Miss Earth Tanzania, Rose Shayo

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth 2010, Rose Shayo
aliondoka nchini leo kwenda Vietnam huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.


Akizungumza kabla ya kuondoka, Rose alisema kuwa amejiandaa viliyvyo chini ya muandaaji ake, Maria Sarungi wa Compass Communications and bila shaka atafanya vyema katika mashindano hayo.

Rose amesema kuwa haendi kuwa msindikizaji katika mashindano hayo na atafanya kila aliwezalo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Miriam Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.

“Najua kuna kushinda na kushindwa, mimi sitarajii kushindwa kutokana na
maandalizi yangu, nawaomba Watanzania wanipe sapoti kubwa wakati wote nikiwa kambini na siku ya mashindano,” alisema Rose.


Maria alisema kuwa, alisema mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano ya kumsaka mrembo huyo yalifanyika mapema mwaka huu.

“Mashindano ya kumsaka mrembo huyu yalifanyika tangu mwezi wan nne mwaka huu kutokana na hali hiyo alipata muda mwingi wakujiaandaa hali inayomuweka katika nafasi nzuri ya kushinda, tutarajie ushindi kwakweli,” alisema Maria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. sio yale yale ya kwetu kama tulivyozoea? haya kila la heri mpendwa kaza buti

    ReplyDelete
  2. Tunakuaminia, kila la kheri!

    ReplyDelete
  3. Masanduku hayo, na uzito mmmm

    ReplyDelete
  4. whatever!!!!!!!!! na upuuzi huu tumechoka nao!!!!!!!!! nini faida ya haya?

    ReplyDelete
  5. Ukifika huko utakua umepauka kweli. Kinguo hicho kwenye ndege???...mhhhh...
    Bongo twahitaji big crush course. Please kwenye ndege dress defensively, not decoratively and dress in layers.

    Mjue hayo mashindano yao wanaanzaga kuwapa point once unapopokelewa huko.

    ReplyDelete
  6. Toba. Kusafiri kwangu kote kwa ndege sijawahi kuona msafiri amevaa vile. Sijui watu watajifunza lini.

    ReplyDelete
  7. 'Personality has got No weather', mwacheni huyo Miss hivyo ndivyo waandaaji wanatarajia huyu model avae sio nyinyi majaji uchwara. Kama umesafiri sana na ndege itusaidie nini wakati kila siku tunaona wazungu na vichupi vyao wanashuka airport?

    ReplyDelete
  8. Lundenga, Chips na Maria nani zaidi? yaelekea huyu mama anawatayarisha hawa mademu tofauti na wapogolo hao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...