OFF SIDE ni filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kuingia katika soko la filamu Tanzania, ikiwa inaigizwa na wasanii mashuhuri wa hapa nchini Steven Kanumba, Vicent Kigosi na Irene Uwoya itazinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ikiwa inasambazwa na Steps Entertainment, hii inaonekana kwamba wasamabzaji hawa wanajribu kupanua soko kwa kuweza kushirikisha wadau wengi katika filamu. Kuvuka mipaka ni hatua kubwa katika Tasnia ya filamu Tanzania.

Steven, Vicent na Irene wataelekea huko wakiambatana na wasamabzaji wao na utafinyika uzinduzi mkubwa na wa mara ya kwanza kutokea katika Tasnia ya filamu Tanzania. Steven na Vicent wanaandika historia Tena. Congo kaeni mkao wa kula, Filamu hilo linakuja karibuni. Tarehe mtatangaziwa...
kwa habari hii na nyingine kibao za filamu za Bongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hongera wacheza sinema wetu kwa juhudi zenu,mmefanya vizuri kuanza kujitangaza nje ya mipaka yetu,ushauri wangu tu mpunguze starehe na kashfa zinazojitokeza kwenye magazeti kila tusomapo,kila mara mnasikika mara billicanas mara mango mara ttc chang'ombe na humo mote ni kashfa tupu,haieleweki kama maisha yenu siku zote huwa mnashinda kwenye mabaa !!!??nyinyi ni kioo cha jamii inabidi muangalie sana mnavyoishi ili mjijengee heshima katika jamii na siyo kashfa kila siku inatia kichefu chefu.
    mdau Haagendaa,Holland

    ReplyDelete
  2. Kutangaza nje ya Tanzania sio tatizo, tatizo liko pale kwenye hadhi ya hizo movie je zinafikia world class market? Mimi nilikua TZ kama miezi miwili iliyopita nikarudi na dvds 26. Tulikaa chini na kuangalia na kufurahia sana lakini mambo kuna mambo mengi yanahitaji kurekebishwa sana. Mimi kama mteja itanibidi nikiwa tena TZ nijiulize je niko tayari kuangalia hizi movie kama mambo ndio hayo hayo?

    Kama mkijirekebisha kweli mtafika mbali lakini msiposikiliza maoni ya wateja itachukua miaka 200 kukubalika kwenye soko la ulimwengu..

    1. Jitahidini kusqueeze movie nzima kwenye DVD moja. Mkijitahidi kuedit na kukata mambo yasiyo na muhimu movie moja itaingia kwenye dvd moja. Kama ni pesa hiyo hela nilizotumia kununua dvd mbili part one and two ni sawa ya dvd moja huku niliko.

    2. halafu soko la ulimwengu mujiulize hao watu wanamuda wa kuangalia movie kwa masaa sijui mangapi. Part one and two sijui ni masaa 3 au manne. Ni refu sana na ukiangalia kuna mambo mengine either mngeyafupisha au kuyaondoa.

    3. Tittle za kizungu kwenye movie ya kiswahili wala haiwaengezei market kabisa. Sana sana inawapunguzia sifa. Mimi ni mpenzi wa foreign movies na zote ninazokuwaga na rent (Spanish na french) Zote zimeandikwa kwa lugha yao. Lakini movie kama ni nzuri utaipenda tu hata kama hujui hicho kilugha chao.

    4. Sioni sababau ya waigizaji wengine waongee kingereza katikati ya movie na kujibiwa kwa kiswahili. Kama ni movie ya kiswahili basi wote muongee kiswahili kama ni kudhungu basi wote muongee kidhugu.

    5. Mkiwa mnatafsiri na kuandika pia muwe mnafanya spell checking. Nadhani huyo aliyeandika script awe ana edit au muajiri mtu mwenye kujua kidhungu aandike. Movie zote zilizokua zimeatafsiriwa zilikua na makosa mengi sana.
    a. tafsiri ya lugha ilikua mbovu
    au b) spellings nyingi sana zilikosema

    Sasa ukimuuzia mtu mwenye lugha yake na wakati umeiharibu hata kuamini.

    6. Msiane na hili na kumaliza na lile. Yaani karibu movie zote nilizoziangalia zina mix messages.(bado sijamaliza zingine) Hadithi moja inaanza na habari hii ukienda part 2 habari imebadilika. Ni heri mkianza kurecord movie halafu mkifika katikati mnapata idea nyingine msikubali kabisa kubadilisha....sticky na kile kile ulichoanza nacho. Na hiyo idea nyingine mnaifanya iwe movie nyingine ..
    Idea mnazo sana tu lakini kuexecute ndio bado kazi ipo.



    Michuzi ukitupa hii hupendi wenzako waendelee na ujue kuna vipindi kibao huku (movie critics reviews) sasa nitashangaa nikiona umeiweka kapuni....

    ReplyDelete
  3. Mdau anon wa Tue Nov 30, 05:45:00 AM
    safi sana.

    Na kuongezea hapo namba sita, sababu haswa ya kuanza na hili na kumaliza na lile ni pale muvi inapoanza kutengenezwa wakati script haijakamilika.

    Madirector wa Bongo msikubali kuanza kushuti muvi ambayo script yake haijakamilika.

    Kama muvi itakuwa na part 2, basi hakikisha script ya part 2 nayo iko tayari ndio uanze kushuti part 1.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...