TANZANIAS BEWARE OF KENYANS IN OUR LABOUR MARKET
Mkuu wa kaya napenda kuleta malalamiko rasmi kwa serikali yetu na kuwataarifu watanzania wenzangu jinsi wakenya wanavyopata kazi kinyemela hapa nchini na kuwafukuza watanzania ili hatua zipasazo zichukuliwe haraka maake vinginevyo watanzania wote wataishia kuwa wamachinga tu ! Huu ni uchunguzi wangu tangu soko huria lianze julai mosi mwaka huu
This will show how Kenyans are hypocritic and a nuisance to Tanzanian's development!
Ikumbukwe kwamba lengo la soko huru lilikuwa ni kufungua milango ya uwekezaji na ufanyaji kazi kwenye eneo letu la Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na mpaka sasa makubaliano ni kwamba wananchama wa nchi 5 za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi kwenye nchi yoyote ila kwa hapa kwetu wageni lazima waombe vibali vya kufanyia kazi wanapopata kazi hapa kwa muda wa miaka 5 ijayo ambapo vitaondolewa kabisa.
Hivyo Mkenya, Mganda,Mrundi,au Mrwanda akija hapa akipata kazi kihalali ataomba kibali uhamiaji . Ikumbukwe kuwa wenzetu Wakenya walianza ubepari zamani hivyo si ajabu ni nchi ya 2 kufanya biashara kwa wingi na Tanzania baada ya Uingereza hivyo pia tunategemea wakenya wengi wawepo kufanya kazi Tanzania lakini kwa kushindanishwa na wazalendo .
Cha ajabu mzee ni kwamba hawa wenzetu badala ya kutumia ushindanishi unaotakiwa sokoni kwa kuangalia vigezo na uwezo wa mtu wao wameanza kutumia propaganda,mizengwe na mbinu nyingine chafu za kuwaondoa watanzania kwenye nafasi zao na kuwapa wakenya.
Utakuta mtu anapewa kazi kwenye kampuni ya kikenya then anapigwa zengwe kuwa utendaji wake ni mbovu na kesho yake analetwa mkenya hata kama mtanzania ni mzuri kwa vigezo vyote au pia kuna kazi zinahitaji training kwao hawatakupa hiyo training kwa makusudi ili ionekane huwezi kazi wamlete mkenya!
Mbinu nyingine wanayotumia wanakupeleka training kwao Nairobi labda mwezi mzima na huku nyuma wanamleta mkenya anafanya kazi zako kisha wewe ukimaliza training unaambiwa hukufikia vigezo wanavyotaka hivyo ujiuzuru au wakufukuze kazi au watakutafutia kisa chochote tu hata cha maisha yako binafsi yasiyohusiana na kazi yako halafu unatishiwa kuwa watakufukuza au ujiuzuru nwenyewe! Kisha wanaenda uhamiaji kumwombea kibali mkenya wao wakitoa sababu kuwa mtanzania waliyemweka ameshindwa kufikia vigezo wanavyotaka
Wadau hizi ni baadhi ya mbinu tu wanazotumia hawa wenzetu kunyakua kazi wa watanzania kwa nguvu ! Kuna mifano mingi na watu wengi wameathirika na hizi mbinu chafu za wakenya hivyo naona muda muafaka umefika wa mamlaka husika kufanyia kazi hili jambo!
Tunaelewa kuwa Kenya maisha ni magumu sana ndo maana wanakimbilia huku kutafuata kazi wakati hakuna watanzania waliofanikiwa kupata kazi Kenya kwa kuomba tu kwenye makampuni ya Kikenya ukiacha wanaopelekwa na makampuni nya kimataifa yaliyopo Tanzania . Hii ni kwasababu Wakenya wana dharau sana (Kenyans are very arrogant) kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki na wanajiona wao wanajua kila kitu. Hii imesababisha hata wao kwa wao wabaguane kimakabila hivyo kampuni ya Mkikuyu huwezi kumkuta Mjaluo au Mkamba ! hiki ndo chanzo cha wao kuuana mwaka juzi baada ya uchaguzi wao maake kule kwao wanaishi kwa mbinu za msituni (survival of the fittest) .
Hata hapa kwetu wafanyakazi wengi walio chini ya mabosi wakenya wanadharauliwa na kunyanyaswa kisa ni watanzania hata kama wana uwezo kuwazidi hao wakenya !
WATANZANIA TUFANYEJE
Ningependa kuwashauri wadau wanapokutana na hali hii wasikae kimya na kusubiri mungu awasaidie . wajue kwamba huu ni mpango maalum ambao wenzetu wamekuja hapa kupokonya ajira za watanzania hivyo tuchukue hatua madhubuti ambazo ni pamoja nazifuatazo:
-hakikisha kila unapofanya kitu kizuri ofisini kwako bosi wako anajua .Hii itakusaidia sana wakati wa kureview performance yako kazini . wenzetu wanaijua sana kuitumia mbinu hii inayoitwa corporate politics! Akifanya jambo dogo tu lazima amwambie bosi wake hivyo kujilinda pakitokea tatizo baadaye.
