Mkurugenzi wa shindano la Urembo liitwalo Giraffe Unique Modol 2010,Bw.Methuselah Magesse akizungumza mchana wa leo katika moja ya kumbi za hoteli ya Giraffe jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa shindano hilo linalotarajiwa kuanza hivi karibu.


Kampuni ya Unique Entertainment imeandaa shindano la uanamitindo linalojulikana kama Giraffe Unique Model 2010 litakalofanyika Desemba 24 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Unique Entertainment, Methusaleh Magesse alisema kuwa shindano hilo litajumuisha washiriki ishirini.

Alisema kuwa washiriki hao watapatikana katika mchujo utakaofanyika Novemba 20 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View.

Aliwataja majaji watakaohusika katika mchujo huo kuwa ni mbunifu maarufu wa mavazi nchini Ally Remptula, mwanamitindo Victoria Martin, Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald na mcheza filamu maarufu Steven Kanumba.

Alivitaja vigezo vitakavyotumiaka katika shindano hilo kuwa ni urefu wa futi 5’ 8’-6’, hips 35-37, kiuno 26-29 na kifua 32-35.

Vigezo vingine ni muonekano wa kiuanamitindo, kijiamini na umri 18-25, tabia njema na minato.

Aliwataka wasichana wenye sifa hizo kujitokeza Giraffe Hoteli Novemba 20 kwa ajili ya mchujo kupata washiriki 20 watakaoingia kambini katika hoteli hiyo Desemba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michu,
    Tuletee habari za uchaguzi. Haya mengine yasubiri. Hayana umuhimu kama uchaguzi wa nchi yetu.

    Nasikia Sugu kishatangazwa mshindi Mbeya Mjini.

    ReplyDelete
  2. Lete matokeo ya Uchaguzi achana na upumbavu huu wa nini??

    ReplyDelete
  3. Nbeya mjini hoyeeeeeeeeee....smart people do the right things

    ReplyDelete
  4. Ankal huoni kama hii habari inachafua hali ya hewa? Akatangazie kwenye magazeti ya urembo. Watu tuko serious na issue nyeti unatuwekea urembo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...