Mwanamuziki nguli toka Congo Kinshasa Bozi Boziana akiwa na mwanamuziki nyota wa kike Blessing Ayembe wakiongea na waandhishi wa habari baada ya kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport tayari kuungana na Twanga Pepeta kwa maonesho na kurekodi pamoja. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Twanga Pepeta Da'Asha Baaraka, Boziana na Blessing watafanya mazoezi ya pamoja na African Stars kabla ya kurekodi albamu ya pamoja katika mikakati ya bendi hiyo kupasua anga ya kimataifa. Picha na John Bukuku


Big up Twanga, fanyeni kolabo ya kufa mtu hapa kwani huu ndo wakati wa kujitangaza na manguli wa muziki. I can't wait to buy your album
ReplyDelete