Watanzania tusikae kimya kusubiri bosi wako aone mwenyewe kuwa wewe unafanya kazi vizuri sana ! mfuate bosi mweleze mafanikio yako kazini na sio kujificha bosi akipita koridoni oooh utakula wa chuya !
Pili tuhakikishe tunazijua sheria za kazi vizuri na sio kutishiwa tishiwa tu na hawa wakenya wakati nchi ni yetu bwana ! tujenge utamaduni wa kusoma haki zenu ndani ya sheria ya kazi ili likitokea jambo tuweze kujitetea ipasavyo. Japokuwa sheria zenyewe zina mapungufu kwa mfano mwajiri anapewa uhuru wa kuchagua akurudishe kazini au akuachishe kazi na kukulipa mshahara wa miezi 12 tu ! sheria ibadilishwe hii !
Tatu tujifunze bargaining skills wakati wa kuomba kazi maake utakuta wengi wetu mishahara ni midogo sana kwani wakati wa kuomba kazi tunamwachia mwajiri ajipangie mshahara wa kukulipa matokeo yake hata ukimpeleka mahakamani atakulipa vijisenti vya miezi 12 na kukufukuza kazi huku nafasi yako akipewa Mkenya na kulipwa kama expatriate.
Nne tungependa vyombo vinavyohusika na kutoa vibali vya kazi kwa wageni (hasa wizara ya mambo ya ndani, wizara ya kazi na professional bodies ) vijiridhishe kweli hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi ambayo kibali kinaombwa. Hivi kweli jamani hatuna wahasibu wa kutosha mpaka Mkenya aje awe management account (mhasibu wa ndani) au financial controller (mhasibu mkuu ) hapa Tanzania wakati NBAA wanatoa CPA mara 2 kwa mwaka ! hawa vijana wanaomaliza hizi qualification watafanya kazi gani sasa ? Tuachane na njaa za muda na utamaduni wa kuabudu wageni ! Tuamini wazalendo na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi .
Tano watanzania tubadilike tujenge attitude ya kujituma kazini maake soko la kibepari ndo linavyotaka ! ukiwa mvivu kazini wakenya watazidi kuja na kuchukua nafasi zetu nasisi tutaishia kulalamika tu ! hivi sasa mabenki makubwa 3 madirector wao ni Wakenya ! mshahara wa director mmoja tu unatosha kuwalipa watanzania zaidi ya 20 wa ngazi za chini na hapo bado hujazungumzia wenzao waliowaleta toka Kenya na vitu wanavyonunua kwa makampuni yaliyo Nairobi hata kama kuna makampuni ya Tanzania yanazalisha kitu hicho hicho maake bosi ndo mwamuzi !
Naomba kuwakilisha
Mdau aliyetendwa na wakenya !!

NIMEFURAHIA SANA COMMENTS ZAKO KWA KWELI NAKUPONGEZA SANA MWANANCHI,HAWA JAMAA WANAKUJA NCHI YETU TUNAWAPA HESHIMA YA KINDUGU ILA WAO NI KINYUME WANATUDHARAU MNO.WAAJIRI WA BONGO ACHENI ULIMBUKENI WA KUKUMBATIA WAKENYA KISA KIINGEREZA.
ReplyDeleteMpendwa mdau uliyetendwa na wakenya pole sana..
ReplyDeleteNi kweli na nakuunga mkono asilimia 100 Watanzania tuamke tuache nidhamu za uoga! Kama unafanya kitu ofisini make sure ur boss knows that ur the one who did it! hao jamaa wanapenda kutoa report za kazi za wenzao tuuuu basi.
Pia ni vizuri kuwa wawazi kwani wana tabia ya kujipendekeza kwa boss ili aonekane mzuri au anachapa kazi zaidi.. so... kwa wapendwa woote mnaofanya kazi na wakenja just be carefull and play in ur position very well don't leave ur room open kwa wao kukuingilia sana.. coz pia wana mtindo sana wa kuchunguza hata kwenye draws za desk yako au kwenye comp umeweka nini.. usipokuwa makini hata emails zako (personal) watakuwa wanasoma ili wakutafutie sababu..
Just be exxxtra carefull! and be urself!
Brother mambo vipi nimependa sana ulivyojitokeza kwa ujasiri. Mimi nafanya kwenye kampuni moja sio ya kikenya lakini makao makuu yapo kenya na mabosi wakenya
ReplyDeleteKwa kweli inasikitisha sana ila jiulize kwanini wengi wanafanya hivyo. Mimi na wewe tunajua tunatabia na sera m
Acha mambo ya zamani kaka, tuko msimu wa JK umesahau nini???? nchi ishauzwa longtime unalalamika wakenya, je umefanya kazi kwa wasauzi au wachina je?? nomaa mzeiya
Gangamaaa fungua biashara yako, wengi tumenyanyasika sema wakenya wanatufundisha mengi sana. Remember this is not their country its yours.
