

shukrani baada ya kutangazwa mshindi

Maalim Seif Shariff Hamad akikubali matokeo
MGOMBEA WA CCM KATIKA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESHINDA URAIS ZANZIBAR KWA MUJIBU WA MATOKEO YA TUME YA UCHAGUZI SASA HIVI KWA ASILIMIA 50.1%
MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AMBAYE KAPATA ASILIMIA 49.9% AMEKUBALI MATOKEO NA KUIPONGEZA CCM NA MGOMBEA WAKE. ANAHUTUBIA HIVI SASA NA KUMKUBALI DK. ALI MOHAMED SHEIN KWA KUPATA RIDHAA YA WAZANZIBARI KUWAONGOZA KWA MIAKA 5 IJAYO AKIWA RAIS WA AWAMU YA SABA VISIWANI HUMO.
HATA HIVYO MAALIM SEIF AMESEMA KUNA DOSARI ZINAZOTOKANA NA BADHI YA MAOFISA NA KUMUOMBA RAIS MTEULE KUWA MWANGALIFU NA HILO ILI NCHI ISIFIKE PABAYA.
AMESEMA KATIKA UCHAGUZI HUU HAKUNA MSHINDI AMA MSHINDWA. MSHINDI NI MZANZIBARI. NA KAMUOMBA RAIS MTEULE AHAKIKISHE HILO ILI HALI YA HEWA ISIJE KUCHAFUKA. ANAMALIZA HOTUBA NA KWENDA KUMPA MKONO DK. SHEIN HUKU VIFIJO NA NDEREMO VIKIUMUKA KATIKA KILE KILICHOITWA MATUMAINI MAPYA KWA ZANZIBAR.
DK. SHEIN ANAITWA KUONGEA SASA.ANAINUKA NA KUELEKEA KWENYE KIPAZA SAUTI. UKUMBI UMEJAA MSISIMKO SI WA KAWAIDA. ANAMFAGILIA MAALIM SEIF KWA HOTUBA FUPI LAKINI NZITO, ANAAHIDI KUSIMAMIA VYEMA UUNDAJI NA UENDESHAJI WA SERIKALI YA MSETO NA KUKUBALIANA NA MAALIM SEIF KUWA HAKUNA MSHINDI ILA WAZANZIBARI WOTE KWA MUSTAKABALI WA MAENDELEO YA VISIWANI.
GLOBU YA JAMII INAMPONGEZA
DK. MOHAMED ALI SHEIN KWA USHINDI HUU WA KIHISTORIA.
VIDEO YA TUKIO HILI INAANDALIWA. TUVUTE SUBIRA........
TUKIO HILI LINARUSHWA LIVE NA TBC ONE
HAHAH Habari nDiyo hiyo.. CCM Oyeeeeeeeee! na bado pambafff!!
ReplyDeleteBFREAKING, naona kaka spidi ya kuandika ilikuwa kali sana :)
ReplyDelete50.1% ? Hmm.
ReplyDeleteNampongeza Maalim Seif kwa kuonyesha busara kubwa kukubali matokeo kiungwana!!!!
ReplyDeleteThe essence ya demokrasia: Mshindwi anakubali; anakaa chini na kutafakari kusimama na kushindana tena, ma la!
ReplyDeleteMaalim Seif ...hilo ndilo alilokuwa analipigania manake alishakubali kushindwa hata kabla ya uchaguzi kufanyika ... kwa kuwa kaahidiwa umakamu wa Rais!
ReplyDeleteAMA KWELI MEDIA ZIMEJAA PROPAGANDA HAPA TUNAPUMBAZWA AKILI KABISA!!!NAONA HATA WEWE MSOMAJI UNAANZA KUKUBALI KWAMBA NDIVYO ILIVYOKUWA MAALIM POA KAKUBALI HAKUNA PROBLEM HAHAHAHA SHENZI TYPE!!!KWELI TANZANIA NI NURSERY SCHOOL-UJI WA MCHELE
ReplyDelete66.4% ya kura zote, huu ni mwanzo tu hatukati tamaa, 2015 CCm mtakuwa na 22%, mtang'oka tu.
ReplyDeletena ukitaka kujua ni kuwa watu wote wale walikua wanajazana kwenye mamikutano ni walikwenda kushangaa watu kutoka mjini wamefika kutembelea vijiji vyao na kusikiliza miziki iliyokua inapigwa kwa bure tu. Watu wote pale walikua hawako pale kusikiliza sera za kiongozi wala nini. Nasikia watu walioshow up kuvote ni wachache sana kulingana na mamikutano yaliyokua yanavuta watu wengi sana ...
ReplyDeleteKelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji!!! CCM oyeeeee
ReplyDeleteUshindi wa kihistoria really?
ReplyDeleteof course, as EXPECTED. next?
ReplyDeleteKwa maalimu Seif hana ofisi rasmi kuanzia leo?
ReplyDeleteAlhamdulilah tunashukuru mungu uchaguzi kwa Zenji umeisha salama na amani huu ndio ukomavu wa siasa naimani mtaelewana na serikali ya mseto itakua safi kabisa na mtaangalia maendeleo ya nchi Dr sheni na Maalim seif Hongera sana sana kwa kudumisha amani.
ReplyDeleteChef Issa
Hongera mshindi na mshindwa. Hiyo ndiyo demokrasia ati! Tuendeleeni kudumisha amani.
ReplyDeleteTanzania oyeee,alhamdulilah mpaka sasa tunajivunia kuwa na amani ktk nchi yetu inshallah itaendelea amani hii na utulivu na maenddeleo yatakuwepo, eti michuzi si ndio eee,hongera pia kaka michuzi kwa jitihada zako za kutujulisha kila kitu mungu akubariki,na aibariki Tanzania yetu ameen.
ReplyDeleteSafi sana. Wewe uliyesema eti Maalim Seif kaahidiwa umakamu wa Rais wacha ujinga wako. Zanzibar hakuna post ya VP. Kazi ya kuimarisha CCM inaanza sasa. Tuone hao wawakilishi wa chadema kama watatekeleza ahadi walizoziweka kwa wananchi wa majimbo yao. Yatakuwa yale ya Tarime kukombolewa na CCM. Ni kweli kabisa mdau: mkoromo wa chura haumzui tembo kunywa maji. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
ReplyDelete.........Maalim Seif alishakubali nafasi ya umakamu, nimeipenda sana hiyo!
ReplyDeleteAissseh! kuna watu mafundi eeenh! hesabu zimepangwa mpaka zimekubali vile walivyotaka! mweeeh!
Kaka Michuzi mbona na wewe unaanza kuckachua matokeo tena. matokeo kamili ni Shein 50.1% na Seif 49.1% na sio 49.9%. 0.8% iliyobaki wamegawana wagombea wa vyama vingine.
ReplyDelete50.1%?thats too close for comfort
ReplyDelete