Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.
MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hiyo ni preview ya baraza la mawaziri. Meghji anarudi fedha au unaibu waziri mambo ya nje na Nahodha mambo ya Ndani halafu Prof. Makame Mnyaa Mbarawa naibu fedha.

    ReplyDelete
  2. Too much speculations Msemakweli, how do you know that? You need to put your facts together before you come up with this type of speculations. I am not a fun but let the man do his job.

    ReplyDelete
  3. Speculation za Msemakweli zina sura ya ukweli. Lazima kuna watakaopewa uwaziri katika orodha hiyo.
    Sijakata tamaa, bado kuna nafasi saba.

    ReplyDelete
  4. hivi Spika ni ANNA S. MAKINDA AU ANNE S. MAKINDA? HUU UBATIZO UMETOKEA LINI?

    ReplyDelete
  5. Uteuzi wa Nahodha unafurahisha, the guy is still young and energetic, angeachwa ni kupoteza nguvu kazi! Bravo

    ReplyDelete
  6. Hongera!! Nimefurahi kumuona huyu mama, ni mchapa kazi na muadilifu. Japo kuna wakati watu walijaribu kumchafua kwa mambo ya sio na ukweli. Hongera Zakia...CCM tunakuitaji!!!

    ReplyDelete
  7. Msemakweli,
    Pole sana kwa kushiriki siasa za shangwe. wewe sio mshauri wa Rais,msemaji wa Ikulu lakini umerukia kunadi na kuthibitisha hisia zako kwa umma. Ulichokifanya sio DHAMBI ila una recruit mjengo wa fikra zisizo tendaji na hujapima kiasi gani utaathiri fikra za wengi wasio jua utaratibu.

    Iwe hivyo isiwe hivyo mwache Mhe. Rais atekeleza madaraka aliyo pewa na Katiba.

    Naogopa kuwa na rafiki kama wewe.

    Maina Owino.

    ReplyDelete
  8. Ahh, mdau hapo juu kula tano, yani inajulikana saana kuwa spika wa punge jina lake ni ANNA MAKINDA, ila kuna mbumbumbu mmoja akaandika anne makinda, ndio kila mtu anafata nyayo ingawa wanajua wazi jina la huyo mama ni anna makinda na si anne!!!! Hadi ankal naye yumo katika ubofoaji huu!!

    ReplyDelete
  9. Unayejiiata Msemakweli umepiga ramli kujua baraza la mawaziri au ni mfagizi mbea wa ofisi ya mzee?

    Wacha hizo za miaka ya 90 amabpo housegirl alikua anajua maamuzi ya waziri kwa vile mumsimulia mai waif wake na waif husimulia watoto na housegirl.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...