Ndugu Mdau ulieathirika na Wakenya...
ReplyDeleteUlichoeleza kina ukweli wa dhati kabisa na mfano hai ni mimi ninaeandika hii comment....
Umetoa njia mmbadala za kutumia pindi watu wanapokumbwa na hayo matatizo.. katika kusisitiza hilo ni vema vyombo vinavohusika na matatizo ya kazini vikapata picha halisi ya haya matatizo sababu mimi nilireport tatizo langu lakini kimtizamo niliona kama mhusika wa chombo kile hanielewi vizuri or rather she was not getting the real picture of what I meant....
Mimi nashauri vyombo vinavohusika na kutatua matatizo makazini viwe vinapita makazini kila mara kuona kama wafanyakazi wanatendewa haki na pia haki na utaratibu mzuri unatumika kuajiri watu...
Pia nashauri vyombo vinavohusika na kutoa vibali vichukue juhudi ya kujiridhisha kwamba hamna Mtanzania mwenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi flani ndio watoe vibali vya Mkenya kufanya kazi hapa nchini...
Ni kweli kwamba Watanzania tu wapole na wazembe kidogo lakini ni vigumu mtu kubadilika mpaka ajikute kwenye mazingira flani yatakayomlazimu kubadilika... Lakini wenzetu ni watu wenye dharau na tabia mbaya ya kujipendekeza kwa bosi na cha kushangaza wengine wanajiita wameokoka....
Inatia Uchungu sana Jamaa,ukweli hatukua tayari kuingiua kwenye hii jumuia.
ReplyDeleteMi niko Uk lakini wakenya ukikutana nao wanadai wanaenda straight away Tanzania coz is a virgin market na wenzao wana waahidi kazi hata kabla ya kufika Tz.
Naomba watz wenzangu tuchukue hatua,EU yenyewe haiko hivyo coz all most post kubwa zote hapa UK zinachukuliwa na Wa UK wenyewe then ndo france,spain,italy,polish etc wanafuata.
Na wakenya for sure they are very rude and arrogant!
Kwanini watz tumekubali kuingia kwenye hii kitu bila kujiandaa lakini?
Mdau UK
DARWIN,alisema it is survival of the fittest and elimination of the unfit-hence hizi crocodile tears zako hazina nafasi-ni mfumo wetu wa elimu ambao in all aspects unatufanya tuwe second best-a graduate anakuwa hana hata basic communication skills.
ReplyDeleteKweli inauma unapoona mgeni analipwa mshahara mkubwa na maendeleo wanapeleka kwao kweli aipendezi ya hata kuna na mahospital yameajili watu ngazi za juu wote ni watu kutoka nje.
ReplyDeleteinabidi tujitume kisawa sawa
harafu mimi natafuta mtu wakushirikiana naye kuanzisha kitu kikubwa ambacho naona akipo hapa kwetu Tanzania kwa wakenya kipo na kinatoa ajili kwa wingi nchini kenya lakini sina mtaji. kuhusu ardhi aina shida aliyetayari anitafute dor_7@yahoo.com
ReplyDeleteMdau.
ReplyDeleteNimefurahishwa na uzalendo wako na utetezi wa maslahi ya nchi. Ila ningependa zaidi na hoja yako ingekuwa ya uhalisia zaidi kama ungetoa mifano hai. Ungesema ulifanya kazi kampuni ipi (sio lazima utaje jina, hata mahali ilipo au kazi inazofanya), ukafukuzwa na mkenya mwenye cheo gani,lini, akaletwa nani kuchukua nafasi yako n.k. Hii ingesaidia hata vyombo husika kufuatilia. Nimegundua kwamba mambo yanayofanyika kwa uonevu na dhuluma yakitolewa kwenye vyombo vya habari kama hivi wahusika hutetemeka sana na mamlaka husika huazia hapa kuchukua hatua. Pili nawasihi wazalendo wenzangu msifumbie macho mambo haya. Mimi niliwahi kufanya kazi na kampuni moja ambayo ni Internet Service Provider (ISP). Asili yake ilikuwa ni Kenya. Makao yake yalikuwa pale 50 Mirambo, opposite na Umoja House. Mara nyingi wakuu walikuwa wanaletwa kutoka Kenya. Kuna wakati waliletwa jamaa toka huko wa-4 kwa mpigo. Tulijua hawana vibali na pia walikuwa vilaza (hawana uwezo) ukilinganisha na wabongo. Mmoja wetu kwa siri alitoa taarifa uhamiaji. Jamaa walikamatwa, wakaswekwa ndani, bahati mbaya wakahonga wakatoka, wakawa wanafanyia kazi mafichoni mpaka walipopata vibali kwa kuhonga! Sasa vyombo vyetu vyenye mamlaka haya ni corrupt lakini hii isitukatishe tamaa, tupige kelele tunapoona shida kama hii. Wanachotushindwa wakenya ni kiingereza tu. Watanzania tufanye bidii kujifunza english. Kweli sasa hivi mipaka ya ajira imefunguliwa watatuvamia sana. Kama kabla mipaka haijafunguliwa walikuwa wanaingia kiujanja ujanja na wako wengi, itakuwaje sasa!
