Mwalimu akiwa Butiama
Kaburi la Mwalimu Butiama

Mwalimu na Mama Maria enzi hizo
Mwalimu na Mama Maria walipomtembelea mama mzazi wa Julius Kambarage Nyerere

Mwalimu akiingia kanisa la St. Peters. Alikuwa mcha Mungu sana
Mwalimu na Marais Kenneth Kaunda wa Zambia,
Mzee Jomo Kenyatta wa Kenya na Dr Milton Obote wa Uganda
Mwalimu akimkumbatia JK baada ya kukubali matokeo ya kura za kuwa mgombea urais wa CCM Mwaka 1995 huko Dodoma
Mwalimu akiongea na Mwandishi Freddy Macha walipokutana Rio de Janeiro, Brazil

Mwalimu na Mama Maria wakiwa India nyumbani
kwa Mama Indira Gandhi na mwanae Rajiv

Mwalimu akimkaribisha Madiba Ikulu, Dar

Mwalimu akitembea kuunga mkono Azimio la Arusha kwa kutembea toka Butiama
Mwalimu, Mama Maria na Mzee John Malecela wakiwa na Iddi Amin, Uganda
Mwalimu akiwa na viongozi wengine wa nchi zisizofungamana na upande wowote
Mwalimu akitaniana na Tom Mboya na viongozi wengine Kenya

Mwalimu akisalimiana na Iddi Amin Dadah wakati wa mkutano wa OAU Addis Ababa, Ethiopia

Mwalimu na Mzee Malecela katika mkutano wa OAU ambapo Iddi Amini alikuwa akihutubia
Mwalimu akicheza bao na wazee wa Butiama huku Rais Ali Hassan Mwinyi na Mama Maria wakishuhudia
Mwalimu na Familia


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. MAREKEBISHO (picha ya saba kutoka juu): Nafikiri unamaanisha mwaka 1995 na sio 2005 maana Mwl. alifariki mwaka 1999 hivyo haiwezekani kuwa alikuwa hai mwaka 2005

    ReplyDelete
  2. msaada tutani

    Mimi ni mdau wa globu ya jamii, nipo Sweden.Naomba msada kwa yoyote anayejua mtandao au link naweza kupata nyimbo za maombolezi ya Mwalimu Nyerere.

    Natanguliza shukrani.

    Mdau

    ReplyDelete
  3. HE WAS A SPECIAL PERSON! R.I.P!

    ReplyDelete
  4. mwalimu ni mfano mzuri sana wa kuigwa na watanzania
    aliweka mbele na kuthamini kisomo
    mwadilifu
    kutokuwa mbinafsi wa kujilimbikizia mali au wizi,
    and conceptual mind thinking head.
    alikuwa anaheshimika na marais dunia nzima

    angekuwa rais leo wachina wasingethubutu kuja kutulaghai na kutuibia kama kinachofanyika sasahivi.

    alichokosea ni ujamaa/usocialist uchumi unaotegemea ujamaa umeshindwa warusi wachina wote wameubwaga ujamaa wamejiunga na wamarekani wamekuwa matapeli wakubwa na wezi kama wamarekani na waingereza.

    jamani hii imekaaje? mgodi wa kahama tanzania tunapewa asilimia 5 ya faida inayopatikana

    waarabu wanachukuwa asilimia 65 ya faida inayopatikana kutoka kwa kampuni za waingereza na wamarekani zinazochimba za mafuta uarabuni!
    mbona sisi ni vichwa maji sana?

    ReplyDelete
  5. would be useful to include DATES on pictures, imo

    ReplyDelete
  6. Very inspiring... Great Memories...!!! Tanzania Yenye watu wenye haiba kama hii inawezekana!!!

    ReplyDelete
  7. I am not sure kama angelikuwepo leo bado angekuwa mwana-CCM

    ReplyDelete
  8. VIJANA: KUMUENZI MWALIMU JULIUS NYRERE

    Napenda kutoa changamoto kwa vijana wa Tanzania waliomaliza digrii ya kwanza, kama ifuatavyo:

    Kama Nyerere alikuwa ni mfano mkubwa si katika fani ya elimu tu, bali pia katika fani nyinginezo, vijana wetu igeni mfano wa Nyerere kwa kugombea “The Julius Nyerere Master's Scholarships.”

