Katibu mkuu wa CUF Mallim Seif Shariff Hamad akimpongeza JK baada ya Dr.kikwete kuapishwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar
Rais joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpongeza Rais Dr.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kuapishwa
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe(kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Dr.Jakaya Kikwete katikati pamoja na makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal ikulu jijini Dar muda mfupi baada ya sherehe za kuapishwa zilizofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe(kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Dr.Jakaya Kikwete katikati pamoja na makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal ikulu jijini Dar
JK akiwa ikulu jijini Dar katika picha na pamoja na marais waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake.kutoka kushoto ni Rais Rupiah Banda wa Zambia,Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini,Rais Mwai Kibaki wa Kenya na Rais Josepha Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC
JK akiwa kazini ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuapishwa kuendelea kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kazi ya kwanza aliyoitekeleza Rais ilikuwa kumteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Jaji Frederick Werema aliteuliwa na kuapishwa kuendelea kushika wadhifa huo.div>


Mie nawapongeza sana CUF na CCM sababu wamejali wananchi wao katika kukubali Serikali si Chama tena jamani lazima tumkubali Raisi wetu.
ReplyDeletejamani! te! te! kumbe mtu akiwa na mvi harafu akivaa suti anapendeza kweli utu uzima dawa,waheshimiwa wamependeza
ReplyDelete"Mbaazi ukikosa maua husingizia jua",pole Dk S raha.
ReplyDeleteZaununu-Amsterdam
HA ha ha, nimeipenda hiyo ya Mbaazi ...Hongera CUF hongera CCm... Silaha umesusa wenzio wala!!!
ReplyDelete