Marehemu Askofu Stephen Mwakasuka

Leo, tarehe 15/11/2010 imetimu miaka miwili tangu tulipoondokewa na mpendwa wetu Askofu Stephen Mwakasyuka.
Ni kweli kifo hakizoeleki, kwani sisi Watoto, Ndugu, Marafiki na Wapendwa wote tumejitahidi kuzoea hali ya kutokuwa na mtu muhimu huyu bila mafanikio.

Sisi, akina Phoebe, Florence, Jossey, Tungibwaga, Mponjoli, Atuganile, Frida, Salome, Gwakisa, Christian na Lazaro pamoja na wapendwa wote tunazidi kuliwazwa na imani kwamba ipo siku tutakuwa pamoja baada ya taabu zote za dunia kwisha.

“Nikasikia sauti ikitoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafaao katika Bwana tangu sasa. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” - Ufunuo 14: 13

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Poleni sana akina Atuganile na ndugu zako kwa kumpoteza baba. Namkumbuka Askofu Mwakasyuka alipokuwa pale Rungwe Mission na baadaye akahamia Lutengano. Kyala abhape amaka bho tukukumbuka ukufwa kwake "Mungu awape nguvu na faraja tunapokumbuka kifo chake" Ameni.

    ReplyDelete
  2. Tulikupenda sana Babu, lakini Mungu alikupenda zaidi.

    ReplyDelete
  3. Pole sana mpenzi dada Frida!

    Joe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...