Mimi nikiwa kama mzawa mtanzania mwenye kampuni niliyoienyea sana kuijenga nimeawaajiri wakenya kama afisa masoko, afisa uzalishaji, asiza ajira na afisa wa pesa, walahi hizo nafasi walikuwa watanzania wavivu kupindukia na u hasara tupu. Toka soko lifunguliwe na kujaribisha kuwaajiri hawa maofisa, walahi faida yangu imeongezeka na ufamisi kazini kama kazi. Mpaka sasa uzalendo nimeusahahu.Ofisa masoko wa zamani mtanzania alikuwa mpaka wanawatukana wateja, pia kuna wakati halikuwa wameishika kampuni yangu mateka siwezi kuwafanya lolote, wananitishia Labour
ReplyDeleteSoko huru la kazi linaleta changamoto kwa watanzania waweze kupata ushindani waache uvivu na wajitume. Nadhani miaka 2-3 ya ushindani watanzania wenzangu tutakuwa fit tu na kushindana barabara na wakenya.
Asante sana.
Alex Bura
elimu ya lazima tena bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita ipewe msukumo kwa nguvu zote
ReplyDeleteCCM oyee
ReplyDeleteEeh bwana umenena. Hili ni neno na lahitaji kufanyiwa kazi haraka mno. Tumuombe tu ankal awe na ujasiri wa kumuingia Mh. Mwapachu (EAC)kuhusu mustakabali wa vijana wetu wanaohitimu vyuo vya juu, tutawapeleka wapi, kama ndo hapa kwetu tumevamiwa. Nakuita kuvamiwa maana wao huko kwao hakukaliki, wote wamekimbilia kwetu, wa kwetu wakienda huko waambiwa hawana uwezo (labda wa lugha), kitu ambacho si kweli. Ankal akusanye data za kutosha ampe huyu mheshimiwa. Jambo hili lisipelekwe sana ki-siasa, maana mwisho wa siku hawa watapeleka forex kwao, na sie tunabaki na nini. Chunguzeni makampuni mengi ya Kenya, angalieni uwiano ndio mtaona ukweli. Wameingizwa na wazimbabwe sasa. Wakenya wana historia ya ubaguzi na majigambo, kwanza wao kwa wao, sasa wakija kwetu si ndo kabisa. Tulifanyie kazi vinginevyo, vijana jiandaeni, jua kali mno.Na nina hakika wakiingia waongeaji kifaransa, tumeula wa chuya. Ankal, tafadhali, tuko nyuma yako.
ReplyDeleteTuondokee hapa na chuki zako. Kama huwezi kazi wanaoweza wataifanya.
ReplyDeleteDuniani = Waafrika vs wazungu
Afrika = Tanzanians vs Kenyas
Tanzania = Chaga vs Nyakyusa
Kilimanjaro = machames vs kiboshos
.
.
.
we vs them all the time.
As bob marley said....."me no know how we and dem' ago work it out"
Wakenya na watanzania ni watu wamoja, usidanganyike na mpaka hewa uliochorwa berlin miaka 125 iliyopita.
I agree with you and thanks for this exposure.I will do my best to strengthern my entry barriers by demonstrating my competence,skills including the interpersonal skills and the power of my knowledge to ensure I can't get evicted from my post by these bias people.
ReplyDeleteMdau wa "Aluta Continyua", INGAWA ALIANZA NA MANUNG'UNIKO MENGI YA KUONEWA, ametoa hoja nzuri sana ya jinsi ya kuhakikisha kuwa mahali popote pale unapofanya kazi, iwe ni kampuni ya Baba yako, ya Mchina, Mwingereza au ya Mkenya, unatakiwa kuzingatia: fanya kazi kwa bidii, tumia muda wa kazi ipasavyo, timiza malengo uliyopangiwa, hakikisha kuwa boss wako wa kazi amejua kuwa umetimiza wajibu wako (kama hakuna mfumo wa tathmini ya utendaji kazi), pale penye mapungufu mwambie ungependa kujifunza zaidi, nk. Lakini cha msingi zaidi ambacho waajiri wengi wa kutoka nje za wanakwazwa ni tabia za Watanzania wachache maofisini na viwandani (sio wote) kushindwa kutofautisha muda wa kazi na na muda gumzo na mambo ya kifamilia. Je ni mara ngapi unafika ofisi unakuta mtu amekazana kupiga gumzo na rafiki yake au anaongea kwenye simu mambo ya kicheni pati? Kuomba ruhusa kila wiki ni kawaida, leo anauguliwa na jirani yake (wala siyo ndugu) na kesho mjomba wa babu yake kafariki. Wenzetu huko wanakotoka watu wanajituma sana, na wanafuata sheria za kazi kwa makini sana. Kumbuka hata hapa hizo sheria zipo lakini