JK akicheza na Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vunjo Mh. Augustine Lyatonga Mrema wakati wa mnuso wa kuwapongeza wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Mzee Yusuf ambaye kundi lake la Jahazi Modern Taarab lilikuwa likitumbuza.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hapo nyimbo gani ilikuwa inapigwa ? "mkuki" nini?

    ReplyDelete
  2. Siyo "nyimbo" wewe, ni wimbo.

    ReplyDelete
  3. Hii safi sana.Tuleteeni na video yake

    ReplyDelete
  4. Mrema ni mwanasiasa mpevu asiye na siasa za chuki wala uhasama. Anaangalia utaifa na si ubinafsi kama baadhi ya wanasiasa wa upinzani wafanyavyo. Hongera mzee wa kiraracha, mungu yuko nawe.

    ReplyDelete
  5. sirumba , Raisi alikuwa anacheza tarabu !! LOL

    ReplyDelete
  6. Wimbo wa alamba alamba alamba tena
    Safi sana ila anapiga makofi sijui.

    ReplyDelete
  7. URafiki wa mashaka.

    ReplyDelete
  8. wape wape vidonge vyao wakimeza wakitema shauri yao

    ReplyDelete
  9. Watu wanasema mrema kazeeka wakati anakata Rhumba namna hiyo...Endelea kutete haki za wananchi mzee wa kiraracha...

    ReplyDelete
  10. Wakati ukuta na kila jambo na wakati wake. Mzee Yusuf na tungo zake na staili yake anaburudisha kwenye dhifa ya Rais na Wabunge.

    Haya ni ya wakati huu. Wakati ule katika dhifa kama hii wangekuwa JKT na Mzee Issa Matona, Bia Hassan, Ali Mtoto Sefu, Elizabeth Sijira, Patricia Hilary na wengineo. Au Captain John Komba na kundi zima la JWTZ Cultural Troupe. Au Mzee Ramadhani Mwinamila na kikundi chake cha Hiari ya Moyo. Na Police, JWTZ, JKT au Magereza Brass Band.

    Natamani kuona jinsi waheshimiwa walivyokuwa wanasakata Mipasho ya Mzee Yusuf. Sijui na wao walikuwa wanasakata kama wanavyosakata mashabiki wa kule Lango la Jiji?

    ReplyDelete
  11. Mrema kanifurahisha sana maana inaonyesha hana chuki au hata kama anayo basi anachofanya hiki ni kitendo cha busara sana. Ijapokuwa mimi ni shabiki wa CCM lakini kwa roho yake hiyo ya kispoti ninamuombe dua Rais Kikwete ampe uwongozi katika serikali yake kwa sababu uwezo wa kulifanya hilo kisheria anao. Brema big up.

    ReplyDelete
  12. Je wabunge wa CHADEMA walisusia mnuso pia? I'm just curious...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...