
YANGA imeendela kuinyanyasa Simba msimu huu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Simba inafungwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuchapwa mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya Ngao ya Hisani iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji hatari Jerryson Tegete ndiye alipeleka msiba kwa mabingwa hao watetezi, Simba, baada ya kufunga bao hilo katika dakika ya 70 baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Juma Kaseja wa Simba kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Simba inafungwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuchapwa mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya Ngao ya Hisani iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji hatari Jerryson Tegete ndiye alipeleka msiba kwa mabingwa hao watetezi, Simba, baada ya kufunga bao hilo katika dakika ya 70 baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Juma Kaseja wa Simba kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Habari Kamili


Dalali uko wapi?
ReplyDeleteKina Rage kazi inawashinda.
simba tutaishinda vipi yanga wakati mwenyekiti yuko kwenye kampeini za ubunge????????????????inauma
ReplyDeletegood news hii ni dalili tosha ya ushindi wa CCM,tutasherehekea ushindi vizuri 31/10/10
ReplyDeleteHongereni Yanga, na wapenzi wake. Mnyama kishachinjwa, sasa ni kumtafuna tu!
ReplyDeleteAnkal mbona unatunyima raha tupe habari mnyama alivyokufa jana. Au kampeni? Tunaitaji kuona picha zaidi.
ReplyDeletesasa mwenyekiti ndiyo anayecheza au ndiyo kocha?
ReplyDeleteNamuunga Mkono Wakuti hapo juu. Ankal tunaomba tupate picha nyingi. Baadhi yetu tuko ughaibuni na tungependa tuone mnyama alivyotafunwa. Mbaya zaidi hayo yametokea mbele ya kundi la Friends of Simba wanaojifanya kuwa simba haifungiki mbele yao. Najua safari hii lazima mutampeleka Nchumnga na Mosha katika mahakama ya wanyama pori kwa kosa la kumuua mnyama
ReplyDeletehee hee hizi rangi vipi jamani? Yanga sisiemu Simba chadema au?
ReplyDeletekwa kweli inatia raha kumchapa mnyama tena nyumbani kwake. sasa mkae mjipange mpunguze maneno. mmekuwa na mipango yenu ambayo si ya soka ya uwanjani. njia zimeshajulikana. na watu wameshaziba kwa hiyo mntakiwa kujipanga na kuwaaambia wachezaji wenu kuwa sasa wakaze buti. hongera sana YANGA. inaonyesha kuwa umoja ni nguvu.
ReplyDeleteKazi ya uongozi ni kuhakikisha maandalizi yanaenda vizuri. Viongozi wanapokuwa karibu wachezaji wanajisikia kwamba hapataharibika neno wakiwa nje ya uwanja. Ni sehemu ya maandalizi ya kisaikolojia.
ReplyDeleteSi mliona hata Taifa Stars enzi za Ndolanga ilikuwa inafungwa kabla hata haijaingia uwanjani kwa sababu "Tyson" alikuwa na uwezo wa kusema Mwameja hataichezea timu mpaka yeye aondoke FAT. Kisaikolojia hakuwasaidia wachezaji kwa uongozi wake.
rage uchague moja SIMBA AU CCM.
ReplyDelete