tuliamua kuzipuuzia na imekuwa kama utamaduni wafanyakazi kudhani wana haki ya kutembeleana na kupiga gumzo muda wa kazi. Hatujali viwango vya ufanisi--hata nimeona mafundi cherehani akishona shati anaacha nyuzi zinaning'inia-- au ukiingia kwenye mgahawa meza hazijapanguswa na wafanyakazi wamesimama tu wakipiga gumzo. Hilo wenzetu linawakatisha tamaa, maana hujaajiriwa ili kugeuza mahali pa kazi ni sebule ya nyumbani kwako. Samahani kwa Watanzania ambao hawana hizo tabia, wanachapa kazi kwa bidii-- wako wengi--ndo maana mdau wetu kwenye malalamiko yake hakusema hao Wakenya humfukuza kila Mtanzania. Jambo jingine ambalo ningependa kugusia ni ile dhana ambayo imejengeka kuwa Mkenya (au mgeni yoyote) akija hapa Bongo akaanzisha kampuni yake na kuajiri, kwa mfano, Wakenya wenzie watano na watanzania kumi na tano, sisi tunalalamika kuwa hawa Wakenya watano wamechukua kazi za Watanzania. Je ni kweli usemi huo? Kwa maoni yangu, ni Watanzania 15 wamechukua kazi za Wakenya 15 kama huyu Mkenya angeamua kufungua hiyo kampuni Mombasa au kupanua ukubwa wa kampuni kule Kenya. Kwa maneno mengine, mgeni yoyoye, au Mkenya au Mchina, anapokuja TZ na kuwekeza hapa kwa kufungua kampuni (hata kama ni mgahawa), anakuwa amesaidia kuziba pengo la huduma au bidhaa zinayohitajiwa (pengine ni kuboresha tu), na hivyo kutengeneza ajira ya Watanzania. Tukilijua hilo tutaona kuwa malalamiko yetu yangetakiwa kuelekezwa kwa Watanzania wenye mitaji ambao wanashindwa au serikali imeshindwa kuwawezesha kuanzisha hiyo huduma au biashara ili itoe ajira kwa Watanzania. Angalizo la pili ni kuwa, unapopata mtaalamu (daktari, injinia, mekenika, mwalimu, nk) kutoka nje, ni sisi tunaofaidi kwa maana ya kujaza mapengo ya wataalamu ambao ilitakiwa tuwe tumewasomesha na kuwatengenezea sehemu za ajira. Kimsingi inatakiwa ile nchi ambayo anatoka yule mtaalamu itulalamikie kuwa tumewaibia mtalaamu wao ambao walitumia raslimali yao kumsomesha. Kwa maelezo hayo, ningependa kurudia tena umuhimu wa kijikagua wenyewe kwa nini waajiri toka nchi za nje wanatulalamkia na hivyo kupata kisingizio cha kuleta wataalamu wao. Kwa hilo narudia kumsufu tena mtoa hoja kwa kutushauri tufanye nini ili waajiri toka nje za nje (ametumia mfano wa Wakenya) wasipate sababu ya kutubadili. Kanuni alizozitaja zinatakiwa zitumike hata kwa ofisi za serikali, mashirika ya umma na kampuni binafsi za Watanzania wenzetu ili huduma ishamiri kweli kweli. Kumbuka kuwa hakuna bepari ambaye anawekeza mtaji wake ili kupata hasara. Lengo ni faida: hivyo Mtanzania asiye na ufanisi hamfai, lakini pia raia mwenzange kama ni mvivu hamfai, au kama anatoza mshahara mkubwa kuliko Mtanzania mwenye bidii kama yeye,naye hamfai. Hivyo akipata fursa ya kuchangua kati ya watu wawili wenye sifa sawa, Mtanzania na Mgeni, kama mgeni anadai mshahara zaidi atamchukua Mtanzania, kwa vile anataka faida. Tuache kunung'unika na badala yake tufanyie kazi mapungufu yetu.
ReplyDeletePoleni kama nimwekwaza kwa maelezo haya.
Mzalendo
Uchaguzi umekwisha, tunarudi kwenye ulalamishi!! Kulalama hakufai!!
ReplyDeleteMi nafikiri tatizo sio Wakenya, ni sisi wenyewe. Wale wamefikia kiwango cha ustaarabu cha juu mpaka tunahisi wana makakati wa kutumaliza sisi, sio kweli. wanajua wanachotafuta hapa duniani.
Na sisi tujitambue tunachotafuta hapa duniani, halafu tupigane kufa na kupona kukitafuta, at any cost (legitimately ofcourse!!).
Wale mambo yaliyofanyika hapa juzi huwezi kuwafanyia, na kwao sasa mtu mwenye tuhuma anajiuzulu kupisha uchunguzi, Sisi hapa ndio kwanza mtu anatafuta madaraka mengine!!
Hii ya kusema wako vile kwa kuwa walianza ubepari zamani sio kweli. Kwani Wachina hawakuwa mabepari, angalia wanavyochanja mbuga.
