Mkutano mkuu wa kwanza wa kufunga mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome ulifanyika wikiendi iliyopita kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Italy, uliopo mjini Rome. Mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa ni Naibu Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh.Salvator Mbilinyi.
Agenda ya mkutano huu ilikuwa kuangalia na kujadili mafanikio na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye kipindi cha mwaka mzima wa Jumuiya. Watanzania walijitokeza kwa wingi na kuongelea maswala mbalimbali ambayo waliona yatawasaidia kwenye mwaka mpya wa Jumuiya.

Jumuiya ya Watanzania Rome, inapenda kutoa shukrani kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy kwa ushirikiano waliouonyesha kwenye kufanikisha mkutano huu.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Kwa picha na habari zaidi tafadhali tembelea blog ya Jumuiya hapa:
www.watanzania-roma.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya ni mambo mazuri lakini je kwa watu waishio kama Verona ama maeneo ya Bolzano itakuwaje ? fanyeni marekebisho kuna kitu katika blog yenu hakisomeki vizuri ´ quelli che vivono al di fuori di Roma´Sentensi ina mashaka kwa kuwa AL DI FUORI haikubaliki na pia kuna neno Mensilmente amapo hili ni MENSUALMENTE....hongreni kwa jumui yenu.
    mdau WESTENDE-BELGIE

    ReplyDelete
  2. ndugu mimi Nipo Italy kwa muda wamiaka 30 mjini Cesena..unahakika na maneno ya kitaliano uliyoaandika hapo juu??sei sicuro che la parola mensualmente essiste puo sostituire la parola mensilment in quello frase. Grazie aspetto le risposte!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...