Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Shariff Hamad akiwatangazia wafuasi wake waondoke eneo la Bwani Hoteli yalikokuwa yakitangazwa matokeo ya uchaguzi ambapo hatimaye waliondoka kwa amani baada ya kusota eneo hilo tangu asubuhi. Baadaye Maalim Seif alirejea kusikiliza matokeo eneo hilo kukiwa na utulivu na amani ikiashiria sasa Zenji mambo mswano na kwamba Zanzibar mpya itayokuwa na serikali ya kitaifa imezaliwa. Picha na Bashir Nkoromo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hapo si amani bali ni kuwa Maalim kaona ndiyo anaelekea lala salama walau aambulie umakamu wa Rais!

    ReplyDelete
  2. kitu gani bwana? hata mi ningepaza sauti kuwaambia waondoke, umakamu wa raisi sio mchezo bwana.... kuku kwa mrija kila mwezi uko kwenye swissair kwenda kula bata. Mwacheni mwanangu ale matunda ya muafaka

    ReplyDelete
  3. Kwa watu makini wanaoitakia Zanzibar mema. Kauli nyingine ambazo hazijengi zaidi ya kubeza hazisadii kitu Zanzibar.

    Rejeeni Kauli ya JK alipokuwa akilihutubia Bunge mara tu alipoingia madarakani.

    Hongera Dk. Shein na Hongera Maalim Seif. Wanaobeza walikuwa wananufaika na siasa za mfarakano. tuwabaini na tuwakatae.
    Ankali kuwa makini.

    ReplyDelete
  4. Kama ilivyokuwa zimbabwe na kenya, viongozi wa upinzani wanapoahidiwa fupa basi upinzani huwa unakwisha.

    Hiyo ndio proof kuwa upinzani wao wote sio kwa ajili ya wafuasi wao bali ni kwa manufaa yao.

    Subirini tu mtaona ahadi zote alizokuwa akiweka hazitotimizwa sasa kashapata fupa. Siasa za afrika bwana!!!!

    ReplyDelete
  5. Salaam Ankal mithupu...

    Naomba niseme kuwa Seif HAmad ameniinspire, na laiti kama ningekuwa Zanzibar basi ningependa sana nimshike walau mkono , kwa kweli Seif ni SHUJAA anaefaa kupongezwa na kuigwa, mimi ni Mbara halisi kwetu ni pale Kunduchi Pwani, lakini nimemfurahia Seif kwa sababu hakuwa mbinafsi, amewafikiria sana watu wa Zanzibar and he did that for the blood of the people of Zanzibar, kwa sababu laiti kama angesema hakubali matokeo basi leo hii tungeshuhudia umwagaji wadamu kama ule wa chaguzi zilizopita nyuma, lakini amekubali matokea na amewasihi watu wake watulie, na hakufanya hivyo kwa kuwa anataka kula bata! kwa sababu hata kabla bata alikuwa anakula mara ngapi tumesikia Seif yupo Uk, mara ughaibuni etc, lakini kwasababu swalazima linawagusa wazanzibari na sio wabara! waacheni wajiamulie kufanya wanayoyaona yanawafaa wao na kamwe msiwabeze! HONGERA SANA MAALIM SEIF, WEWE NI KIDUME NA UNAFAA KUIGWA KATIKA NYANJA ZOTE,.,..NAWAOMBEA KWA ALLAH SUB-HANA WA TAALA AWAWEZESHE KUONGOZA KATIKA HII SERIKALI MPYA YA MSETO KWA UADILIFU WA HALI YA JUU NA NAAMINI MTAWEZA ..., MUNGU IBARIKI ZANZIBAR MUNGU IBARIKI TANGANYIKA

    ReplyDelete
  6. BIG UP SEIF
    WAZANZIBAR NDIYO TUNAJUA UMASIKINI TULIOUPATA KUTOKANA NA VURUGU ZA MIAKA YOTE ILIYOPITA.

    ReplyDelete
  7. Sasa Maalim ukishapewa umakamo utawashuhulikia wale waliowaonea wenziwao huko nyuma, kwa kuwapiga na kuwadhulumu mengi tu kwa sababu za vyama wanavyo support? i am not holding my breath.

    Yametokea kenya na zimbabwe, viongozi wa wapinzani walipopewa umakamo wamewasahau wanachama wao na mentality zao zimekuwa sawa na watawala wakuu. na mmalim naamini atakuwa vivo hivyo.

    Cha kushukuru ni kuwa uchaguzi umeisha kwa salama na bila ya watu kupoteza maisha yao, mengine ni PUNDA YULE YULE, LILOBADILIKA NI SOJI!!!

    ReplyDelete
  8. Maalim hongera kwa maamuzi ya busara japo umeshinda ila hakuna shida ilimradi amani ipo. Iko siku tutafika tu.

    ReplyDelete
  9. Dili zilizofanywa kati ya ccm na Maalim Seif zinamaanisha kuwa Demokrasia haitakuja kuja Zanzibar hivi karibuni. Kwa nini serikali ya mseto? Ni muhimu matokeo ya uchaguzi yaheshimiwe na chama kilichoshinda kiunde serikali na sio kutangaza serikali ya mseto kabla hata ya uchaguzi. what's the point of spending money for elections then?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...