NDUGU MICHUZI NA WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA JAMII. NAOMBA MNISAIDIE KUMTAFUTA BABA YANGU MPENZI KWA JINA ANAEJULIKANA LA AMARI ADAM SALIM AMBAE ALIONDOKA NYUMBANI TANZANIA KATIKA MIAKA 25 ILIYOPITA KUELEKEA NCHI ZA ULAYA.
HAIJULIKANI ULAYA GANI ALIYOKWENDA ISIPOKUWA MARA YA MWISHO ALIWASILIANA NA BABA YAKE (BABU YANGU) AKIWA NCHINI UTURUKI MIAKA KUMI NA TANO ILIYOPITA.
BABA YAKE (BABU) MZEE ADAM SALIM YUKO HAI NA ANAISHI DAR ES SALAAM. BWANA AMARI ANAKUMBUKWA SANA NA FAMILIA YAKE HASA BABA YAKE MZAZI ANAMKUMBUKA KWA MAJONZI MAKUBWA SANA.
TUNAOMBA MTU YOYOTE AMBAE ANAEJUA TAARIFA ZAKE AU ANAJUA ALIPO TUSAIDIE KWA KUWASILIANO. SAFARI HII NIMEAMBATANISHA PICHA IWEZE KUSAIDIA. SIO NZURI SANA ILA NDIYO NILIYONAYO KWA SASA.
SAKI-07759745334 UK
Email saki.adam@yahoo.co.uk
SAKI-07759745334 UK
Email saki.adam@yahoo.co.uk
Ndugu yangu Saki ungeomba balozi zetu ziulizie na jela za huko ughaibuni maana nahisi ingawa sina hakika sana kuwa baba yako alizamia nje kutafuta maisha. Tujaalie kuwa haitakuwa Iran au Saudia maana kama ni nchi hizo ujue mengine
ReplyDeletePole sana Saki, ila hiyo picha haionekani na jina inawezekana ameshabadili, njoo uwe mwanagu tu!!
ReplyDeletepole sana ndg yang huyu mkamtafute uturuki,kwani ndiko kuna wazee wengi sana waamiaji kule,nahata juzi nimetoka huko kuna wazee wengi sana wa kizenji na wakibongo na nilijaribu kuongea na mmoja jina kapuni akasema ana mwaka huu wa kumi na tano yupo huko hawjui ndg zake mwaka huu wa kumi na tano na wengine ni ombaomba
ReplyDeletesiyo Omari mesco huyu kweli?
ReplyDelete