Tusitafute tatizo kwa jirani, tujiangalie wenyewe!!
Mdau wa "Aluta Continyua", INGAWA ALIANZA NA MANUNG'UNIKO MENGI YA KUONEWA, ametoa hoja nzuri sana ya jinsi ya kuhakikisha kuwa mahali popote pale unapofanya kazi, iwe ni kampuni ya Baba yako, ya Mchina, Mwingereza au ya Mkenya, unatakiwa kuzingatia: fanya kazi kwa bidii, tumia muda wa kazi ipasavyo, timiza malengo uliyopangiwa, hakikisha kuwa boss wako wa kazi amejua kuwa umetimiza wajibu wako (kama hakuna mfumo wa tathmini ya utendaji kazi), pale penye mapungufu mwambie ungependa kujifunza zaidi, nk. Lakini cha msingi zaidi ambacho waajiri wengi wa kutoka nje za wanakwazwa ni tabia za Watanzania wachache maofisini na viwandani (sio wote) kushindwa kutofautisha muda wa kazi na na muda gumzo na mambo ya kifamilia. Je ni mara ngapi unafika ofisi unakuta mtu amekazana kupiga gumzo na rafiki yake au anaongea kwenye simu mambo ya kicheni pati? Kuomba ruhusa kila wiki ni kawaida, leo anauguliwa na jirani yake (wala siyo ndugu) na kesho mjomba wa babu yake kafariki. Wenzetu huko wanakotoka watu wanajituma sana, na wanafuata sheria za kazi kwa makini sana. Kumbuka hata hapa hizo sheria zipo lakini tuliamua kuzipuuzia na imekuwa kama utamaduni wafanyakazi kudhani wana haki ya kutembeleana na kupiga gumzo muda wa kazi. Hatujali viwango vya ufanisi--hata nimeona mafundi cherehani akishona shati anaacha nyuzi zinaning'inia-- au ukiingia kwenye mgahawa meza hazijapanguswa na wafanyakazi wamesimama tu wakipiga gumzo. Hilo wenzetu linawakatisha tamaa, maana hujaajiriwa ili kugeuza mahali pa kazi ni sebule ya nyumbani kwako. Samahani kwa Watanzania ambao hawana hizo tabia, wanachapa kazi kwa bidii-- wako wengi--ndo maana mdau wetu kwenye malalamiko yake hakusema hao Wakenya humfukuza kila Mtanzania. Jambo jingine ambalo ningependa kugusia ni ile dhana ambayo imejengeka kuwa Mkenya (au mgeni yoyote) akija hapa Bongo akaanzisha kampuni yake na kuajiri, kwa mfano, Wakenya wenzie watano na watanzania kumi na tano, sisi tunalalamika kuwa hawa Wakenya watano wamechukua kazi za Watanzania. Je ni kweli usemi huo? Kwa maoni yangu, ni Watanzania 15 wamechukua kazi za Wakenya 15 kama huyu Mkenya angeamua kufungua hiyo kampuni Mombasa au kupanua ukubwa wa kampuni kule Kenya. Kwa maneno mengine, mgeni yoyoye, au Mkenya au Mchina, anapokuja TZ na kuwekeza hapa kwa kufungua kampuni (hata kama ni mgahawa), anakuwa amesaidia kuziba pengo la huduma au bidhaa zinayohitajiwa (pengine ni kuboresha tu), na hivyo kutengeneza ajira ya Watanzania. Tukilijua hilo tutaona kuwa malalamiko yetu yangetakiwa kuelekezwa kwa Watanzania wenye mitaji ambao wanashindwa au serikali imeshindwa kuwawezesha kuanzisha hiyo huduma au biashara ili itoe ajira kwa Watanzania. Angalizo la pili ni kuwa, unapopata mtaalamu (daktari, injinia, mekenika, mwalimu, nk) kutoka nje, ni sisi tunaofaidi kwa maana ya kujaza mapengo ya wataalamu ambao ilitakiwa tuwe tumewasomesha na kuwatengenezea sehemu za ajira. Kimsingi inatakiwa ile nchi ambayo anatoka yule mtaalamu itulalamikie kuwa tumewaibia mtalaamu wao ambao walitumia raslimali yao kumsomesha. Kwa maelezo hayo, ningependa kurudia tena umuhimu wa kijikagua wenyewe kwa nini waajiri toka nchi za nje wanatulalamkia na hivyo kupata kisingizio cha kuleta wataalamu wao. Kwa hilo narudia kumsufu tena mtoa hoja kwa kutushauri tufanye nini ili waajiri toka nje za nje (ametumia mfano wa Wakenya) wasipate sababu ya kutubadili. Kanuni alizozitaja zinatakiwa zitumike hata kwa ofisi za serikali, mashirika ya umma na kampuni binafsi za Watanzania wenzetu ili huduma ishamiri kweli kweli. Kumbuka kuwa hakuna bepari ambaye anawekeza mtaji wake ili kupata hasara. Lengo ni faida: hivyo Mtanzania asiye na ufanisi hamfai, lakini pia raia mwenzange kama ni mvivu hamfai, au kama anatoza mshahara mkubwa kuliko Mtanzania mwenye bidii kama yeye,naye hamfai. Hivyo akipata fursa ya kuchangua kati ya watu wawili wenye sifa sawa, Mtanzania na Mgeni, kama mgeni anadai mshahara zaidi atamchukua Mtanzania, kwa vile anataka faida. Tuache kunung'unika na badala yake tufanyie kazi mapungufu yetu.