    Katika kumuenzi Julius Nyerere University of Edinburgh ilizindua mwaka 2009 misaada ya masomo kwa wa-Tanzania (The Julius Nyerere Master's Scholarships). Sijui kama misaada hii inagombaniwa?

    Kwa vijana wetu wa-Tanzania wenye kutaka kugombea misaada hiyo (The Julius Nyerere Master's Scholarships), maelezo zaidi yanapatikana: http://www.ed.ac.uk/schools-departments/student-funding/postgraduate/international/region/nyerere

    BAP

    ReplyDelete
  9. Nimewahi kuandika mchango wa Julius Nyerere katika fani ya elimu. Hata hivyo, inafaa kuuandika:

    JULIUS NYERERE NA ELIMU NCHINI: MAELEZO BINAFSI

    Mwalimu, pumzika; ulifanya mengi, hususan katika fani ya elimu nchini!

    Tunajitawala (Tanganyika) nikimaliza Darasa la 9! Kabla ya uhuru wetu, Nyerere akiwa kiongozi wa Serikali ya Madaraka, alitoa ubaguzi wa rangi uliopendelea Wazungu na Wahindi/Waarabu wachache na ubaguzi wa dini katika sekta ya elimu. Kuondoa huo ubaguzi ulikuwa ni mchango mkubwa kwa sisi wa-Matumbi!

    Wakati nikiwa Darasa la 7, wanafunzi wenye “akili” waliruhusiwa kuandika mtihani wa Darasa la 8. Walioshinda, walingia Kitato cha 1! Wakati huo huo, mtihani wa "Territorial Standard Eight" ulitolewa ili kuongeza nafasi kwa wanafunzi wa Kidato cha 1.

    Mwanzoni, ilikuwa tunachujwa na huo mtihani wa "Territorial Standard Eight" ili kuwapata wanafunzi wachache tu wa sekondari. Wakati huo huo Kidato cha 1 kilikuwa na mitaala (streams) miwili. Badala ya kuwa na wanafunzi 45, kikawa na wanafunzi 90! Mchango mkubwa!

    Nikiwa Kidato cha 1, mtihani wa “Territorial Standard Ten” (uliokuwa kiwazo cha kumaliza elimu ya sekondari) ukatolewa. Waliokuwa wakichaguliwa kungia Kidato cha 3, ni wale walioshinda Daraja la Kwanza na la Pili. Kila mwanafunzi aliyeingia Kidato cha 1 alikuwa na nafasi sawa ya kumaliza Kidato cha 4. Mchango mkubwa katika kuinua elimu!

    Kufuatia uhuru wetu, Nyerere alizuru Ulaya na Amerika (kwa lugha ya kukejeli ya leo, kutembeza bakuli). Akiwa Amerika, ombi kubwa lilikuwa ni kupata misaada kutoka serikali za Amerika ili kupanua elimu, walimu wakufundisha Shule za Msingi/Sekondari (kufuatia kuondoka kwa walimu wa UIngereza) ikiwa ni pamoja na misaada ya matayarisho ya kujenga Chuo Kikuu nchini.

    Wakati huo huo, wanafunzi wenye “akili” wa Kidato cha 3 waliweza kujaribu mtihani wa "Cambridge School Certificate – Ordinary Level" wa kumaliza Kidato cha 4. Walioshinda, waliingia “High School” – Kidato cha 13. Huo ulikuwa ni mchango mkubwa ki-elimu! Zaidi, karo mashuleni iliondolewa. Kila mtoto wa “Tanganyika” aliweza kujiunga na ki-masomo bila kujali ni mtoto wa tajiri au kabwera!

    Nilipokuwa Kidato cha 4, watoto wenye “akili” waliruhusiwa kujiunga na “High School”. “Pre-selection” ilikuwa kabla ya matokeo ya "Cambridge School Certificate – Ordinary Level”, yaliyokitolewa mwezi wa Februari na hali shule zikianza mwezi wa Januari.

    Mwaka wetu 1963 tukawa wa kwanza kuchaguliwa! Mimi na wenzangu wanane tulichaguliwa kuingia “High School”. Tukiwa Kidato cha 5, masharti ya kuijunga na "university" yakatelemshwa. Badala ya "principals" tatu na "subsidiaries" mbili, mwenye "principal" moja na "subsidiary" moja aliweza kuijunga na University of East Africa. Wanafunzi wakaingia wengi Chuo Kikuu!

