ANKAL asalaam aleikum.

Nina mawazo tofauti kidogo juu ya uamuzi wa kuwa na brass band kwa ajili ya "kuimba nyimbo za Taifa" pale tunapokuwa na shughuli japo tekinolojia ya "CD" ilisumbua. Nadhani panapokuwa na tatizo la ki-ufundi, jibu lake linapaswa kuwa la "kiufundi".

Kama tekinolojia ya CD imekataa/inasumbua; je hakuna badala yake??? jibu ni kuwa zipo !!!! Kama CD imekataa, hata wimbo husika ungewekwa kwenye Hard disk ya Kompyuta au hata "CD/DVD za ziada" bado ungeweza kupigwa na mambo yakaenda vyema.

kuweka brass band ni gharama kubwa; kuanzia mazoezi ya nyimbo husika na siku yenyewe ya shughuli ; maana hao watu wa band itabidi kuwagharamia (posho).

Ninahisi viongozi husika wanaweza kuliangaliaa tena suala hili hasa ile Tume ililyoundwa kushughulikia tatizo hili la "kitaalamu rahisi".

Nawasilisha, wadau nao wachangie
--

Mdau

Adam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Wajua walioamua kurudisha Brass band ni watu ambao walikurupuka tu, hawakufikiria kwa undani zaidi. Kuna njia nyingi tu ambazo zingeweza tumika au zinaweza kutumika kuepusha tatizo lililotokea uwanjani.Moja ya tatizo ni kutokuwa na utaratibu wa kujiandaa na kuchukulia kila kitu kwa mazoea tu. Naamini kama Kaijage angejiandaa kwa kutest kabla, na kuhakikisha kuwa anakuwa na backup radio player au computers kama mbili au tatu tofauti, sidhani kamaa zingekwama. Kurudi kwenye brassband kwa sababu CD iligoma (Nahisi wali burn CD za kichina na sio orijino) ni sawa na leo hii kuamua kutembea kwa miguu ati kwa sababu jana ulipanda gari ukapata ajali.

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe ndugu yangu naona unataka turudie kulekule, wewe umeambiwa kutokupigwa wimbo wa Taifa ilitokana na hitilafu za kiufundi, sasa hizo CD ama hizo DVD za diada zitapigiwa wapi? Mimi nilichoelewa ni kwamba mitambo ilileta shida maana yake vifaa kama amplifier may be speakers na matatizo mengine tu, kwa hivyo kuwa na CD za ziada bado siyo ufumbuzi, naunga mkono uamuzi wa Serikali kuweka Brass Band, kwanza hiyo tu ni burudani pia kuona Band iki perform live. Sasa kuhusu gharama wewe usipate shida nadhani faida itayotokana na mauzo ya mechi hizo watatenga ki percentage kidogo kuweza ku fund hiyo kitu, kwa hiyo wewe relax usipate shida ukadhani Walimu ama Manesi watakosa mishahara yao eti kwa sababu ya uamuzi huo wa Serikali.
    Mdau Bob Dash, Nawasilisha!!

    ReplyDelete
  3. Kwa nini mtumie technologjia, Jamani hao wasanii wetu wanaweza wakauimba huo wimbo wa Taifa Tanzania tena watajisikia raha na heshima kubwa. Ni tunukio lisilo mpaka kuaminiwa kuimba wimbo wa taifa. Kuhusu wimbo wa mataifa menginene labda hapo ndipo mabo ya ufundi yatahitajika, japokuwa najua bebndi ya jeshi ( kama bado ipo) inaweza kupiga wimbo wowote.

    ReplyDelete
  4. Wee mdau acha ubaili wa ki****a,
    watu wote wangiwa wabahili kama wewe
    kusingekua na maendeleo,
    wee unajua uwanja unaingiza Tsh ngapi mpaka washindwe kugharamia Band?
    Ndio maana hata viti na vyoo
    wanashindwa kusafisha.
    Nafikiri hata tickets zikiwa na No
    gharama zauchapishaji zitapanda ndo maana hawaziweki.

    ReplyDelete
  5. Hivi Watanzania tuna matatizo gani...??!!

    Kuna ugumu gani wa kupiga wimbo wa Taifa uwanjani...au hili nalo tunahitaji Wawekezaji waje kutusaidia???!!!

    ReplyDelete
  6. Kama tatizo ni mitambo nani alifanya ukaguzi wa mwisho katika kukabithi uwanja?. na sehemu ya retention katika malipo ya kila mwezi ya sub-contractor na contractor kwanini yasitumike kutengeneza mitambo hiyo, watanzania tunapenda kuongea lakini hakuna kitu tunajua, katika sheria za ujenzi jct 2005 kila valuation ya kila mwezi lazima iwe na retention ambayo ni 20% ya malipo yanayotolewa haya ndiyo kazi yake sasa kurekebisha matatizo kama haya, je mpangilio huu ulifanyika? au hapana? na kama hapana kwanini? na Florian kaijage alikuwa subcontractor wa hiyo sehemu ya mitambo? jibu hapana, je kama alijaribu ikakubali na ikagoma wakati timu zimejipanga kuimba nyimbo za mataifa yao hilo kweli ni tatizo la Florian? Haya yoye yanatokana na nchi kutojiwekea kitu kinachoitwa quality kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi na ukiangalia na kufabya uchunguzi zaidi labda TBS watu wa viwango walia sahii zao na kukubali mitambo hii inayoleta aibu kila siku. Na mwisho sishangai kwani hili ni suala dogo sana ukilinganisha na uchakachuaji wa mafuta, mbona waziri na wahusika wa nishati hawakufukuzwa kazi? Tenga baada ya kumsimamisha Florian ulitakiwa wewe uanze na baadae watu kutoka serikalini na mtu aliye issue final certificate katika project completion awajibishwe.
    Pkahatano. BSc(Hons) HND in Construction.

