MAREHEMU MAMA KANAELI EDWARD NTALIMA
Siku, miezi, miaka imepita na leo umetimiza Miaka 21 tangu Mwenyezi Mungu alipokuita kwake . Ilikuwa ni ngumu kuamini lakini hatimae ilikuwa hivyo. Tulikupenda sana lakini tunajifariji kuwa Mungu alikupenda zaidi yetu na pia uko kwenye pumziko la amani unaangaziwa na mwanga wa milele ukistarehe kwa amani japo haupo nasi kimwili ila kiroho upo nasi daima.
Unakumbukwa sana na watoto wako George,
Priscila na Matilda, Dada & Kaka zako, Wadogo zako, Wakwe, wajukuu zako.
Raha ya milele akupe ee Bwana,
na mwanga wa milele akuangazie,
upumzike kwa amani.
Amina
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...