ReplyDeletePoleni kama nimwekwaza kwa maelezo haya.
Mzalendo
IVI NYIE WATZ UCHAGUZI SI UMEISHA KWA AMANI ATI PALE KWENU. SASA MNALALAMI KITU IPI TENA SASA. KWANI NI SIE WAKENYA NDO TUNA ELECT AO LEADERS WENU. BADO HAMJAJIPANGA NYIE, MWAONGEA MANENO MINGIII. SASA.
ReplyDeletePOLENI ATI.
HABARI NDO IYO.
Mimi naomba serikali ifungue mdahalo kuhusiana na education standard ya bongo,mimi nafanya kazi katika recruitment office,inaniumiza kichwa sana pale tunapowafanyia interview wabongo,yani sometimes unatia shaka degree yake kama ni kweli,communication skill zero,simple english ya kujielezea zero,personality impression zero,then unataka nikuchukue nimuache mkenya,i cant do that
ReplyDeleteMimi nilivyokua mfanyabiashara Tanzania, nilishuhudia mwenyewe kuwa Watanzania ni wavivu wa kazi. Watanzania tunapenda story nyingi kazini na kazi hatupendi kufanya.
ReplyDeletePia, kwa elimu, Wakenya wapo mbele sana kuliko sisi. Ndio maana, ofisi nyingi kubwa za Umoja wa Mataifa na NGOs wapo Kenya na sio Tanzania. Uchumi wao pia ni mkubwa kuliko wetu kutokana na elimu yao na ujuzi wao.
Kwa kuwa tumewapa ruhusa serikali ya Jamhuri kukubali Tanzania kuwa katika jumuiya hii, ni lazima tuwakubali Wakenya na wennginewe wafanye kazi Tanzania kwa kuwa kuna uhuru wa wananchi wa Jumuiya kufanya kazi popote sasa.
Nadhani Watanzania bado tupo na siasa yetu ya Ujamaa ndio maana ni tabu sana kufuata matakwa ya "bepari" kazini. Ukiitwa kujieleza kwa nini kila siku unachelewa au unasoma gazeti wakati wa kazi, unaanza kulalamika kuwa unaonewa au "wageni" wana ubaguzi wa rangi.
Mimi nilikuwa mfanyabiashara mjini Dar es Salaam miaka 15, na najua kuwa kama tajiri, nitampa kazi Mkenya kuliko Mtanzania japo kuw a mimi ni Mtanzania kwa kuwa Mkenya anafanya kazi na kuheshimu kazi yake. Pia Kiingereza chake na elimu yake ni bora zaidi. Tabia ya kikazi ya Mkenya na Mtanzania ni tofauti kabisa. Sisi ni gumzo sana , wao ni kazi sana.
Maraha ni pesa
USA (karibu an Mungu)
Yani cha kushangazi ni kitu gani Jamani? Yani ni jana tu tulikuwa na nguvu ya kupiga kura na kutafuta wa kututetea? je lala miko lako umelifikisha offisi ya uhamiaji? Je aliyefukuzwa ameriport wapi? Je wannchi wana nguvu zao za kusikilizwa je kama Watanzani ambao hakuna wa kutusaidia kwa nini tusianzishe kamwamko, changamoto, kwa hao wageni kuwajulisha kwamba macho yetu yapo kwao, na kama watanzania wananchi wasituingilie mapka chini ya uvungu.
ReplyDeleteUkitaka kujuwa kwamba bado tupo nyumba na hatujui ni lini tutaibuka kwenye hilo shimo, Si tumetoka kwenye uchaguzi watu mmechaguwa kiongozi ambae ataleta maendeleo, sasa hayo ndiyo maendeleo tuliyochangu. Hakuna haja ya watu kulalamika zaidi. Kura yako ndiyo ilikuwa nguvu yako na kama umeshatumia kura yako vizuri, hakikisha uliyemchaguwa nakusaidia kwenye hli tataizo na kama hutaki kufanya hivyo. Funga mdomo wacha wakenye wachape kazi na wewe kawe mmachinga.
ReplyDeleteUnaweza kulalamika sana lakini watanzania lazima tubadilike
ReplyDelete- Uvivu
- Elimu Duni (Kiingereza)
- Ushindani - sababu ya ujamaa
- Rushwa
- Uaminifu
- Exposure
Upendeleo na kupeana kazi upo hata miongoni mwa watanzania. Tafuta kazi ambayo itakufanya ushindane. Siku za ujamaa zimekwisha. Wakenya wanaoishi nchi ya nchi yao ni kama asilimia 38 ya wasomi wote. Pesa wanazotuma kwenda Kenya ni $1 billion kwa mwaka ambayo ni karibia budget ya Tanzania. Dhana ya kwamba wakenya wanishi kwa tabu ni propaganda ambazo hazitatufikisha popote.