    ReplyDelete
  7. Utamu wa Tanzania ni ule wa kuunda tume, kila jambo halipati suluhisho mpaka iundwe tume ili watu wajipatie pesa.

    Natungoje tume nyengine itakayoundwa ili kuzingatia na kutafakari yale yatakayoagizwa na tume iliyoundwa.

    ReplyDelete
  8. Wawekezaji wata patikana tu.World Bank ipo IMF ipo wata tu saidia.We have lots of Ph.Ds and we know what to do.

    ReplyDelete
  9. Nyie mnaotetea kuwa ni matatizo ya kiufundi amkeni haraka. Tatizo ni uvivu wa wahusika. Kushindwa kuangalia system nzima kama inafanya kazi mapema na kabla ya watu kuanza kuingia uwanjani, wali-assume tu kwa vile huko nyuma vilifanya kazi basi na leo vitafanya kazi. Pia ni uvivu wao wa ndio uliowanya kutokuwa na plan B.

    Rule of thumb: Always have a plan B

    ReplyDelete
  10. Mimi sidhani kama CD iligoma au ilikuwa empty. lazima CD ilikuwepo na ilikuwa imerekodiwa labda watuambie player ndio ilikuwa na matatizo. Kama issue ni CD tuu hapa kitu kidogo kama Ipod au Laptop kinaweza tumika kutoa input ya system. Tanzania kila maamuzi yetu huwa si ya kitaalamu huwa ni ya kukurupuka zaidi na kuruka tatizo badala ya kulitatua. Sasa tunaona watu wanavyodhani issue ikuwaje badala kuhoji waliohusika issue ilikuaje. Ninashangaa pia watu kama Radio clouds nao wanavojikomba kama vile wanataka kutuonyesha ile issue wangekuwa wao kisingeharibika kitu. Tabia ya kuhukumu watu kwa kudhania italihangamiza taifa.

    Mimi.

    ReplyDelete
  11. Anonymous of 05:28:00 hilo ni wazo zuri hata mie nilikuwa nafikiri hivyo.wangetumia wasanii wa hapo bongo kuimba wimbo wa taifa kwenye mechi.au hata yule aliyeshinda bongo star search then mnamkodisha aimbe wimbo huo akiwa uwanjani live.Naona hapo patakuwa patamu saaaana...

    ReplyDelete
  12. Aisee kwanza tangu lini ukaona Wimbo wa Taifa unapigwa kwenye playback kwa CD's,ni NCHI gani hiyo inafanya hivyo tuambie?We ndugu yangu umetokea mkoa gani,jamani tusiwe tunakurupukia mambo na kufuata maneno ya vijiweni,Brass band ni Muhimu kwa taifa wewe,kwanza tunatoa vipaji vya upigaji Drumm's na vyombo vingine nk,Nikuulize swali wewe,ushawahi kutumia CD's au wasema tu,unajua CD's nazo zinamatatizo yake pia,endapo zinapata Scratche's na nk huwaga Zina kwamaga pia(Stack)na tukija upande wa Computer nazo zinamatatizo yake mfano,Computer lisipo kuwa na Specifacation za kutosha mfano Ram ndogo,Hard Disk capacity ndogo limejazwa mavitu mengi au hata sababu ya VIRUS pia husababisha Computer kuwa Slow nayo itazingua tu siku ya siku,sasa we Sikiliza babu Brass band ni Muhimu ndugu,tunataka tufanye vitu Live na Sio Playback,Njoo Marekani huku uone watu wanavyopenda kutumia Live Band,hivi sisi tutafika lini jamani?tunaacha kuzungumzia mambo yatayoleta Maendeleo kwa Taifa letu kama Maswala ya Ufisadi na Rushwa yanavyozidi kushamiri kwa kasi na kuirudisha nchi yetu nyuma kimaendeleo tunaangalia maswala ya Brass Band?Tuache upuuzi jamani sisi Watanzania.

    ReplyDelete
  13. Watanzania wengi hatujui kuimba wimbo wetu wa taifa baada ya kugoma hivyo vifaa tungeweza kuimba. Pili brassband ikiimba ndio safi tutazipata niymbo live lakini pia maafande watapata riziki. Hivi hujui hawafanyi kazi nyingine zaidi ya hiyo. Huu ndio wasaa wa wao kutoka outing and they really enjoy wako radhi hata bure. Hofu yangu ni kama matarumbeta yao ni ya kichina yanaweza goma vilevile kama hiyo mitambo yao ya uwanjani

    ReplyDelete
  14. WACHINA WATATUIMBIA KWA BEI POA KULIKO KUNUNUA CD SIMNAJUWA WACHINA WALIVYO RAHISIII YAHHEEEEE.

    HUKU WANAWAIBIA MAGOLD KWA MACONTAINER
    KALAGABAHO.

    ReplyDelete
  15. mie nakubaliana na pendekezo la mdau. kuleta mabrass band ni kwenda hatua kadhaa nyuma. akina 'rasmakunja' wataangalia mpira bure kwa kisingizio cha kupuliza mitarumbeta.

    ReplyDelete
  16. mie nakubaliana na pendekezo la mdau. kuleta mabrass band ni kwenda hatua kadhaa nyuma. akina 'rasmakunja' wataangalia mpira bure kwa kisingizio cha kupuliza mitarumbeta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...