    Nyerere alianzisha Chuo Kikuu cha kwanza nchini Tanzania. Na baadaye, alipendekeza “Azimio la Musoma’ lililoruhusu waliomaliza Kidato cha 4 na wenye ufanisi wa ki-kazi wa miaka miwili waweze kujiunga na Chuo Kikuu.

    Elimu ya “bure” toka Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu. Kila mtoto wa m-Tanzania kupewa nafasi sawa bila kujali rangi ya ngozi yake, dini au utajiri!

    Nyerere alituandikia, Elimu ya Kujitegemea. Mpaka leo hii tumeshindwa kuyatekeleza yaliyomo; kama sio kuyatupa!

    Mbali na kuongeza nafasi za ualimu masomoni hapo Mlimani, Nyerere aliagiza wanafunzi wa ki-Tanzania, waliochukua masomo ya sayansi, kila mmoja achukue pia somo la ualimu ili kukidhi mahitaji ya fani hii nchini baada ya wakoloni walimu kuondoka.

    Wengine tunaiona michango hiyo kuwa ni yenye uzito mkubwa katika kuwekeza kwa kile waitacho wataalam, “human development”.

    ReplyDelete
  10. Wengi hapa mliotowa michango yenu katika hizi picha mumeshindwa kujiuliza leo inakuwaje zimewekwa picha za mwalimu na baadhi ya picha za marais wa nchi nyengine ikashindikana kuwekwa picha hata Moja ya Mzee Abeid Aman Karume ,tumepigwa na butwaa wengi wetu ama kweli unapokuwa hupo na lako halipo.

    ReplyDelete
  11. CERTAINLY he would not be mwana-CHADEMA, at least for now

    ReplyDelete
  12. michuzi please tafuteni siku ya kumuhenzi mzee e moringe sokoine ni mmoja wa watu walio safisha mafisadi tanzania mwaka 1982 waharabu na wahindi walimueshimu sana RIP MDAU USA BOB RICH

    ReplyDelete
  13. VIJANA: KUMUENZI MWALIMU JULIUS NYRERE

    Changamoto kwa vijana wa Tanzania waliomaliza digrii ya kwanza:

    Kama Nyerere alikuwa ni mfano mkubwa si katika fani ya elimu tu, bali pia katika fani nyinginezo, vijana wetu igeni mfano wake kwa kugombea “The Julius Nyerere Master's Scholarships.”

    Katika kumuenzi Julius Nyerere University of Edinburgh ilizindua mwaka 2009 misaada ya masomo kwa wa-Tanzania (The Julius Nyerere Master's Scholarships). Sijui kama misaada hii inagombaniwa?

    Kwa vijana wetu wa-Tanzania wenye kutaka kugombea misaada hiyo (The Julius Nyerere Master's Scholarships), maelezo zaidi yanapatikana:

    http://www.ed.ac.uk/schools-departments/student-funding/postgraduate/international/region/nyerere

    ReplyDelete
  14. Nionavyo mimi, haya mambo ya kumkumbuka nyerere na niniii. Picha kwa wiiingi ni propaganda tu za kisiasa za CCM kuibua hisia za mwalimu ili watu wachague sisiemu kwa kuhusianisha na Nyerere.

    Kumbukeni kuwa Mwalimu alikua na Ideas nzuri ambazo hazikutekelezeka. He was a dreamer, and there's nothing wrong with that....but He COULD NOT DELIVER!!

    ReplyDelete
  15. Lakini ninaamini angekuwepo mpaka leo sidhani kama haya yanayotokea kama yangetokea.... alikuwa na UTHUBUTU WA KUMWAMBIA MTU HAPO HAPANA.....

    ReplyDelete
  16. ANGEJIUNGA NA CHADEMA...HANGEPENDA UCHAFU WA CCM

    ReplyDelete
  17. Tunahangaika kupata vazi rasmi la kitanzania, kwa nini tusivae mgolole wa mwalimu kama kwenye iyo picha? kwa wanaunme! na akina mama wavae kama mama maria??!! Nawakilisha. Pia Michuzi tuoneshe vizuri huo mgplole wa mwalimu akiwa amesimama, ili nikajishonee wa kwangu. RIP Mwalimu

    ReplyDelete
  18. Rest in peace.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...