Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala katika hafla ya uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya Chuo hicho zilizofanyika leo katika ukumbi wa Nkurumah.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Bi. Salome Maro ambaye ni Mwanachuo aliyefanya vizuri na kupata daraja la kwanza akiwa na GPS 4.5 katika kozi ya Computer Science kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Waziri Mkuu Alikuwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Sherehe za Miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam iliyofanyika katika ukumbi wa Nkrumah leo.
Waziri MkuuMizengo Pinda akiongozwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Fulgence Kazaura (kushoto), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala kuelekea kwenye ukumbi wa Nkurumah ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jamani ni GPA na sio GPS, GPS ni Global Positionning System, kwa bongo bado

    ReplyDelete
  2. Ankali nimecheka kinoma, GPS badala ya GPA hii ni kali!!!

    By the way: GPS = Global Positioning System. Ni mfumo wa satelaiti unaokuwezesha kujua uko wapi kijiografia.

    Na GPA = Grade Point Average. Ni mizani ya kupima ufaulu inayotumiwa na taasisi za elimu ya juu.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha kwamba katika habari yote hiyo kwa picha, kinachoonekana ni typing eror! Hivi hamna tiba ya fikra kama hizo?!

    Hongera UDSM kwa kutimiza umri wa kustaafu na Hongera Mdada kwa kutikisa Mlimani 4.5?!

    ReplyDelete
  4. hongera mdada kwakweli 4.5 iz not a joke,..haya miaka 50 down the line i hope viongozi wana mkakati zaidi ya kusherehekea yani wa improve uko halls of residence tumechoka kuning'ia vyooni looh

    ReplyDelete
  5. Nakupongeza sana dada yangu japokuwa sijawahi kusikia GPA ya 4.5, ninachojua mimi GPA huwa inaishia 4.0 labda kwa Tanzania, kazi ipo kweli na huu utoaji wa PHD wakati chuo chenyewe hakitoi PHD

    ReplyDelete
  6. GPS???Naona karibia tunapaa. Nimejaribu GPS bongo mwaka jana 2009 ikawa hakuna ramani ya kudownload, location unknown ndio error nililopata. Halafu huyu mdada kapiga 4.5 out of 4?? LOL . Kichwa kitakuwa si mchezo hiki. Kweli Chuo Kikuu cha University ya Dar-es-Salaam kiboko. Ni chuo kikongwe kabisa africa, vichwa vyote muhimu vimepita hapo:

    ReplyDelete
  7. Kuna kitu kimoja nashindwa kuelewa, hzi GPA za juu kwa bongo ni chache sana au hata hakuna wakati mwingine, lakini nchi kama India, bangladesh watu wanazo kibaoo je ni system yetu mbovu au za kwao ni mbovu(kupeana na za kununua?)

    ReplyDelete
  8. GPS Plus 4.5 OMG...Is real or Just Fununu As Usual...i guess 4.0 GPA...Unless Otherwise kama kawaida Bongo kisiwa cha wapendanao...!!

    ReplyDelete
  9. Dada yetu kafanya vema sana. Ila GPA ya Bongo ni 5.0 (Maximum). Nakumbuka mwaka wetu nilipomaliza pale UDSM, maiaka kama 6 iliyopita, kuna watu 2 ninaowajua kwa majina, walikuwa na 4.5 na hawakupata hata kuwa T/A sababu mwaka huo watu walifikisha 4.8, 4.9 na moja ilikuwa 5.0

    Kwa mifumo ya mahali pengine, the highest (maximum) ni 4.0 na watu wanafikisha 4.0 kama mchezo. Ukibadilisha hiyo 4.5 kwa viwango vya mifumo ya 4.0, unaweza kukuta huyo dada ana 3.7.

    HONGERA SANA DADA

    ReplyDelete
  10. Anko mithupu huyo mdada alipata G.P.A ya 4.7 na sio 4.5 kama ulivyoandika hapo juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...