Hey My bro's
ReplyDeletetuache uswahili wetu... tufanye Kazi, I have been working with Kenyans since my first JOb, these guys are working hard and they know their responsibilities...
I have been so inspired with them and few people think im also Kenyan.. tho its my original but Babu yeke na babu yangu babu yake na babu yake yule babu ambaye nilipewa jina na babu yake wa kumzaa baba yake alizaliwa hapo Mara.. long time hizo mimi mwenyewe nimekulia tegeta na wazaram kibao... Nimeshafanya kazi na organisation kama tatu hapa nchini na za ukweli na nimezidi kujizolea sifa kibao kwani binafsi najua nataka nini kwenye kazi yangu.. wabongo wengi ni wavivu wasioona faida ya kuwajibika wakidhani watamfaidisha bosi.... wanasahau kuwa mafanikio ya organisation pia ni mafanikio yake binafsi... lol! mtu anamafua kidogo haendi kazini, amechelewa daladala basi tena anaishia kulala nyumbani unadhani nani angependa kampuni yake ifanywe kama shule ya chekechea!!! Embu tuamke, najua baadhi ya wabongo ambao ni wachapakazi na wenye uwezo wa kukompit popote duniani... Mdau hapo na kulalamika kote ametoa solutions hata kama mimi haijanitokea embu tujaribu hizo solution na tuone tumefikia wapii... Anyway good job for bringing this on table.
Sango M
Jamani tuwe wakweli. Tatizo si Wakenya, bali ni sisi Watanzania wenyewe. Ukweli ni kwamba Watanzania elimu yetu ni duni mno na kibaya zaidi ni wavivu kupindukia. Tunataka tule vizuri, tuvae vizuri, tuishi katika nyumba nzuri na tuendeshe magari mazuri bila kufanya kazi.
ReplyDeleteUkitaka kuona uvivu wa Watanzania tembelea maeneo ya Posta, Dar es Salaam, saa 2 usiku siku za kazi na utashangaa kuona mji hauna watu. Wote wamekimbilia majumbani mwao kulala!
Ni ajabu na kweli kwamba sehemu hii, ambayo ndiyo kitovu cha serikali na biashara, huwa bado imelala saa 1 asubuhi! Hali katika jiji la Nairobi ni tofauti kabisa. Huko, migahawa katikati ya jiji hufunguliwa saa 10 alfajiri baada ya kufungwa saa sita usiku. Kuna supermarket ambazo huwa wazi saa 24. Daladala (matatu) huanza kufanya kazi saa 9 usiku na kuna baadhi ya njia huduma ya usafiri hupatikana saa 24. Wakenya wanaaza kusoma magazeti ya kesho saa 4 usiku, siyo Tanzania mpaka usubiri saa 3 asubuhi kama utabahatika kuyapata.
Kwa kifupi, Watanzania tumelala na ndio maana Wakenya huja kwetu na kuona fursa (opportunities) ambazo sisi hatuzioni. Wakizitumia fursa hizo, Watanzania hubaki tunalia na kudai tumevamiwa na wageni.
Inapokuja kwenye kazi, tunashindwa kushindana na Wakenya kutokana na uduni wa elimu yetu, upeo wetu mdogo wa mambo na uvivu wetu uliokithiri. Haishangazi kuona karibu makampuni yote makubwa ya kimataifa yanayofanya kazi Tanzania, hasa mabenki, yameajiri Wakenya. Tutake, tusitake, Kiingereza ndio Kiswahili cha dunia na inatia shaka pale mhitimu aliyefaulu vizuri tu chuo kikuu anakuwa hawezi kuandika hata sentensi moja sahihi ya Kiingereza, achilia mbali kuzungumza lugha hiyo.
Tuwapo kazini kazi yetu ni kupiga soga na kufanya kila tuwezalo tusifanye kazi. Naweza kusema bila wasi wasi kwamba hakuna nchi Afrika Mashariki na Kati ambamo watu hutoa visingizio vya uongo vya kutokuja kazini kama Tanzania. Cha ajabu ni kwamba hata sheria zetu zinawalinda wafanyakazi wa aina hii na wao wanalijua hili kwani hukimbilia mahakamani mara moja pale wanapofukuzwa kazi.
Soko letu la ajira limefunguliwa lakini bado tuna kasumba za miaka hiyo ambapo ilikuwa kawaida kwa wafanyakazi serikalini na katika mashirika ya umma kukaa kazini siku nzima bila kufanya chochote au kuomba ruhusa ya siku saba kwenda ngomani.
Dawa ya kutuwezesha kushindana na Wakenya ni kunyanyua kiwango cha elimu yetu, kufanya kazi kwa bidii na kuacha kuendekeza uvivu.