Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atatangaza Baraza la Mawaziri jipya kesho, Jumatano, Novemba 24, 2010.

Rais kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri hilo jipya kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu, 2010.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM
.
23 Novemba, 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mr. Michuzi asante kwa kutuletea taarifa hizi ambazo wengi tunazisubiri kwa hamu sana. Hata hivyo mbona tangazo siyo kamili? tunahitaji kujua muda. Mdau Tokyo

    ReplyDelete
  2. kweli nimekubari watanzania kwa sasa wanafatilia mambo,nimekuwa nikisikia watu wakiulizana hapa na pale kama baraza la mawaziri limeshatangazwa,hata hii ya kutangazwa kesho watu wamesha taarifiana,safi sana tunazidi kubadilika.TUJITAHIDI HATA KWENYE KUPIGA KURA,TUSIISHIE KUJIANDIKISHA ILI KUPATA VITAMBULISHO TU,BALI TUSHIRIKI KUCHAGUA WATU WATAKAO TUONGOZA NI HAKI YETU.

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru kwa taarifa hii, japo naona kama haijakamilika. Hivi kweli Ikulu imeshindwa kabisa kusema kuwa Mhe. Rais atatangaza Baraza saa ngapi? Kusema ni Jumatano ni kitendawili maana ni saa ngapi? Dunia ya sasa watu wanakwenda kwa muda hivi sio suala la siku tu, pia ni saa ngapi kwenye siku hiyo? Naomba next time tupate siku na muda pia....

    ReplyDelete
  4. Does it mean the government has not timing for its activities. Could I be informed abouit the specific time.

    ReplyDelete
  5. Saa ngapi wazee?

    Wengine tunasubiri kujisikia majina yetu redioni na kwenye tv.

    ReplyDelete
  6. nadhani hili tangazo si kamilifu mwandishi amekurupuka, mimi kama mkuu wa taasisi ya utangazaji nikitaka kutuma mwandishi wangu kuchukua habari hii NIMTUME WAPI NA SAA NGAPI? TAFADHALI WAHUSIKA TUKAMILISHIENI TAARIFA HIZO

    ReplyDelete
  7. Ni nani anachagua mawaziri? Ningelitamani mawaaziri wachaguliwe kutoka wabunge waliochaguliwa na wananchi tu na sio walioteuliwa. wanza hata sijui waliteuliwaje au na anani anafanya hii process? But anyway ndio bongo yetu na katiba inahitajika kubadilishwa sana....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...