Klabu ya Maveterani wa Mpira wa Kikapu (OLD GUARDS) ya jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuondoka Jumamosi tarehe 27.11.2010 kuelekea jijini Tanga kushiriki Bonanza la siku moja katika kundeleza ujirani mwema na kuhamasisha ukuaji wa Mchezo huo hapa nchini. Ikiwa Mjini Tanga itacheza na klabu za maveterani za mkoa wa Tanga, Arusha na Kilimanjaro

Pamoja na Michezo hiyo, Klabu ya Old Guards ikiwa Tanga itashiriki katika shughuli zingine za kijamii kwa mujibu ya ratiba itakayopangwa na wenyeji ambao ni Klabu ya Tanga Old Guards.

Tunawashukuru Kampuni ya GAPCO kwa udhamini wao wa kusafirisha Timu za Maveterani kwenda kwenye Bonanza hilo na tunaendelea kuongea na wadhamini wengine mbalimbali ili kufanikisha Bonanza hili

Ahsanteni

Lawrence Cheyo
- Mratibu wa Bonanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...