
Chuo Kikuu Cha Dodoma leo kimewatunuku Shahada ya Heshima ya
Udaktari (Doctor Honoris Causa) Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa kutambua michango yao mbalimbali katika Nyanja za siasa na sekta za elimu nchini ikiwemo kuasisi ujenzi wa Chuo hicho. Pichani ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, akimtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari Rais Dr.Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo. Katikati ni Makamu mkuu wa Chuo Profesa Idriss Kikula
Kula Nondoz Mkuu wa Kaya! Kazi kubwa unafanya katika nchi yetu, Hongera sana!
ReplyDeleteHongera sana Mheshimiwa Rais Dr Dr Dr J Kikwete. Hongera pia Mheshimiwa Dr BW Mkapa.
ReplyDeleteDr Kalikali
NB: Nina swali Dr Michuzi. Naomba wadau wanisaidie. Hivi siku hizi Dr Remi Ongala yuko wapi? Simsikii.
Ninampa Dkt JK hongera. Sina tabu na JK kutunukiwa PhD ya heshima, lakini kama wahusika wangevuta subira kidogo, wakazalisha angaa PhD moja ya kusotea kitabu (ninaomba kusahihishwa na kufuta hoja yangu kama wameishafanya hivyo) kabla ya kuanza utotoaji wa PhD za heshima, ingeashiria walivyokuwa serious. Hii inadhihirisha wasiwasi ambao umekuwa ukielezwa na baddhi ya wadau kuhusu mustakabali wa UDOM kitaaluma!!!!
ReplyDeleteHonoris Causa in what? Michuzi waulize wenzako mseme kitu kilichokamilika. Hakuna Honoris Causa kavu kavu.
ReplyDeleteHalafu ile uliyosema GPA 4.5 pale kwenye picha na Pinda ya UDSM, badilisha hakuna kitu kama hicho duniani, labda Bongo tu kwenue ufisadi. GPA ya mwisho ni 4.0.
Swali jingine, kwa hiyo JK sasa atakuwa Dr. Dr. Jakaya Kikwete?
bravo JK,wewe unastili hiyo nondo,maana chuo kikuu cha dodoma,ni juhudi zako binasfi,kilikuwa hakiko katika ilani ya uchaguzi wa ccm 2005 2010
ReplyDeleteHuyu atakuwa Mkwere wa kwanza kwa kuwa na vyeti vingi vya kutunukiwa na vyuo mbalimbali Nchini na Duniani.
ReplyDeletemkuu tembelea Mzumbe kuna gap ya mikopo sijui uongozi una njama gani.wanafanya mitihani na njaa na wanaitwa kuanza vyuo bila hela na wengi ni masikini wa kutupwa kama huna means unakula polisi.
ReplyDeleteMkuu wa kaya ni msomi kweli. Sasa amekuwa Dokta dokta.
ReplyDeleteJAMANI INGEKUWA KAMA WALAO NI CHUO KIKUU CHA MLIMANI INGEELEWEKA, SASA CHUO HICHO AMBACHO HATA HAKIJATENGAMAA NA JANA TU ALIKUA AMEKIFUNGUA NA KISHA MFUNGUAJI WA CHUO KUPATA DEGREE YA HESHIMA PAPO KWA PAPO HAPO SIJAWAPATA BADO.
ReplyDeleteHIVI TANZANIA TUNAENDA WAPI SASA? MIPANGO KAMA HII NDO TUNAINUA ELIMU YA NCHI AU NI SHAURI YA KUIGA KUTUNUKU HESHIMA WATU?
KAZI IPO
Anonymous wa 11:33:00 PM, hivi wewe ni mtanzania kweli? Je unaujua mfumo wa Elimu ya Tanzania? au ulizaliwa tu tanzania ukatokomea nje sasa ona unaumbuka hata hujui kuwa nchini kwako GPA inaishia 5.
ReplyDeleteAnd thats why there are diffrernt grade scales; 4.0, 5.0 etc. all you need to do is convert your GPA to other scales to get your equivalent score.
Yaani sijui hata nikusaidieje... jitahidi kufanya utafiti kabla hujamcrush mtu, ndo maana nivizuri always kuwa polite na kuongea bila kujifanya much-know.
Nakuonea huruma sana.
Ni hayo tu.
