Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame

2.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
Mhe. Omar Yussuf Mzee

3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Mhe. Haji Omar Kheri

4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.

5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

6. Wizara ya Katiba na Sheria

Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.

7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Hamad Masoud Hamad

8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban

9. Wizara ya Afya

Mhe. Juma Duni Haji

10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto

Mhe. Zainab Omar Mohammed

11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo

Mhe. Abdilahi Jihad Hassan

12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-

Mhe. Ali Juma Shamhuna

13. Wizara ya Kilimo na Maliasili

Mhe. Mansoor Yussuf Himid

14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Said Ali Mbarouk

16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika

Mhe. Haroun Ali Suleiman

17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Suleiman Othman Nyanga

18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Haji Faki Shaali

19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Machano Othman Said

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Issa Haji Ussi

2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Zahra Ali Hamad

3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya

Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya

4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,

Mhe. Bihindi Hamad Khamis

5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati

Mhe. Haji Mwadini Makame

6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,

Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi

Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa leo jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Naomba kuwasilisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Shukran jazeera Mheshimiwa Mtukufu rais wa Zanzibar...ila Mtukufu rais sioni jina la mchapa kazi waziri SAMIA SULUHU...jamani sio kama nampigia debe...she is an iron lady

    ReplyDelete
  2. Naona asilimia %99.5 ni wanaume inamaana hakuna wanawake Zenji wenye qualifications za kuongoza wizara!!!!!!!??????????

    ReplyDelete
  3. Anony wa pili hapo juu...jibu liko wazi kuwa HAKUNA.
    M.A-Kafanabo

    ReplyDelete
  4. Mbona hakuna Wizara ya Fedha inakueje? Sijakufahamu

    ReplyDelete
  5. ....kwani kuna kugawana kati ya wanaume na wanawake!? acheni ujinga wa magharibi! hivi bado kuna umuhimu wa kuwa na waziri asiye na wizara maaalum!!!?

    ReplyDelete
  6. hao waliotajwa kia bihindi ni wanaume? mbona hakuna waziri wa muungano kutoka zenji hilo hamulini? acheni choko choko zenu wacha tujenge zenji yetu.ilarais kakosea sana kumuweka shamhuna sio,na kumtoa waziri kiongozi wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...