Watch live video from cvkvideo on Justin.tv
Alex Kajumulo 'Babu Kaju' na bendi yake ya Mabush Man akiwajibika katika show aliyofanya kwenye mkesha wa Thanks giving kupambana na ugonjwa hatari wa maralia jijini Seattle katika ukumbi wa Tripple Door. Show hio ilirushwa live katika TV kadhaa na kuangaliwa na mamilioni ya watu sehemu mbalimbali duniani

mpiga kinanda wa Bush Man Band akila mzigo
Show ilipigwa live na vituo kadhaa vya TV
DJ Catundu akiwa mitamboni wakifanikisha show na mtaalamu mwenzie
Ukumbi wa Triple Door jijini Seattle ulifurika

TO ALL MY FANS WORLDWIDE, ONE MILLION VIEWERS ON THE INTERNET WORLWIDE AND 125,000 VIEWERS ON LOCAL CABLE IN THE GREATER SEATTLE AREA, THANKS VERY MUCH FOR WATCHING MY SHOW. I WOULD LIKE TO THANK SCANTV FOR GIVING ME THE CHANCE TO SHARE MY MUSIC WITH YOU. FOR THOSE WHO LOVE MY MUSIC, YOU CAN BUY MY SONGS ON I-TUNES, AMAZON, ZUNE, CDBABY, AND ANYWHERE DIGITAL MUSIC IS SOLD. WE WILL BE RELEASING A DVD VIDEO AND CD COMBO WITH THE LIVE SHOW SOON. IF YOU ARE INTERESTED, PLEASE GO TO WWW.BABUKAJU.COM
AND JOIN MY EMAIL LIST. REMEMBER: ONENESS IS TOGETHERNESS. PEACE.
ALEX

Here is the link for the Malaria is Dangerous live concert video.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Not Dj Catundu but he`s Dj Katunda and his name is Idriss Katunda.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  2. Alex kajumulo pamoja na weakness ya majisifu na mwembwe zake za ufahari,huyu jamaa namkubali vision yake with a full determination,yupo smart katika initiation za project zake,kama mutamkumbuka hakuwa mchezaji mzuri katika mpira lakini alijitangaza kiasi cha kuchanganywa na abroad media kuwa yeye ni mchezaji bora wa Africa,na sasa yupo katika mziki na utaniambia sasa hivi atatajwa kwenye nomination za best African musician
    big up bro,hivi ndivyo watu wanapaa,ila pia jitahidi kuitangaza tangaza nchi yako katika music wako.
    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni wa Istanbul wewe ni mtu husiyemfahamu Alex kwani huyu jamaa siyo mtu wa kujisifu na mbwembwe, huyu ni mtu wa kujichanganya na mtafuta hela mzuri sana kwani project za mpira Tanzania yeye alichokuwa anatafuta kujulikana Africa kama agent suala ambalo alilifanya na kumwezesha kuuza wachezaji kutoka pale nyumbani na Ghana, na huyu jamaa amekaa na wazungu muda mrefu bila kuwa mwalifu kama nyie vijana wa siku hizi mkishakwenda marekani mnafanya wizi wa kadi za benki, magari na kwenye viwanda tabia hizi zitakufanya jamii ya wazungu wakuogope lakini kajumulo yeye ni mwenzao kwani yeye anafanya nao kazi, akisema Ariginal sound inashow wazungu wanafika, lakini vijana wasiku hizi nyie mnapanga kuiba kwa wazungu hata wazee mnakofanya care. Hongera sana kajumulo niliangalai hii show live kupitia internet ilikuwa kali. Kuhusu kutangaza nyumbani amekuwa akifanya hivyo uniform za bendi zina bendera ya Taifa, na ukisikiliza mziki wake wa global warming unahusu mlima kilimanjaro.

    ReplyDelete
  4. Tarehe Sat Nov 27, 04:22:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    wewe mzushi , mbona una sifia kwama mwenyewe vile. unajifagilia wazi wazi,
    kwa mimi nakubali jamaa mtafutaji, hila naona anamwelekeo jana tu alikuwa kafunika tanzania kama sponsor wa mpira wa miguu. wakati hule hata angegombea ubunge angepata. kwa jinsi watu walivyo jua jamaa ana mpunga sana. Sasa hivi yuko wapi anaimba eti music , music wenyewe ajuhi kuimba , mtu mzima anajitia haibu tu , kwa umri wake na alipo kuwepo asingekuwa anakimbizana kimbizana na bendi , eti bush man . LOL

    ReplyDelete
  5. Vijana wakitanzania hakuna lolote mnajua kwani mlivyokuja ulaya na america nyie mnatoboa masikio bila kukjua ni skio lipi la wanaume na mashoga, kumbuka ni watu wangapi watachangia malaria kutoka kwenye show hii? kajumulo anafundisha mpira vijana kama mia mbili hivi kwa mwezi kila kijana analipa dola mia mbili hii shilingi ngapi? na huyu jamaa ana biashara nyingi kwani huyu ni mtu anazungumza na wazungu kwani last tiome nilikuwa naye Uk alikuwa kwenye mikutano ya biashara. Ndugu zangu nyie waosha vinywa nani kachangia kitu nchi yake Tanzania? mmebaki kelele tu.Mpira Tanzania ilikuwa kujitangaza ndiyo maana mnamjua Kajumulo, je kani kasoma vitabu vyake huyu mtunzi na ana vitabu, vijana fanyakazi wacha kuja ulaya kuoa wanawake ili mpate makaratasi.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...