Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa wakikata utepe kuashiria kuazindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ndiye Mkuu wa chuo cha Dodoma, na Dk. Bilal ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chuo hicho. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Home
Unlabelled
JK afungua rasmi chuo kikuu cha UDOM leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dr Michuzi,
ReplyDeleteHivi Dr B. W. Mkapa hakuwahi kupata udaktari wa falsafa wa heshima ili na yeye tuanzae kumwita Mheshimiwa Rais Mstaafu Dr Benjamin William Mkapa? Na Mtukufu Rais Mstaafu Dr Ally Hassan Mwinyi je? Nakumbuka Nyerere alipewa nyingi tu. Tafadhali anza kumwita Mheshimiwa Mwalimu Dr Nyerere Kambarage Nyerere.
Ni maoni tu, Mkuu Mheshimiwa Photojournalist Dr Issa Michuzi. Nia siyo kuchafua hali ya hewa. Usinitupe kapuni.
Ni mimi,
Dr Kalikali
NB: Tuwekee article nyingine ya Dr John Mashaka na pia za Engineer Dr US Blogger na Mh Dr Shayo ili tuelimike.
Nimemsikilaiza Mheshimiwa kwa utulivu sana. Kaongea mazuri kuhusu IT na microsoft, ni vizuri sana. Lakini itakuwa na maana gani kuwasha kompyuta usiku tu wakati mgao ni muziki wa kila siku? Tafadhali Mheshimiwa angalia suala ya Umeme na Maji kwa karibu.
ReplyDeleteKaka Kalikali nimecheka sana, nimebatasamu! Kwakweli kule nchi za nji maprofesa na Dokta wengi wanajiita kwa majina tu. Lakini huku ukipata honorary doctorate, basi Dr.So and So kotekote. Naona Dr. Itumike kwa madaktari wa afya tu!
ReplyDeleteHeshima ya u Dk inavyotumika hapa nyumbani ni ishara ya ufisadi. Najua Dr Issa Michuzi ataitia kapuni hii.
ReplyDeleteAcheni wivu wabongo! Mtu akiitwa prof. Dr (PhD). Eng. Mwakipesile inawapunguzia ninii? Kwa vile huko mjini watu wanaitwa Asukile tu (hata Sir name haitajwi) ndo tuige tu? Acha bwana Bongo kupata hiyo Dr. hata ya Heshima tu si Mchezo!! Mtu unaenda huko mjini kusaka master ukiwa na 30 years unakuta supervisor wako ana umri kama huo na ni full professor... Acha bwana wenye nazo watambe!
ReplyDeleteHabari Dr.Issa Michuzi,
ReplyDeletevipi tupe habari nyumbani huko wamepokeaje baraza jipya la mawaziri?
MICHUZI ITAKUWA BUSARA SANA UWE UNACHUJA HIZI COMMENT ZA KIJINGA, KAMA MTU HUNA COMMENT SI LAZIMA UANDIKE TU ILI KUONEKANA. KUNA MAANA GANI KUANDIKA KISHA UNAOMNGELEA ETI MTU KUITWA DOCTOR, ACHENI USHAMBA NA WIVU USIO WA KIMAENDELEO. COMMENT ZIWE CONSTRUCTIVE KUONYESHA UKOMAVU WA KI UTU UZIMA.
ReplyDeleteNahisi ulimaanisha ni Chuo Kikuu cha Dodoma na sio Chuo Kikuu cha University of Dodoma.
ReplyDeleteMsahihishaji wako wa kila siku.
TUNAWAPONGEZA VIONGOZI WETU KUZIDI KUTANUA UWANJA WA ELIMU MAANA NDIO UFUNGUO WA KILA KITU, KUHUSU KUITWA DR, ASANTE ANON 11.21PM HAWA WATU WANA CHUKI BINAFSI HAWANA JIPYA,NA WAITWE DR MADAKTARI TUU HAIWEZEKANI PIA MAANA KUNA DR,(Dr,Slaa)WA SHERIA ZA KANISA UTAMWITAJE?NA KUHUSU MGAO HIVI UKO DUNIA GANI WEWE? BIDII ZINAZOFANYWA HUZISIKII NA MATATIZO YALIYOZUKA NI WA MUDA TUU WACHENI HIZO KILA KITU KWENU KUTIA ILLA NA NONGWA?
ReplyDeleteNdg Michuzi hebu tupe data za ukweli Chuo cha Dodoma UDOM kilianza wakati wa awamu ya 3 au 4 naomba jibu tafadhali
ReplyDeleteAWAMU YA NNE YA UTAWALA WA JK
ReplyDelete