Mwanamuziki wa siku nyingi Mzee Makasy akimjulia hali mwanamuziki mwenzie Muhidin Maalim Gurumo (KAMANDA) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili. Uncle Gurumo yupo wodi ya Mwaisela namba 1 kwa sasa baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kunradhi kwa picha haionekani vizuri.Picha na mdau Rajab Mhamila.

Globu ya Jamii inamtakia Kamanda Gurumo nafuu ya haraka na inatoa wito kwa wapenzi wa muziki kujitokeza kumsaidia mzee wetu huyu ambaye ni mmoja wa wanamuziki wachache waliosalia wakiendeleza fani kwa weledi wa hali ya juu huku ukikuza vipaji vipya kwa wakati huo huo.

Wakati huo huo, Rais

Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu, Novemba 29, 2010, amemtembelea hospitali na kumjulia hali mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, Bwana Muhidin Gurumo, ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Bw. Gurumo ambaye amelazwa Wodi Mosi, Mwaisela, amekuwa hospitalini hapo tokea Alhamisi iliyopita, Novemba 25, 2010, akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Rais Kikwete amekaa na mwanamuziki huyo kwa kiasi cha dakika 15 na baadaye madaktari bingwa wa moyo wa MNH wamethibitisha kuwa hali ya Bw. Gurumo imetulia na kuwa akiendelea na hali ya sasa anaweza kutolewa hospitali wiki ijayo.

Rais Kikwete ambaye baada ya kumjulia hali Bw. Gurumo alitaka kumtembelea na kumjulia hali mwanamuziki mwingine, Bw. Remmy Ongala, ambaye naye amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matatizo ya figo.

Hata hivyo, Rais Kikwete amejulishwa kuwa Bw. Ongala wakati huo alikuwa nje ya wodi yake kwa ajili ya kufanyiwa vipimo katika sehemu nyingine ya hospitali hiyo. Bw. Ongala naye amelazwa Wodi ya Sita, Mwaisela hiyo hiyo.

Kwa miaka mingi, wanamuziki hao wawili wenye vipaji vikubwa vya muziki wametamba katika muziki wa Tanzania. Bw. Gurumo amekuwa nyota wa muziki katika Tanzania tokea miaka ya 1960 na amepigia ama kuongoza baadhi ya bendi maarufu za muziki katika Tanzania zikiwamo za NUTA (baadaye JUWATA na OTTU) ambayo sasa inaitwa Msondo Ngoma Music Band, Orchestra Safari Sound (OSS) na DDC Mlimani Park (Sikinde).

Naye Ongala kwa miaka mingi aliongoza bendi ya Super Matimila, kabla ya kuingia katika muziki wa Gospel.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mola atamsaidia na kumwafu, kumpa afya na uzima na kuendeleza tena Libeneke la Msondo.
    Tuko pamoja nae kwa kila aina ya dua.
    Ewe Mola wetu tubariki kwa dua letu!
    Amina.

    ReplyDelete
  2. Jabali pekee la mziki (kwa wanaofanyia kazi muziki wa nyumbani) aliyebaki,Mungu atamsaidia afya njema na kurudi kundini.

    ZAUNUNU

    ReplyDelete
  3. Inshallah mwenyezimungu atampa nguvu, Ila Ushauri wangu Mzee wetu wa Muziki huyu ni Mtu mzima sana najuwa watu watasema watu wazima wengi wanaimba bado, ila bora apumzike atulie ni muda wakufanya Ibada mwenyezimungu anakupenda zaidi ndomana anakupa mitihani na mitihani mengine inakuwa mizuri kwa binadamu. Kutoka kwa M.

    ReplyDelete
  4. Dr. Michuzi Asante sana kwa habari hizi nzuri. Mungu amlinde kamanda wetu Wa ukweli.

    ReplyDelete
  5. Mwacheni baba wa watu aimbe muziki wake, kwa wasiojua muziki ni rahisi sana kusema kile ni kiburudisho cha moyo.
    Suala nisilo lipenda ni hilo la kusaula nguo wagonjwa ama ni kwa ajili ya joto au uniform hazijakauka? mbona shughuli!

    ReplyDelete
  6. Pole sana mzee wetu

    ReplyDelete
  7. Tunakuomba Mungu uliyembinguni umpe nafuu na hatimae kupona kabisa mzee wetu Maalim Ngurumo, mzee wa Masaki, Ameen.

    Aliii... Mwanazanzibar
    MZEE WA MSONDO

    ReplyDelete
  8. Mwenyenzi Mungu akupe nafuu ya haraka upone urudi kwa familia kuliendeleza taifa letu Pokea uponyaji kwa jina la Yesu Amen

    ReplyDelete
  9. Tunakuombea kwa Mungu,utapona tu, na utarudi kwenye shuguli zako kama kawaida.

    ReplyDelete
  10. Pole sana mtaalamu, sasa mjomba inabidi apumzike aanze kuwaongoza na kuwafundisha vijana kupiga muziki. Kupanda jukwaaani na siku nyingine usiku wa manane nadhani kwa umri huo haifai tena.

    ReplyDelete
  11. Kamanda Gurumo tunakuombea Mola atakupa afueni tunakumiss sana TCC Chang'ombe

    ReplyDelete
  12. ankal jaribu kuulizia ulizia hapo BITCHUKA kaja kumjulia hali kamanda?si unajua kipindi kile mara nginde,mara ndekule kote huko walikua pamoja.bitchuka sauti ya mwanzo kamanda anamaliza sauti ya mwisho.hasa wimbo huu: kaka kinyogoli nakushukuru kwa yote ulionitendeaaa...niliposafiri ng'ambo watoto wangu uliwaangaliaaa....kwaio wewe sio rafiki bali ni ndugu wa niaaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...