Wagombea wakisubiri kujieleza


Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba akitaja majina matatu yatayopelekwa kuteua mgombea mmoja wa Uspika


Mh. Kate Kamba
Mh. Anna Abdallah

Mh. Anna Makinda

KAMATI KUU LEO IMEPENDEKEZA MAJINA MATATU YA WANA CCM WATAKAOGOMBEA NAFASI YA USPIKA KATI YA WAGOMBEA 13 WA CHAMA HICHO WALIOJITOKEZA. MMOJA WAO NDIYE ATAYETEULIWA KUSIMAMA KUGOMBEA BAADA YA KUPITISHWA

NAO NI MH. ANNA ABDALLAH,
MH. KATE KAMBA NA MH. ANNA MAKINDA.

MAJINA YA WANAOWANIA UNAIBU SPIKA YANATAKIWA YAFIKE OFISI ZA BUNGE KESHOKUTWA NOVEMBA 15, 2010.

KATIBU MKUU WA CCM AMESEMA SASA HIVI KWAMBA KAMATI KUU YA CCM IMEAMUA KWA MAKUSUDI KUMPA NAFASI MWANAMKE KUONGOZA MOJA WA MIHIMILI MITATU YA NCHI KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA JAMHURI YA MUUNGANO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Alitabiri Baregu kwamba haikawii gender aspect ikatumika. Mdau wa Bristol Uni.

    ReplyDelete
  2. Tumekwisha....bunge la kasi na viwango kwishnei!

    ReplyDelete
  3. Sasa jiandaeni tupate Rais wa Kike. Kazi ipo Tanzania. Anna Abdallah anafaa, nakuomba sana tena sana ukemee ufisadi. Ujue kuwa wanawake tunakosa haki zetu.

    Mdau USA Nusu na TANZANIA Nusu.

    ReplyDelete
  4. Maskini Samwel Sita pole sana. Watanzani tuko nyuma yako. Tunajua ni juhudi zako za kupambana na ufisadi ndizo zimesababisha hadi ukawekwa pembeni. Kama ni dhawabu iko kwa Mungu na sio kwa wanadamu, hivyo usikate tamaa. Nafasi ya kupambana bado unayo. Songa mbele. Nawapa hongere waliopendekezwa. Atakayeteuliwa naomba aige mfano wa Sitta.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Baba Sitta, najua wee ni mpiganaji sana bado una nafasi hata ya kwenda kuomba hiyo nafasi kama mgombea binafasi kwani katiba inaruhusu si lazima upitie kwenye chama,najua wabunge wengi tu wa ccm na upinzani watakusapport

    ReplyDelete
  6. Nyie mifumo dume mnaong'ang'ania Sitta, Sitta, mnata kusema hao wanawake hawafai? Anna Makinda, Anna Abdallah, hata Kate Kamba ni wanawake walioitumikia nchi hii kwa muda mrefu, nyie mnataka kila siku wanawake wawe wanashika nafasi ya unaibu tu?

    Kwa taarifa yenu safari hii na waziri mkuu ni mwanamke!

    ReplyDelete
  7. Haya na sisi tumpate Nacy Pelosi wetu hakuna lolote ni kuiga umarekani ...

    ReplyDelete
  8. im not into politics but im happy that Sitta is out of the game.as a woman im happy to see one among these three woman will be a speaker.now its our time,all Tanzania woman we should make sure we are going sambamba with wanaume.i cant wait to see members of parliament bungeni i think it will be like footbal match btwn CCM and CHADEMA.But all in all members of parliament u shld do what u said to us when u were doing the campaign.we are waiting for nguvu mpya kasi mpya in maendeleo

    ReplyDelete
  9. May the Best Woman Win!

    ReplyDelete
  10. Wanawake tunaweza!
    Let's wait and see!

    ReplyDelete
  11. ha ha ha wewe ... anonymous Wed Nov 10, 11:05:00 PM .... nancy pelosi wetu, hopefully CCM haitawakuta yaliyomkuta obama na dems 2010 .....republican si wamerudi juu tuu pamoja na record yao chafu!....2015 si mbali!

    ReplyDelete
  12. Najua bwana Michuzi hii utaibana kama ulivyofanya juzi. Hata hivyo nitaendelea kuandika! Hilo ni goli la kujifunga kwa chama tawala. Wanainchi wanaangalia kwa karibu sana. Nani hajui utaratibu ulio tumika hapa? Timu inayoendelea kushinda haitakiwa kubadirishwa!!

    Mimi kama mwana CCM ninaona hapa tunaendelea kuwapa nafasi wapinzani!
    Msemwa kweli ni mpenzi wa wote!!

    ReplyDelete
  13. HIYO NI JEURI YA FISADI. USIFANYE MCHEZO, UKISHINDWA KUTETEA MASLAHI YAO LAZIMA WAKUPIGE CHINI.KULIKUWA HAKUNA SABAU YA KUMTOA SITA KWENYE KITI HICHO WAKATI KUNA WATU WALIKIKALIA TOKA UHURU. SABABU IMETUMIA NI GENDER LAKINI UKWELI HALISI WANAUJUWA WANA CCM WENYEWE. KAHI NI NDOTO TANZANIA NA TUJIANDAE NCHI KUTAFUNWA KWA MIAKA MINGINE MITANOM MOAKA TUTAKAPOAMKA

    ReplyDelete
  14. bunge lina hitaji mtu kama chenge. this is a very serious place na si watu wa majungu. ccm acheni chuki na mumchague chenge. by now mmekwisha tambua kuwa chuki na wivu havileti maendeleo.

