni kosa. kwani hayo matangazo yanayobandikwa njiani mchague fulani na fulani nayo ni makosa? Hii ujumbe kama ni hii inayotembezwa kwenye email basi tunajua kwanini hawataki watu wapate. Mimi niliforwad hizo email kwa vile zina ukweli ndani yake na mwenye kupokea naye akisoma akasona basi siku ya kupiga kura ni yeye mwenyewe achague anayeona anamfaa..

    Hii wameona watu wengi watabadilisha mawazo ya kupiga kura kama wenye hela wanaweza kutandaza mabango kila mahali kwa nini wasio na hela wasiweze kutumia simu na mitandao ya bure kuwakilisha ujumbe wao.

    Mimi sio kabosa kuna kosa gani la kupokea ujumbe na kusoma na kuelewa kila kitu na kuforward kwa watanzania wenzangu.

    Ndio ulimwengu wa mitandao huo hamna siri siku hizi. Nyie mtahakikisha mnayoyafanya hayawafikii raia na kujua watu hawaoni wala hawasikii hii mitandao itawaumbua

    KURA YANGU NAJUA NINAYEMPA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...