Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu, Novemba 29, 2010, amemtembelea hospitali na kumjulia hali mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, Bwana Muhidin Gurumo, ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Bw. Gurumo ambaye amelazwa Wodi Mosi, Mwaisela, amekuwa hospitalini hapo tokea Alhamisi iliyopita, Novemba 25, 2010, akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Rais Kikwete amekaa na mwanamuziki huyo kwa kiasi cha dakika 15 na baadaye madaktari bingwa wa moyo wa MNH wamethibitisha kuwa hali ya Bw. Gurumo imetulia na kuwa akiendelea na hali ya sasa anaweza kutolewa hospitali wiki ijayo.
Rais Kikwete ambaye baada ya kumjulia hali Bw. Gurumo alitaka kumtembelea na kumjulia hali mwanamuziki mwingine, Bw. Remmy Ongala, ambaye naye amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matatizo ya figo.
Hata hivyo, Rais Kikwete amejulishwa kuwa Bw. Ongala wakati huo alikuwa nje ya wodi yake kwa ajili ya kufanyiwa vipimo katika sehemu nyingine ya hospitali hiyo. Bw. Ongala naye amelazwa Wodi ya Sita, Mwaisela hiyo hiyo.
Kwa miaka mingi, wanamuziki hao wawili wenye vipaji vikubwa vya muziki wametamba katika muziki wa Tanzania. Bw. Gurumo amekuwa nyota wa muziki katika Tanzania tokea miaka ya 1960 na amepigia ama kuongoza baadhi ya bendi maarufu za muziki katika Tanzania zikiwamo za NUTA (baadaye JUWATA na OTTU) ambayo sasa inaitwa Msondo Ngoma Music Band, Orchestra Safari Sound (OSS) na DDC Mlimani Park (Sikinde).
Naye Ongala kwa miaka mingi aliongoza bendi ya Super Matimila, kabla ya kuingia katika muziki wa Gospel.
Mola atamsaidia na kumwafu, kumpa afya na uzima na kuendeleza tena Libeneke la Msondo.
ReplyDeleteTuko pamoja nae kwa kila aina ya dua.
Ewe Mola wetu tubariki kwa dua letu!
Amina.
Jabali pekee la mziki (kwa wanaofanyia kazi muziki wa nyumbani) aliyebaki,Mungu atamsaidia afya njema na kurudi kundini.
ReplyDeleteZAUNUNU
Inshallah mwenyezimungu atampa nguvu, Ila Ushauri wangu Mzee wetu wa Muziki huyu ni Mtu mzima sana najuwa watu watasema watu wazima wengi wanaimba bado, ila bora apumzike atulie ni muda wakufanya Ibada mwenyezimungu anakupenda zaidi ndomana anakupa mitihani na mitihani mengine inakuwa mizuri kwa binadamu. Kutoka kwa M.
ReplyDeleteDr. Michuzi Asante sana kwa habari hizi nzuri. Mungu amlinde kamanda wetu Wa ukweli.
ReplyDeleteMwacheni baba wa watu aimbe muziki wake, kwa wasiojua muziki ni rahisi sana kusema kile ni kiburudisho cha moyo.
ReplyDeleteSuala nisilo lipenda ni hilo la kusaula nguo wagonjwa ama ni kwa ajili ya joto au uniform hazijakauka? mbona shughuli!
Pole sana mzee wetu
ReplyDeleteTunakuomba Mungu uliyembinguni umpe nafuu na hatimae kupona kabisa mzee wetu Maalim Ngurumo, mzee wa Masaki, Ameen.
ReplyDeleteAliii... Mwanazanzibar
MZEE WA MSONDO
Mwenyenzi Mungu akupe nafuu ya haraka upone urudi kwa familia kuliendeleza taifa letu Pokea uponyaji kwa jina la Yesu Amen
ReplyDeleteTunakuombea kwa Mungu,utapona tu, na utarudi kwenye shuguli zako kama kawaida.
ReplyDeletePole sana mtaalamu, sasa mjomba inabidi apumzike aanze kuwaongoza na kuwafundisha vijana kupiga muziki. Kupanda jukwaaani na siku nyingine usiku wa manane nadhani kwa umri huo haifai tena.
ReplyDeleteKamanda Gurumo tunakuombea Mola atakupa afueni tunakumiss sana TCC Chang'ombe
ReplyDeleteankal jaribu kuulizia ulizia hapo BITCHUKA kaja kumjulia hali kamanda?si unajua kipindi kile mara nginde,mara ndekule kote huko walikua pamoja.bitchuka sauti ya mwanzo kamanda anamaliza sauti ya mwisho.hasa wimbo huu: kaka kinyogoli nakushukuru kwa yote ulionitendeaaa...niliposafiri ng'ambo watoto wangu uliwaangaliaaa....kwaio wewe sio rafiki bali ni ndugu wa niaaa.
ReplyDelete