KIROMO VIEW HOTEL & RESORT YATOA UDHAMINI
WA 150,000,000.00 KWA MISS UTALII TANZANIA 2010
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiromo View Hotel & Resort Bw. James Nicholaus akiongea katika moja ya hafla nyingi zinazofanyika hotelini hapo. Kuhusu kiota hiki BOFYA HAPA
Hoteli ya kitalii ya Kiromo View Hotel and Resort iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, imethibitisha kudhamini fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2010.Hoteli hiyo imethibitisha kudhamini kambi ya warembo 60 kwa siku 21 wanaowania taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2010.Udhamini huo unathamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja na hamsini (150,000,000/=).
Akithibitisha kudhamini Shindano hilo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kiromo View hotel and Resort,Ndugu James Nicolaus, alisema kuwa hoteli yao ni moja ya hoeli bora nchini,ambayo siku zote imekuwa mstali wa mbele katika kusaidia na kuchangia ukuaji wa Utalii,Michezo na Utamaduni nchin,kupitia kudhamini vikundi na matukio mabalimbali ya Michezo ikiwemo mashindano ya urembo nchini.
Lakini udhamini wa mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania 2010,ni mkubwa na tumesukumwa zaidi na malengo ya mashindano haya ya kutangaza,kukuza na kuendeleza Utalii na Utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimataifa.Tumesukumwa pia na mafanikio ambayo mashindano haya yamepata kitaifa na kimataifa katika muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita.
“Ni dhahiri Shindano hili kubwa kitaifa kufanyikia mkoani Pwani tena katika Wilaya yetu ya Bagamoyo,ni heshima kubwa kwa mkoa,wilaya na wananchi wote wa Mkoa huu,ambao ni miongoni mwa Mikoa michache nchini ambayo ina hazina kubwa ya vivutio vya Kitalii kama Hifadhi ya Taifa ya Saadani,Kitamaduni,kihistoria na fulsa nyingi za uwekezaji tangu katika sekta ya viwanda,kilimo na Utalii.
Ni matumaini yetu kuwa Shindano hili kufanyikia mkoani Pwani ,ni fulsa ya pekee ya kuonyesha na kutangaza vivutio vya Utalii,kitamaduni na mianya ya uwekezaji iliyopo mkoani Pwani na maeneo ya jirani.Hapa nichukue fulsa hii kutoa wito kwa wadau mabalimbali wa Utalii,Utamaduni,Uwekezaji , wafanyabiashara na makampuni mabalimbali binafsi na ya umma ya Ndani na nje ya mkoa wa Pwani kufuata nyayo zetu kwa kujitokeza kwa wingi kudhamini Mashindano haya ili yaweze kufana na kufikia malengo yaliyo kusudiwa”.
Akizungumza kwa niaba ya Miss Tourism Tanzania Organisation,ambao ndio wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo nchini,Raisi wa mashindano hayo Gideon E.G.Chipungahelo aliushukuru sana uongozi na wafanyakazi wa Kiromo Hotel kwa kudhamini Shindano hilo na kuahidi kwamba watafanya kila wanacho weza na kutumia kila tunacho weza kuitangaza hoteli hiyo kitaifa na kimataifa,na kwamba washiriki wa Miss Utalii Tanzania ,Daima watakuwa ni mabalozi wa kudumu wa hoteli hiyo ikiwa ni shukrani kwa udhamini huo.
Aidha aliahidi kuwa fainali hizo mwaka huu zitaendeshwa kwa ubora mkubwa na kwa viwango vya kimataifa,ili hatimaye washindi watakao patikana waweze kudumisha rekodi ya ushindi na heshima ya mashindano haya na Tanzania kimataifa.Washindi watawakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss United Nation 2011,Miss University Africa 2011,Miss Globe International 2011,International Miss Tourism Pageant 2011,Miss Tourism University world 2011,Miss Heritage world 2011, na Miss Tourism world 2011 .
Fainali za taifa mwaka huu zitafanyika wakati wa mkesha wa mwaka mpya Tarehe 31-12-2010,katika hoteli hiyo ya kitalii ya Kiromo Hetel,ambapo warembo 60 wenye mataji ya Mikoa,kanda na vyuo Vikuu wata wania nafasi za kuwakilisha Tanzania katika mashindano mabalimbali ya Dunia, kwa kutwaa Taji la taifa na tuzo mabalimbali za mashindano haya.
Tofauti na fainali zilizotangulia ambapo zilijikita katika kuhamasisha Utalii wa Ndani na uelewa wa Utalii kwa wananchi,mwaka huu fainali hizi zimejikita zaidi katika kutangaza Hifadhi za taifa,Utalii wa kitamaduni,Utalii wa ndani na Maeneo ya kihistoria kwa wananchi na Kimataifa,ili waweze kuvielewa vivutio hivyo,wavitembelee na hatimaye wavitangaze kitaifa na kimataifa,ili kupanua wigo wa kumfanya kila Mtanzania kuwa balozi wa Utalii na Utamaduni wa Tanzania

ahhh kaka chonya mbeya najua meno yote nje....mambo yamerudi tena!!
ReplyDeleteMkubwa mwenzangu,
ReplyDeleteVyumba shing. ngapi hapo kwani kule ulikotuambia tubofye tumebofya lakini hawajaweka bei za vyumba.
Pliiz