Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo. Picha na mdau Clarence Nanyaro wa VPO
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Profesa Idrissa Kikula akimweleza jambo Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo hicho mjini Dodoma leo. Kulia ni Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo kikuu cha Dodoma. Picha na mdau Clarence Nanyaro wa VPO


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa wakikata utepe kuashiria kuazindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ndiye Mkuu wa chuo cha Dodoma, na Dk. Bilal ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chuo hicho. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Dr Michuzi,

    Hivi Dr B. W. Mkapa hakuwahi kupata udaktari wa falsafa wa heshima ili na yeye tuanzae kumwita Mheshimiwa Rais Mstaafu Dr Benjamin William Mkapa? Na Mtukufu Rais Mstaafu Dr Ally Hassan Mwinyi je? Nakumbuka Nyerere alipewa nyingi tu. Tafadhali anza kumwita Mheshimiwa Mwalimu Dr Nyerere Kambarage Nyerere.

    Ni maoni tu, Mkuu Mheshimiwa Photojournalist Dr Issa Michuzi. Nia siyo kuchafua hali ya hewa. Usinitupe kapuni.

    Ni mimi,
    Dr Kalikali

    NB: Tuwekee article nyingine ya Dr John Mashaka na pia za Engineer Dr US Blogger na Mh Dr Shayo ili tuelimike.

    ReplyDelete
  2. Nimemsikilaiza Mheshimiwa kwa utulivu sana. Kaongea mazuri kuhusu IT na microsoft, ni vizuri sana. Lakini itakuwa na maana gani kuwasha kompyuta usiku tu wakati mgao ni muziki wa kila siku? Tafadhali Mheshimiwa angalia suala ya Umeme na Maji kwa karibu.

    ReplyDelete
  3. Kaka Kalikali nimecheka sana, nimebatasamu! Kwakweli kule nchi za nji maprofesa na Dokta wengi wanajiita kwa majina tu. Lakini huku ukipata honorary doctorate, basi Dr.So and So kotekote. Naona Dr. Itumike kwa madaktari wa afya tu!

    ReplyDelete
  4. Heshima ya u Dk inavyotumika hapa nyumbani ni ishara ya ufisadi. Najua Dr Issa Michuzi ataitia kapuni hii.

    ReplyDelete
  5. Acheni wivu wabongo! Mtu akiitwa prof. Dr (PhD). Eng. Mwakipesile inawapunguzia ninii? Kwa vile huko mjini watu wanaitwa Asukile tu (hata Sir name haitajwi) ndo tuige tu? Acha bwana Bongo kupata hiyo Dr. hata ya Heshima tu si Mchezo!! Mtu unaenda huko mjini kusaka master ukiwa na 30 years unakuta supervisor wako ana umri kama huo na ni full professor... Acha bwana wenye nazo watambe!

    ReplyDelete
  6. Habari Dr.Issa Michuzi,

    vipi tupe habari nyumbani huko wamepokeaje baraza jipya la mawaziri?

    ReplyDelete
  7. MICHUZI ITAKUWA BUSARA SANA UWE UNACHUJA HIZI COMMENT ZA KIJINGA, KAMA MTU HUNA COMMENT SI LAZIMA UANDIKE TU ILI KUONEKANA. KUNA MAANA GANI KUANDIKA KISHA UNAOMNGELEA ETI MTU KUITWA DOCTOR, ACHENI USHAMBA NA WIVU USIO WA KIMAENDELEO. COMMENT ZIWE CONSTRUCTIVE KUONYESHA UKOMAVU WA KI UTU UZIMA.

    ReplyDelete
  8. Nahisi ulimaanisha ni Chuo Kikuu cha Dodoma na sio Chuo Kikuu cha University of Dodoma.


    Msahihishaji wako wa kila siku.

    ReplyDelete
  9. TUNAWAPONGEZA VIONGOZI WETU KUZIDI KUTANUA UWANJA WA ELIMU MAANA NDIO UFUNGUO WA KILA KITU, KUHUSU KUITWA DR, ASANTE ANON 11.21PM HAWA WATU WANA CHUKI BINAFSI HAWANA JIPYA,NA WAITWE DR MADAKTARI TUU HAIWEZEKANI PIA MAANA KUNA DR,(Dr,Slaa)WA SHERIA ZA KANISA UTAMWITAJE?NA KUHUSU MGAO HIVI UKO DUNIA GANI WEWE? BIDII ZINAZOFANYWA HUZISIKII NA MATATIZO YALIYOZUKA NI WA MUDA TUU WACHENI HIZO KILA KITU KWENU KUTIA ILLA NA NONGWA?

    ReplyDelete
  10. Ndg Michuzi hebu tupe data za ukweli Chuo cha Dodoma UDOM kilianza wakati wa awamu ya 3 au 4 naomba jibu tafadhali

    ReplyDelete
  11. AWAMU YA NNE YA UTAWALA WA JK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...