    ReplyDelete
  15. Huyu bwana Makamba simuelewi kabisa, yeye anasema wakati umefika kwa mwanamke kuongoza bunge, hivi hajui kwamba kuna uchaguzi wa spika kutoka vyama shiriki vya siasa?kwanini aseme wakati umefika,au pendekezo la ccm ndio linakuwa moja kwa moja hata kama kuna mshindi toka chama cha upinzani?

    ReplyDelete
  16. Mimi nampenda huyo aliyevaaa Nywele nachuro....siyo kuva mawigi...

    ReplyDelete
  17. Unaona tofauti ya mihimili hii mitatu inavyokuwa tofauti sasa?! Jaji Mkuu ni ajira ya kudumu -akiteuliwa mpaka astaafu. Rais akitaka kurudia term anapewa heshima na ukimpinga unaweza kufutwa chama. Speaker anatupwa nje kama hakuwahi ku-exist bila kujali heshima na mchango wake. Je bado hii mihimili ina nguvu sawa au ni serikali inataka kuvikanyaga vyombo vingine na hivyo inaandaa mazingira ya kuvitumia tu kwa kuwaweka watu ambao inadhani ama ni yes yes au ni mteremko kwao.....!!! Bado sana lakini tutafika tu

    ReplyDelete
  18. Tumuombee sana atakaechaguliwa kati ya hawa,kwasababu huwezi kujua kwamba je amechaguliwa kwa sababu zipi za msingi maana hiyo ya gender ni sababu mnayotupa sisi wasikilizaji lakini nyinyi mliowapendekeza hao, mnayo sababu kuu,na nzito ambayo ni siri yenu.Tunawapongeza kama mmewapendekeza hao kinamama kwa maendeleo ya Taifa.

    ReplyDelete
  19. We anony hapo juu....Si kwamba wanawake hawafai...ila kuna umuhimu wa kuwa na spika atakayeleta harmony na demokrasia pevu katika bunge hili lenye wapinzani wengi kihistoria.Kwahiyo hoja yako kuwa akina Anna A na Anna M eti wameitumikia nchi kwa muda mrefu so wapewe uspika haina tija.

    ReplyDelete
  20. Hongereni sana warembo. yaani ninauhakika mtawadhirihirishia kuwa hali inapokuwa ngumu wanawake ndo wanajuaga la kufanya mambo yaende sawa.

    ReplyDelete
  21. Jana TBC walimuhoji Kingunge akasema sifa za spika bora.

    Nanukuu awe spika anaye ruhusu hoja kujadiliwa bungeni bila kunogewa na kujikuta anajiingiza katika mijadala na pia kuruhusu mijadala ili aweze kupenyeza ajenda zake binafsi katika mijadala hiyo.

    Kauli ya Mzee Kingunge ni nzito na ninaomba atakaye kuwa spika, azingatie hilo.

    ReplyDelete
  22. ....Kazzi kwekwelii!! Ukianza kufilisika........inaanza "AKILI" kisha mali inapotea kidogo kidogo!
    Ukishtuka....ham'mad!......choka mbaya!!

    ReplyDelete
  23. Nancy Pelosi ama Mama Clinton safari atapatikana tu. Hata Liberia President tunaye safari. Kipange sawasawa. Nawashanga kwa nini hamukujitokeza mapema kupambana na JK. Mkawa kama Mama Clinton na Pres Obama. Sasa jiandae kwa ajili ya 2015. Wanawake tusilale amka wewe usinziaye uone mambo. Dr. Migiro katufungulia tuzidi kuamka.

    Narudi Tanzania nataka kuanzia Udiwani mpaka nifike Ikulu. Tutapambana Mungu ni mwema na muaminifu ataniongoza kwa rehema zake.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  24. hebu achen hoja zisizo na macho wala maskio, msishabikie tu kuwa ni wanawake. swala la msingi ni uwezo, mambo ya gender hebu yaweken pembeni, mimi naamini binadamu wote ni sawa, mwanamke ana uwezo sawa na mwanaume lakin sio ushabiki wa kihisia tu like mnavyofanya hapa. Toa maoni kwa kupima jamani na sio kihisia.Pia kutumikia nchi kwa muda mrefu sio kigezo, kigezo ni utendaji wa kazi na uadilifu. Tunataka mtu muadilifu asiye na uoga wa kukemea maovu, asiye na maslahali binafsi, akiwa mwanaume au mwanamke mie kwangu yote sawa tu.

    ReplyDelete
  25. mhmm kama zamu yako imefika! kalibu

    ReplyDelete
  26. WANAUME WATANZANIA WANAKUWAGA WAGUMUKUTAWALIA NA WANAWAKE HUO NDIO MWANZO . anna makinda sio fisadi

    ReplyDelete
  27. Hongera Kamati Kuu. Hongera akina mama. Naona mhe Rais anaanza kufanya vitu vyake. Hapa demokrasia ndani ya chama imefanya kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...