Duka lenye vitu vya ukweli linalojulikana kwa jina la CHOCOLATE PRINCESS BOUTIQUE ambalo linapatikana pale Mikocheni kwa Mwalimu maeneo ya TALK OF THE TOWN limefungua blog mpya.

Jipatie vitu vya ukweli kwa bei nafuu kabisa kuanzia mavazi ya wakinadada pamoja na wakina kaka na watoto pia kwa kipindi hiki kinachokwenda kwenye sikukuu.

Tembelea blog ya duka hilo ili kujionea
vitu vinavyouzwa na uchague unachokipenda.
Wasiliana nao kwa simu namba:
+255 712 020272 / +255 773 787272
www.chocolateprincessboutique.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ungeweka basi price halafu siku vikiwa kwenye sale basi unapiga tarumbeta humu. Nimekwenda kwenye blog ninachoona ni picha tu. Sasa picha bila brand na price sijui ndio kibongo bongo lakini kama unatafuta na masoko kwenye mablog ni muhimu kuposti all the information...

    Mimi niko huku lakini kama ungeweka price na brand name ya vitu vyako labda ningependezwa na vitu kadhaa niwachukulie jammaa home kuliko kununua na kuposti...

    Sasa nyie mnaficha ficha price halafu mnatangaza kwenye blog sijui iweje..Tuvione tu au hutaki kuviuza? Tuambiane kwasababu kuna watu wengine wanafurahia kuona duka limejaa bila mteja

    Biashara ni matangazo lakini effective ad pia ni muhimu...

    ReplyDelete
  2. ndio maana kuna contact zao wasiliana nao, tatizo watu wakiwekaga bei mnaanza kudiscuss bei na hata kujidai huku dola moja huko mnauza bei iyo, mnasahau vitu vimependishwa ndege vimefushwa huku na ushuru vimelipiwa

    mkiwekewa brand . mnasema mh ya kichina iyoo aldo itakuwa iyoo

    tena nyie wabeba mabox ndio wa kwanza wewe nunua tu utume kwa nduguzo wabongo wenyewe tunajuana tunapiga simu au kwenda dukani

    NAWASILISHA

    ReplyDelete
  3. Hata mimi nimeliona hilo maana nimeingia katika hiyo blog all i see ni bidhaa bila price, lakini sishangai sana mana ndio tabia ya wabongo wanatangaza biashara halafu hawasemi bei wanasema tu bei nafuu!! Mboni na wenzio wote wenye maduka na mmefungua blogs make sure unaweka prices watu wajue ni how much na vinatoka wapi plus name brands..mana mnatuuzia vitu vya PRIMARK NA ATMOSPHERE ambavyo mnanunua kwa Pound 3/4 alafu mnatuuzia laki mbili kiatu na vitop na magauni ya pond 5 mnatuuzia elfu 70...

    ReplyDelete
  4. mdau hapo juu,ulitaka gauni la pound 5 aliuze bei gani? kumbuka kuna kusafirisha, kulipia ushuru, rent ya duka na kulipa mfanyakazi,inatoka humohumo kwenye pound ulitaka liuzwe bei gani?hata hiyo elf 70 uliyoitaja ni ndogo, hiyo ndo bei nayo uzia mimi mfanyabiashara wa mkononi tuu,gauni pound 5 nikilishusha bongo elf 70, sasa huyo mwenye duka jee?

    ReplyDelete
  5. Mashauzi tu weka bei watu tujue

    ReplyDelete
  6. Shosty mkielezwa ukweli mnayapa yapa...Badilikeni shukuru tangaza kwa michuzi ni free lakini ungelipia hili tangazo basi ungeula wa chuya. Mkielezwa ukweli mnabakia kusema hivi vile...wanaosema kuhusu bei uliyoipanga ni kama kelele za mlango tu. Wewe weka bei na maelezo yote utapata wateja wanaoafford kununua hivyo vitu vyako otherwise good luck kwa vile matangazo ya bongo ni kazi sana.

    ReplyDelete
  7. Vip naweza pia kupata Contact ya huyo Binti kwenye tangazo ? Ana Ka HIPS....Dah.

    ReplyDelete
  8. Ushauri wa bure angalia Amazon kuna bei, wekja bei watu wajue kama wana walk in or not

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...