Dr Kalikali umesahau kuwa na Profesa maji marefu yumo ndani ya bunge mwaka huu mambo mswano.
ReplyDeleteDr Hamnazo
Napipomgeza Serikali kwa juhudi wanazofanya za kukuza elimu nchini na Chuo Kikuu Dodoma ni mfano wa kuigwa? Je maandalizi gani Serikali inafanya kwa ajili ya wasomi hawa? Pia pale UDOM kunahitaji ukarabati mkubwa sana wa mitambo ya maji ili kuwe na green areas. Ni pakavu sana pale na kuna upepo mkali wenye vumbi jingi. Upandaji miti viti? Tusiishie kujenga tu majengo, tutengeneze mazingira pia. Hongera JK kwa kupewa PhD na Ben.....Sasa itabidi uonyeshe kweli kama ulistahili kupewa au la. Jenga uchumi wa nchi sasa. Shilingi inazidi kuporomoka na vitu vinazidi kupanda bei. Najua JK ni mchumi lkn, mh....
ReplyDeleteHii inaonyesha wazi watanzania wengi ambao tunajifanya tunajua kutumia mtandao lakini hizi comments zinaonyesha dhahiri ujinga wetu. Myahudi katunga Google kuwapata wajinga kama nyinyi. masuali yanayoulizwa humu mengine bora kuyavumilia tu maana yanadhihirisha level ya somo la maarifa ya watanzania. Jamani jifunzeni kutumia mitandao. Google yupo kwa nini uhangaishe bongo kuwaelimisha watu wasioelimika. Hebu bonyeza anavyokueleza honoris causa. Halafu msiseme mimi ni mdini, lakini hizi digrii chimbuko lake limeanzia kanisani ambako ndiko askofu alikuwa (enzi hizo) na madarka ya kumpa mtu digrii za bure bila ya kuhenya. Anyway hata haya magauni, MTANDIO na TASSEL(hood na kofia) wanayovaa katika mahafali chimbuko lake ni kanisani, sisi hatujavumbua gurudumu, tunaiga tu. Historia ipo hivyo muulize google atakupa habari zote. BILA YA KUHENYA AMA KWA KITABU AU KUWA NA MCHANGO MKUBWA (KWA KANISA ENZI HIZO) AU KWA JAMII KWA KUWASAIDIA JAMII DIGRII HII HAIPATIKANI.
ReplyDeleteHICHO KIKAO CHA KUMCHAGUA MTU WA KUMPA HONORIS CAUSA KINACHAMBUA SIO CHINI YA MAJINA YA WATU MAARUFU NA WENYE MICHANGO MBALI MBALI KITAIFA NA KIMATAIFA SIO CHA MTAANI AU CHA CHAMA CHA SIASA, NI WENYEWE WENYE HAYO MA MADIGRII YA PHD WALIOYAHENYEA NDIO WANA MADARAKA YA KUZIGAWA PHD ZA BURE. MBONA WENYEWE HAWALALAMIK.
Katika marais wa kimarekani wajinga ni Benjamin Franklin, yeye aliizamisha apewe na aliokwishapewa akawa anajiita
Dr. Franklin.
THIS SAYING IS TRUE: "YOU CAN TAKE AN AFRICAN FROM THE BUSH BUT YOU CANNOT A BUSH FROM AN AFRICAN"
udomm mumuite na obama mumpe moja...
ReplyDeleteUncle hujakosea kusema yule binti kapata G.P.A ya 4.6
ReplyDeleteAnonymous wa 11:33:00 PM ni sijui wa wapi huyo na hajasoma Tanzania.
Mimi ni mhitimu wa UDSM mwaka 2006.Grade Point Average (G.P.A)inayotumiwa na U.D.SM na vyuo vingi Tanzania ni 5.0 scale tofauti na vyuo vingi vya Ulaya ambapo G.P.A ni 4.0 scale.
Mchanganuo ni kama ifuatavyo
2.0 - 2.6 Pass Degree
2.7 - 3.4 Lower Second Degree
3.5 - 4.3 Upper Second Degree
4.4 - 5.0 First Class Degree
Yule binti alipata G.P.A ya 4.6(First Class)
Nakushauri Anonymous wa 11:33:00 PM ukiwa unapata muda uingie google.com uperuzi mambo mbalimbali kuongeza ufahamu wako.Ona sasa ushaumbuka